On Short Notice Bank Kubwa zote CRDB , NMB , NBC , etc.
MNO's kubwa zote (Voda, Yas , Airtel) huwa wana graduate trainee program ya kupokea Fresh graduate na kuwafua na moja ya kigezo ni Good GPA , Sasa wewe na Gentleman GPA yako hata hii fursa huwezi pata inabidi ukaze sana.
Waliopata GPA za kuombea maji wanajifariji kwa kusema eti GPA kubwa sio uwezo
Wasio na uwezo wa kununua magari wanajifariji kwa kusema "IST sio gari"
Wasiosoma kabisa wanajifariji kwa kusema "kufeli shule sio kufeli maisha"
Wasio na hela wanajifariji kwa kusema "pesa hainunui furaha"
Na mwisho kabisa ambalo ndo kundi la wengi ni hawa waliooa wanawake used, second hand yaani wasio na bikra nao wana kamsemo kao ka kujifariji eti "bikra sio kigezo cha mke mwema"
Kila kundi na ujinga wake. Na kuna wengine mpo kwenye makundi yote. Yaani hujasoma au una GPA ya 2.3, huna hela, huna kagari na umeoa mtumba. Pole yako
Jamaa hapa kwetu ndugu zake wamemlia njama akafungwa halafu wakamlaghai mchumba wake akaolewa kwa nguvu na binamu yake. Mwaka umepita wamefanya maarifa wakamtoa cha kwanza anaulizia ni alipo mchumba wake wakamilishe mipango waoane.
Wale wale waliomlia njama wanamshangaa anavyowarudisha nyuma, “Kaka huu ni wakati wa kusahau yaliyopita. Tugange yajayo kama ukoo.”
Wabaya wake wamekuwa na hekima na hawako tayari kuzungumzia mambo yamefikaje hapo yalipofika, “Mke ana ndoa halali na hivi tunavyoongea ni mjamzito. Huwezi kuzungumzia kuachanisha ndoa kaka. Cha msingi ni kuachilia na kuangalia unakaaje na wenzio waliokuharibia maisha.”
“Hii si ndoa halali,” Jamaa analalamika. Jioni hii wataalam wa mazungumzo ya kifamilia wanamwambia ukweli, “Hoja kwa sasa si uhalali wa ndoa kaka. Wenzio wana cheti na kinatambuliwa na Jamhuri. Huu ni wakati wa kuuweka ukoo pamoja.” Jamaa anajiuliza maswali mengi na hana majibu. Hajui afanye nini na wahalifu wa maisha yake.