Regardless of the court’s decision, the man went to war, using nothing but his intellect to fight for his rights and challenge the system. This final submission deserves to be studied in schools.
*MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISU, leo:*
“Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo, "I have fought against white domination and I have fought against blood domination, and my Lords, it is an ideal I am prepared to die for"
Nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa.
Namalziia kwa neno moja:
waheshimiwa majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni
kuamua kama kwa ushahdii huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should not hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope, kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini
msiogope kuniachia huru.
You have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo, hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesn't fit— acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji. Nimemaliza”
Tundu Antiphas Lissu, September 28, 2026. Mahakama Kuu, Dar.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 470
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
d) Wamekaa Mapolisi wanadanganyana hawajui sheria mambumbumbu hawana mwanasheria hata mmoja wanatengeneza kosa. Ukurasa wa 158 wa Record ya Mahakama PW 1 ametaja majina ya timu yake na orodha ya mashahidi wake.
Kwa akili yote hii kesi ilitokea kwa PW 1 George Bagyemu.
The investigation included ASP Gyumi, Mwakabongo, Numbu, Ibrahim, Ramadhani. Hiyo ndio timu ya upelelezi ambayo wote ni Mapolisi tu hapo.
PW 1 baada ya kugundua kuwa hii habari ya kutomshirikisha DPP alibadilisha msimamo akala matapishi yake.
He contradicted himself, page 169 akasema yafuatayo "The chief investigator Amin Mahamba was the one who reported to the DPP by the time I opened the file I did not report officially to DPP.” Na anadai DPP alikuwa anajua hiyo habari maana aliambiwa na Amin Mahamba.
e) PW 1 hakuhusisha wala kutoa taarifa kwa mamlaka nyingine yoyote ya kiuchunguzi wala kiserikali kuhusiana na hilo file la Uhaini.
He did not involve or report to any other government authority about the open up of the treason file na hapa namaanisha sio kesi ya Maembe ni kesi ha Uhaini.
Ushahidi unasemaje?
Ukurasa wa 170 wa record unasema treason ni kosa kubwa sana na pia linahusisha na watu wa TISS na sikuwahi kuzungumza na Mkurugenzi wa TISS kuhusu mambo haya ya Uhaini na sijui kama TISS walipewa taarifa kuhusu kesi hii ya Uhaini.
Anakubali kabisa kwamba kesi ya Uhaini ni kubwa sana lakini anasema sijawahi kuwasiliana sio tu na Mkurugenzi Mkuu wa TISS bali hata Mkuu wa Usalama wa Mkoa wa Dar es salaam kwasababu sio kazi yangu kujulisha.
Sasa Waheshimiwa Majaji kesi kubwa kuliko zote kwenye Jamhuri halafu huyu Polisi anasema hajawahi kuwasiliana na watu wanaohusika na usalama wa nchi hii. Huo ndio ushahidi mnaotizamiwa muukubali mtoe adhabu ya kifo.
Waheshimiwa Majaji haya ambayo nimeyasema hadi hapo kuhusu PW1 katika haya maeneo manne haukuwa clarified kwenye Re-examination na hakuna aliyemuomba afanye clarification angalia ukurasa wa 176 wa record.
Hakuna clarification yoyote kwahiyo maana yake wameukubali na wanategemea Mahakama ikubali kwamba kuna Uhaini na itoe hukumu ya kifo.
Sasa hayo ndo aliyoyafanya PW 1 siku nne za kwanza za kosa hadi Tarehe 08.
Sasa twende kwa Amin Mahamba ambae alikuwa Mkuu wa Upelelezi kuanzia Tarehe 08/04.
The first remarkable thing about PW 16 is that aliimeza hadhithi ya PW 1 hook, line and sinker. Hilo ndio jambo la kwanza, alikubali kila kitu alichoambiwa na George Bagyemu.
Kitu cha pili nilisema juu ya Confusion juu ya kesi ya Upande wa Mashitaka kwa maana ya Confusion kwa mfano PW 16 flattered contradicted about the composition of the investigation team.
Ni lugha gongana kabisa kati ya PW 16 NA PW 1, ukurasa wa 460 PW 16 anasema yafuatayo: The investigation analysis and legal advisory team comprises PW 1 and another officer from DPP office.
Hao watu hawakusema kama walimjulisha DPP na ghafla team ilikuwa na muwakilishi kutoka office ya DPP hakutajwa jina na hakuna aliyekuja kutoa ushahidi hapa Mahakamani.
Of course tofauti kati ya PW 1 na PW 16 wanatoa ushahidi ulikuwa ni muda umepita PW 1 aliwahi kutoa ushahidi na baadae PW 16 ndio akaja. Nilimuuliza anaitwa nani? Akasema jina fulani la Kibantu nimelisahau.
Nilipomkumbusha kuhusu PW 1 kusema hakukuwa na Mwanasheria wewe unasemaje alikuwepo ukurasa wa 160.
The Court should accept my testimony that a team included a lawyer lakini naomba Mahakama ikubali ushahidi wako kwamba kulikuwa na Mwanasheria.
Mahakama ikikubali ushahidi wa PW 16 maana yake PW 1 ni muongo.
Sasa ni Mahakama gani itakayoconvict charge of treason kwa ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri wanaoitana waongo.
Kwa waongo hawa unamtia nani hatiani?
Part 471 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 465
Mhe. Lissu anaendelea kufanya mawasilisho yake ya mwisho (Final submission)
Ushahidi wa utetezi ulikuwa straightfoward kwenye ukurasa wa 592 wa record DW 1 nilisema sio mimi niliyerusha hayo matangazo ni waandishi wa Jambo TV.
Na vile vile uko ukurasa wa 621 na 622. Ushahidi wangu uliungwa mkono na DW 2 , ukaungwa mkono na DW 3, Ukaungwa mkono na DW 4 na ukaungwa mkono na DW 5.
Mashahidi wote wa Utetezi walikuwa consistent kuwa waliorusha matangazo ni wafanyakazi wa Jambo TV.
Lakini Muhimu kuliko yote kwamba ushahidi wa Utetezi uliungwa mkono na PW 17 Shahidi wa Mashitaka aliyekuwepo kwenye tukio na kurusha hayo matangazo.
Sasa Majaji nataka nimalizie hoja hii kwa kusema machache tu juu ya Sheria.
Hoja hii ya Publication ya Video Images kwanza nimesema haipo kabisa kwenye sheria niliyoshitakiwa nayo.
Masuala ya Utangazaji kwa vyombo vya Habari yanaongozwa na Sheria ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.
Mtu yeyote akitaka kujua nani anayewajibika na matangazo yanayorushwa kwenye radio na mitandao basi aende kwenye Media Service Act na kifungu cha 7(1) cha Sheria hiyo kinasema nani mwenye haki ya kukusanya, kuhariri na kutangaza chochote kinachopatikana? Nani anayewajibika na kuyamiliki.
Every media house and journalist shall enjoy the following rights
A. Freedom to collect
B. Freedom to edit in accordance of code of conduct
C. Freedom to publish the news
Kama kweli kulikuwa na makosa walitakiwa waende Jambo TV kwa kifungu hiki ile nonsense inayoitwa Constructive publication imekufa on arrival kwasababu Mwandishi au chombo kinachokusanya habari, kuhariri, kuzirusha ndio chombo chenye habari yenyewe.
Na kweli hili Waheshimiwa Majaji vilevile sitaki kuzungumzia maumivu ya kukaa Gerezani mwaka na nusu.
Nataka nizungumzie simanzi na maumivu ya kuona Mawakili wa Serikali wanaotakiwa kujua vitu hivi rahisi namna hii.
Mwaka na nusu wameng'ang'ania hoja ambayo mtoto anayesoma sheria mwaka wa kwanza angeona vitu kama hivi, kuna kipindi walikuwa Mawakili wanakuja hadi 11.
Jaji tuendelee
Hapana hiyo simanzi yangu itaenda mbali sana nitahitaji compensation.
Jibu la swali kwamba mimi ndio nilichapisha kwenye Jambo TV, jibu lake ni NO. I did not publish.
A year and a half in prison kept away from My family, from My party members nakaa kwenye chumba cha 6 kwa 6.
I have a beautiful house, nimekaaa kwenye chumba cha 6 kwa 6 nimekaaa ndani kwa hoja ya uongo ambayo waliijua hata kabla hawajanikamata, I did not publish the words anywhere.
God knows, I did not and everyone knows I did not, even these people who accuses me one and a half year, wanaonea watu wanatungia watu makosa ya uongo.
Uhaini
Uhaini
Uhaini
Mimi natembea na risasi kiunoni na kuvuta miguu yangu kwasababu ya kuipenda hii nchi.
I can’t imagine watu wasio wajanja kama mimi wanawafanya nini?
Issue no 6 ni kwamba i did not publish those words.
NB. Watu wanalia Mahakamani, akina Mama wanalia sana.
JAJI NDUNGURU ANAOMBA TUMALIZIE HII NUSU SAA Mshitakiwa asiende huko.
Mhe. Lissu anasema lazima niseme.
Hoja ya 7 ni Je Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishwa na hayo maneno?
Whether the Exevutive was intimidated by the alleged words?
Hilo ni swali la saba ninalokwenda kulijibu sasa.
Part 466 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa tuhuma za kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la SATCO, Said Fadhili (54), wakati akitoka kuweka mafuta katika kituo cha Mafuta.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya Said Fadhili kudaiwa kukwangua gari mali ya TARURA lenye usajili namba STM 5806, aina ya Land Cruiser LX 70 Series, lililokuwa likiendeshwa na Mtuhumiwa huyo.
Baada ya tukio hilo kuripotiwa, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John, baada ya kufanya upekuzi, Polisi ilibaini kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni ni toyi na siyo silaha halisi kama ilivyodhaniwa awali.
Aidha, Jeshi la Polisi limebaini kuwa gari hilo halikuwa likitumia namba yake halali ya usajili STM 5806, inayomilikiwa na TARURA, bali lilikuwa likitumia namba T 881 ENZ ambayo ni mali ya Mtu mwingine.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari, likisema kitendo hicho kinaficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa Sheria.
#MillardAyoUPDATES