Haya maandamano ni ya muhimu sana na lazma yasukumwe sana na watu ambao mna access na wananchi both online and on the ground.
Watanzania no one is coming to save us. Lazma tujipiganie wenyewe. We have to fight for a new constitution, Tundu Lissu’s freedom, accountability for October 29 massacre. and we have to fight for new free and fair election.
International pressure itasaidia mauwaji kuogopa kuua tena ila the rest of the work Lazma tufaye wenyewe.
KWAKUWA NI HALALI KWA WAZANZIBARI KULINDA HAKI ZA WAZANZIBARI HAIWEZI KUWA HARAMU KWA WATANGANYIKA KULINDA HAKI ZA WATANGANYIKA.
Kwa yanayoendelea kujitokeza katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuhusu kujitanabaisha kwa misingi ya Uzanzibari na kulinda maslahi ya Zanzibar, je, si wakati sasa kwa Watanganyika nao kuzungumza kwa uwazi, kuhoji kwa uhalali na kujadili kwa kina masuala yanayohusu haki, hadhi na maslahi ya Tanganyika?
Je, Watanganyika hawana haki ya kuhoji na kulinda:
1. Bandari zilizopo ndani ya Tanganyika.
2. Misitu na rasilimali za mazingira za Tanganyika.
3. Rasilimali za asili zilizopo katika eneo la Tanganyika.
4. Hadhi, haki na umiliki wa ardhi ya Tanganyika.
5. Nafasi, haki na uwepo wa watu wasio Watanganyika katika idara na taasisi ambazo si za Muungano.
6. Uhalali wa viongozi wasio Watanganyika kuingia au kusaini mikataba inayohusu rasilimali za Tanganyika, hususan pale ambapo baadhi ya masuala hayo tayari yameondolewa katika eneo la Muungano kwa upande wa Zanzibar.
7.Kuhoji mchango wa Zanzibar katika kugharimia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano na Ulipwaji wa Deni la Taifa.
Ikiwa ni halali kwa Wazanzibari kujadili, kuhoji na kulinda maslahi ya Zanzibar kwa misingi ya utambulisho wao wa kisiasa na kikatiba, kwa mantiki hiyo hiyo haipaswi kuwa kosa kwa Watanganyika kuhoji, kujadili na kutetea maslahi ya Tanganyika.
Katika mfumo wowote wa haki, usawa na kuheshimiana ndani ya Muungano, haki ya kulinda maslahi ya Zanzibar haiwezi kutenganishwa na haki ya Watanganyika kulinda maslahi ya Tanganyika.
Haki hizo zinapaswa kutambuliwa kwa usawa, bila upendeleo na bila kuonekana kuwa ni tishio kwa Muungano, bali kama sehemu ya kujenga Muungano wenye misingi ya haki, uwazi na kuheshimiana.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI ndiyo Msingi bora wa kuliongoza Taifa kutoka katika vitendo vya Ukatili dhidi ya ubinadamu,ukiukwaji wa Haki za Raia na,Mauwaji na Utekaji vilivyofanyika kanla,wakati na Baada ya Tarehe 29 Oktoba 2026.
BAK MWABUKUSI.
Maandamano ya 7/7 yalioandaliwa na GEN Z binafsi nayaunga mkono asilimia mia mbili.
Kiuhalisia naona 7/7 yenyewe inachelewa kufika. Watu hawajazika wapendwa wao mpaka leo ni miezi 7 wanaomboleza hakuna MAJIBU KUTOKA Kwa wakoloni weusi.
Watanzania bado wanaendelea KUTEKWA NA KUPOTEZWA kila siku—wengine wakiwapata wapendwa zao wanawakuta hawana VICHWA wanazika kiwiliwili na hakuna majibu kutoka kwa WAKOLONI WEUSI.
TUNDU LISSU bado yupo jela na hakuna KESI dhidi yake zaidi ya siku 400 sasa, na wakoloni weusi wapo KIMYA tuu ni kama wanaona wanatumudu.
Haya maumivu tunayopitia watanzania lazima wajue tunaumia na sauti yetu lazima waisikie.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inafanya kazi ya kuchochea machafuko.
Sisty Nyahoza aliekwenda kwa marehemu mama Komu na kumshawishi kusaini karatasi ya kufungua kesi ambayo ilifungia chama chetu kufanya kazi siku 309..
Madhara mengine walitaka kukifuta chama kupitia kesi hiyo ya Said Issa.. kwa uwezo wa Mungu tumeshinda..
Sasa Sisty huyo huyo na ofisi hiyo hiyo ambayo inafanya kazi ya kuhujumu chadema usiku na mchana tena wazi kabisa. Inatuandikia barua kila baada ya mkutano na kila neno tunalosema… Maneno pekee tunayoweza kusema tusiandikiwe barua na Sisty ni kumsifia Samia na serikali yake dhalimu ambayo haikuchaguliwa.
Kwa kifupi ofisi ya msajili itaingiza Nchi hii kwenye machafuko ya kisiasa..
Chadema ni taasisi ya Watanzania na Watanzania watailinda dhidi ya hujuma zote.
Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam leo, Alhamisi Mei 28, 2026 imeifuta rasmi na kuiondoa mahakamani hati ya kesi ya madai iliyofunguliwa na kiumbe aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Issa Mohammed na wenzake dhidi ya bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, iliyokuwa inahusu usawa katika mgawanyo wa mali za chama kati ya Tanganyika na Zanzibar.
NB; Kesi hii ndiyo MaCCM waliotumia kuzuia shughuli za CHADEMA kwa siku 310.
MADURO anasema waliua waandamanaji kwa kuwa walibeba silaha za moto na kuua askari. KOMBO anasema waandamanaji waliuwawa kwa risasi kwa sababu waliwatupia mawe askari. MaCCM kaeni kitako na mkubaliane kutoka na uongo unaofanana kwanini mliwaua waandamanaji kwa risasi za moto.
Kuendelea kumshikilia Tundu Lissu 👇 GEREZANI kwa kesi ya UONGO, ni KUITHIBITISHIA DUNIA, kwamba; Tanzania ni laifa la watu WENDAWAZIMU, yaani, WALIOPUNGUKIWA AKILI. Someni BIBLIA katika kitabu cha MITHALI 28:16
Huyu Bwana Kombo anazidi kuthibitisha kwamba waliua watu bila sababu ya msingi… Chande alisema kulikua na training na silaha , kombo anasema mawe!!! anasema ukimlembea jiwe polisi, anatakiwa kukupiga risasi..
Je Bwana Kombo yule mama Mtanganyika pale Arusha, Video yake Inaonekana anakimbia , akapigwa risasi mgongoni, alilemba jiwe kwa nani?
Watu wameuwawa wakiwa nje ya Mageti ya nyumba zao, wengine kwenye sebule , kuna vijana Mwanza mmeaua wakiwa wanaangali Mpira…
Unasema tumeheal!!!! Hamtaweza kufukia mauaji ya kutisha mliyofanya ili mjitangaze kwenye uchaguzi ambao haukuwepo… wote mnakula pesa za damu na dunia haitakaa kimya.