Watanganyika em achaneni na dengue asiwatoe kwenye mstari post kama hizi ndo tunatakiwa tu boost maana suddenly wengine mmeacha kupelekea moto bunge la Tanzania na serikali haramu mnamdiscuss uyo ki mtu since 2025 angeshataka kujitetea angeweka wazi kila kitu why now, em amkeni
TUACHE PROPAGANDA JUU YA UHAI WA WATANGANYIKA.
Hakuna Taifa linalotuonea wala kutuingilia mambo yetu ya ndani kinyume na Sheria za Kimataifa.
Yanayotupata leo yanatokana zaidi na ujinga wetu wenyewe, ukatili wetu wenyewe, na kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi.
Tumeacha misingi ya utawala wa sheria na kujigeuza kuwa miungu watu wasioguswa na uwajibikaji.
Hatuwezi kuua, kutesa, kushambulia na kupoteza maelfu ya watu halafu tukajificha nyuma ya neno “sovereignty.” Huo siyo ulinzi wa mamlaka ya Taifa; huo ni upotoshaji wa dhana ya sovereignty chini ya Sheria za Kimataifa.
Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa (UN Charter), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR), Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR), Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples’ Rights), pamoja na kanuni ya Responsibility to Protect (R2P), Mataifa yana wajibu wa kulinda uhai, utu, uhuru na usalama wa wananchi wake.
Sovereignty katika sheria za kimataifa siyo leseni ya Serikali kufanya ukatili dhidi ya watu wake bila kuwajibishwa. Sovereignty ina mipaka ya kisheria na kiutu iliyowekwa na mikataba ya kimataifa, sheria za haki za binadamu, na wajibu wa Mataifa kulinda wananchi dhidi ya mauaji, mateso, upotezwaji wa watu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Pale ambapo Taifa linashindwa au linakataa kulinda haki za msingi za wananchi wake, jumuiya ya kimataifa kupitia taasisi zake halali inaweza kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za kimataifa ili kuzuia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Ndiyo maana hatua mbalimbali zinazochukuliwa na baadhi ya Mataifa ya Ulaya, Marekani, na taasisi za kimataifa kuhusu maafa ya Oktoba 29 dhidi ya Watanganyika ikiwemo mauaji, upotezwaji wa watu, mateso, na vitendo vinavyokiuka misingi ya haki za binadamu zinaweza kuwa na msingi ndani ya mfumo wa sheria za kimataifa na wajibu wa kimataifa wa kulinda utu wa binadamu.
Tusipokuwa tayari kujiwajibisha wenyewe, tutajikuta tunawajibishwa na jumuiya ya kimataifa.
Ukweli, Haki, Utawala wa Sheria na Uwajibikaji ndiyo msingi pekee wa kulinasua Taifa letu kutoka katika mkwamo huu.
BAK MWABUKUSI
SHAMBANI BUSOKELO
Today marks one year since Tundu Lissu was arbitrarily detained and denied his fundamental rights. Please share this and visit https://t.co/xskhqPZgUd for more information.
#FreeTunduLissu
—Admin
Today is Tundu Lissu Arrest Day
It’s being one year since Samia Suluhu ordered his illegal detention
He remains behind bars while his trial has stalled
@UNHumanRights said his detention is illegal and the govt should release him IMMEDIATELY and compensate him - instead they continue to hold him
This is what an uncivilized barabaric authoritarian govt looks like!
Kiongozi wa nchi ambaye amepitia mengi na anaendelea kuteseka ila hajakata tamaa kuona uhuru, haki na usawa kwa wote!
Imetosha na mnajua hakuna kesi!
Muachieni Tundu Lissu
#FreeTunduLissu
@MariaSTsehai@SuluhuSamia Amejitoa sadaka kwa mateso kwaajili ya wengi,tuliyasoma kwenye vitabu ila naleo kwetu limetokea ila kunawapumbavu bado wanaona kama anasitaili,ila wengi tunajua anateseka kwasababu yakutetea rasilimari ya nchi yake na ndiyo maana mafisadi wakiongozwa na @SuluhuSamia wamempa kesi
Rubani mmoja wa Marekani mwenye uzoefu wa miaka 25 vitani, mkongwe aliyepigana vita tatu na aliyeshiriki mamia ya mashambulizi ya kivita angani, alizungumzia marubani wa kijeshi wa Israel.
Aliandika ujumbe uliosambaa kwa kasi mtandaoni uliosema:
“Nimeruka juu ya Iraq, Afghanistan na Libya. Nilidhani tayari nimeona kila kitu.
Lakini nilipoona kile kinachofanywa na Jeshi la Anga la Israel nchini Iran, niligundua bado mimi ni mwanafunzi.
- Usahihi,
- Mipango ya vifaa na uendeshaji (logistics).
- Kurusha Ndege 200 kwa usiku mmoja.
- Targets zaidi ya 500.
- Umbali wa kilomita 1,500 kutoka nyumbani.
- Hakuna kujaza mafuta angani kutoka vituo vya Marekani.
- Mafuta yote yametoka kambi za nyumbani.
- Silaha zote zimetoka nyumbani.
Ni kama kuruka kutoka Miami hadi New York, ukishambulia Targets njiani, kisha kurejea, wakati ndege 200 zinatembea kwa wakati mmoja bila kugongana hata mara moja.
Kwa marubani wa Israel: Nyinyi si Bora tu katika Mashariki ya Kati, Ninyi ndio bora duniani"