Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche pamoja na Viongozi wengine wa chama hicho wamefika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) kusubiri ripoti ya uchunguzi kuhusu kifo cha dereva wake, Suezi Dani Maradufu kabla ya kuuaga mwili wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, mwili wa Maradufu ulipatikana Julai 1, 2026 katika nyumba ya kulala wageni ya Ntahamba, Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo uchunguzi wa awali ulibaini kuwa pembeni ya mwili wake kulikutwa dawa za binadamu.
Viongozi na Wafuasi wa CHADEMA pamoja na Viongozi wengine wa Chama cha ACT Wazalendo wamekusanyika hospitalini hapo wakisubiri matokeo ya uchunguzi yatakayoruhusu taratibu za kuuaga mwili wa marehemu kuendelea.
#MillardAyoUPDATES
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema uchunguzi wa kisayansi kuhusu kifo cha mwanachama wa CHADEMA, Suezi Dani Maradufu, unaendelea, huku sampuli mbalimbali zikichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kuthibitisha chanzo halisi cha kifo chake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Julai 3, 2026, mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kisayansi na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Bugando pamoja na wataalamu kutoka mikoa ya Geita na Dodoma, wakishirikiana na Afisa Mwandamizi kutoka Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
Uchunguzi huo umefanyika mbele ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ndugu wa marehemu.
Polisi wamesema baada ya uchunguzi huo, sampuli zimechukuliwa kwaajili ya uchunguzi wa kina zaidi wa kisayansi ili kuthibitisha chanzo halisi cha kifo, na kwamba matokeo yatakapokamilika yataisaidia mamlaka husika kubaini kilichosababisha kifo hicho.
Maradufu alifariki Julai 1, 2026 ndani ya chumba alichokuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni ya Ntahamba mkoani Kigoma. Tukio hilo lilizua mjadala mkubwa, huku CHADEMA ikitaka kufanyika kwa uchunguzi huru na wa kina ili kubaini mazingira ya kifo chake.
Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa uchunguzi unaendelea kwa kufuata taratibu za kisayansi na kisheria, na limewataka wananchi kuwa na subira wakati wataalamu wakikamilisha uchunguzi huo.
Tomorrow is another day - Tundu Lissu's trial continues
Madhulmat wajipange kesho maana wamezoea kuleta ujinga kila wakati! Safari hii hawachomoki
Hatutaki kusikia hili wala lile
Muachieni Lissu
#FreeTunduLissu
Pole sana Mhe @HecheJohn. Uso wako unaonyesha uchungu na maumivu uliyobeba moyoni.
Mungu ndiye mfariji na tumaini letu na tumaini halitahayarishi.
Iko siku maumivu hayo yatakwisha kwa maana hakuna kidumucho chini ya jua Mungu ndiye mratibu wa mambo yote na kwa nyakati zote.
‼️🚨Breaking news!‼️
Nduli Idd Amin Mama anahangaika sana kujisafisha na mauaji ya Oktoba 29.
Kwa mara nyingine tena Nduli na genge lake wameingia Mkataba mwingine na lobby firm ya BGR ambapo Nduli amekubali kulipa USD laki mbili na nusu kwa mwezi ambayo ni sawa na Tsh milioni 670 na ushee kwa mwezi!
Ambapo kwa mwaka Nduli na genge lake watailipa hiyo kampuni dola milioni 3 za Marekani ambayo kwa pesa ya madani ni kama bilioni 8 na ushee.
Wakati huo Serikali haram haina pesa hata za kulipa mishahara kwa baadhi ya kada.
https://t.co/KgKxJy0XBM
Mwili wa marehemu Suez Dani Maradufu, aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Bara, John Heche @HecheJohn umefanyiwa uchunguzi wa kisayansi na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Bugando, Geita, Dodoma na Afisa Mwandamizi kutoka Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mbele ya viongozi wa CHADEMA na ndugu wa Marehemu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Philemon Makungu iliyotolewa leo Ijumaa Julai 03, 2026, hatua hiyo ni mwendelezo wa uchunguzi wa kifo tata cha dereva huyo kilichotokea Julai 1, 2026, katika nyumba ya kulala wageni ya Ntahamba mkoani Kigoma.
ACP Makungu ameeleza kuwa mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kisayansi (postmortem) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, na sampuli mbalimbali zimeshachukuliwa ili kubaini chanzo halisi cha kifo chake.
“Baada ya uchunguzi huo wa wataalamu hao wakishirikiana na Jeshi la Polisi, sampuli zimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kisayansi ili kuthibitisha chanzo halisi cha kifo”, imeeleza taarifa hiyo.
Hatua hii ya Jeshi la Polisi imekuja saa chache baada ya viongozi wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche, na Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa kuonekana nje ya hospitali hiyo wakisubiri matokeo ya uchunguzi wa mwili (postmortem) wa Suez ili kufahamu chanzo cha kifo chake. Awali, CHADEMA ilitoa wito wa kuharakishwa kwa kufanyika kwa uchunguzi huo ili kuruhusu taratibu za mazishi kufanyika mapema.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, mwili wa marehemu ulipatikana Julai 1, 2026 katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kwa jina la Ntahamba, ambapo walibaini kuwepo kwa dawa za binadamu aina ya vidonge ndani ya chumba hicho, huku uchunguzi zaidi ukiendelea kubaini chanzo cha kifo hicho.
#TANZANIA:LISSU:KAMA WALITAKA KUNIKONDESHA WATAFUTE UTARATUBU MWINGINE
“Kama walikuwa wanataka kunikondesha, watafute utaratibu mwingine.Hiyo imeharibika”- Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema akizungumza leo muda mfupi mara baada ya usikilizwaji wa maombi ya mapitio kukamilika. Hata hivyo Pamoja na kuwa gerezani kwa takribani zaidi ya siku 400 Lissu ameonekana mwenye bashasha muda wote pindi anapofikishwa Mahakamani.
Jioni hii ibada fupi ya kumwombea marehemu Suez Dani Maradufu imefanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, kabla ya mwili wake kuondoka na kuanza safari kuelekea Tarime, mkoani Mara kwaajili ya maandalizi ya mazishi.
Maradufu alikuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara Mhe. John Heche na alifariki dunia Julai 1, 2026 ndani ya chumba alichokuwa amepanga katika nyumba ya kulala wageni ya Ntahamba mkoani Kigoma. Tukio hilo lilizua mjadala mkubwa, huku CHADEMA ikitaka kufanyika kwa uchunguzi huru na wa kina ili kubaini mazingira ya kifo chake.
Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa uchunguzi unaendelea kwa kufuata taratibu za kisayansi na kisheria, na limewataka wananchi kuwa na subira wakati wataalamu wakikamilisha uchunguzi huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameiomba Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) huku pia akiomba kulipwa fidia kwa madai ya kupotezewa muda kwa siku 139.
Lissu ameyasema hayo leo Julai 3, 2026 wakati wa usikilizwaji wa maombi ya mapitio ya Jamhuri namba 7440840 ya mwaka 2026 mbele ya Jopo la Majaji watatu.
Akizungumza mbele ya Majaji hao walioongozwa na Jaji Shion Mwarija, Muruke na Khamis, Lissu amedai kuwa kesi yake imecheleweshwa kwa makusudi kwa muda wa siku 139, hatua inayodaiwa kumuweka mahabusu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Kwa upande wake, Wakili Mkuu wa Serikali, Nassoro Katuga amepinga hoja za Lissu akisema maombi hayo hayakulenga kuchelewesha kesi na kwamba kifungu cha Sheria kilichotajwa na Lissu hakitumiki katika mazingira hayo ya shauri hilo.
Nje ya viunga vya Mahakama, Wakili wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amezungumza na Vyombo vya Habari kuhusu mwenendo wa shauri hilo.
#MillardAyoUPDATES
Abdul na Sumai kwani Mzee Suez Maradufu amewakosea nini kikubwa mpaka mkaona adhabu ambayo anastahili kupewa ni kuuwawa kwa sumu?
Mbona Mzee wa watu hata hakuwa na shida na mtu yeyote, alikuwa busy na kazi yake ya kumuendesha Mhe. Heche au kosa lake ni kuwa Dereva wa Heche?
Mnahitaji kumwaga damu za watu wangapi ili mtosheke, Oktoba 29 mliuwa waTanganyika wenzetu zaidi ya elfu kumi,
Tangu Nduli Idd Amin Mama aingie madarakani hadi leo mmeteka na kupoteza watu zaidi ya 400 na bado mnaendelea kuteka na kuuwa watu.
Watanganyika wenzangu, hakuna wa kutuokoa, tusiposema inatosha Nduli Idd Amin Mama na genge lake watatumaliza.
Julai 7, 2026 tusimame kwa umoja wetu bila kujali itikadi zetu, tuseme inatosha.
#77Tunatoka #7UP #FreeTanganyika #FreeTanzania
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 230
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo, maombi haya yameletwa kwa lengo moja tu kurefusha mashauri na kuchelewesha kesi ya msingi ili mjibu maombi aendelee kukaa Ukonga gerezani.
Leo ni siku ya 139 kesi haifanyiki na mimi nakaa Gerezani I'm completely innocent but I'm in prison kwa mwaka mmoja na miezi mitatu.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania article 59.b.4 inazungumzia mamlaka ya DPP kutokuchekewesha muenendo wa Mahakama.
Kuzuia Mahakama kuu kuendelea na kesi kwa siku 139 kwa kuleta maombi ambayo wanayajua hayana msingi wowote, kama hii ni kutenda haki then inabidi tutafute tafsiri nyingine ya neno kutenda haki.
Mamlaka ya DPP ni kuwezesha uamuzi wa haki, wa haraka na usiokuwa wa gharama kubwa.
Niko Mahabusu muda wote huo je hiyo ni haki? DPP na Mawakili wake wamepuuza mamlaka ya kikatiba ya DPP kwa maneno yao wenyewe walishabakiza shahidi mmoja lakini haijaendelea kwa siku 139 kwa sababu ya maombi haya.
Mhe. Lissu anasema ombi langu siyo tu Mahakama hii iyakatae maombi hayo siyo tu hilo, maombi yangu Mahakama ya rufani ina mamlaka ya kutoa amri ambazo zingetolewa na Mahakama kuu.
Kwa kutumia kifungu cha 367 cha kutaka mleta maombi anilipe fidia kwa kunifanye nikae gerezani kwa siku 139 bila kesi kuendelea kwa sababu ya maombi yake.
Yakataeni haya maombi na muamuru DPP anlilipe fidia kwa usumbufu wote alionifanyia.
Mhe. Lissu anasema ni hayo tu Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya rufani.
Anasimama Wakili wa Serikali Katuga.
Anasema tumeleta maombi yetu na tumeiomba Mahakama hii tukufu kwamba tumenyimwa haki ya kusikilizwa kwenye huo ushaidi tunaoomba uongezwe, ulikataliwa kabla ya kufika katika hiyo mahakama.
Mjibu maombi ameialika Mahakama hii kwenye proceedings kuanzia pg 391 akizungumzia submission ya uhalali wa notice yetu, tulipata nafasi ya kusikilizwa kuhusiana na notice yetu siyo nafasi ya kusikilizwa kuhusiana na huo ushahidi.
Hatueleweki harafu tunaambiwa tumefanya clever drafting, ushahidi umekataliwa kabla ya kuingizwa, tulisikilizwa kwenye notice tu.
Mjibu maombi anaposema tulipewa haki ya kusikilizwa hakutuelewa kwenye angle gani. Kuirejesha Mahakama hii katika kifungu cha 308 anasema ni kuomba rufaa kwa Mahakama hii sisi tulikuwa tunaonesha walichokifanya na kilichotakiwa kufanyika.
Katunga anaendelea kusema
Sisi hatujaleta maombi haya kuchelewesha kesi tumekuja hapa kuiomba Mahakama iwese kutafsiri Sheria. Kifungu cha 367 kinatumika pale Mahakama inapokuwa imesikiliza kesi na kuona kwamba kesi ni ya kutengenezwa.
Kwa mujibu wa Sheria tunasema maombi yetu ni ya muhimu tunaomba yakubaliwe na yatazamwe na kuita hizo proceedings kuangalia kile ambacho tunakilalamikia.
Jaji anasema basi baada ya kusikiliza pingamizi la awali pamoja na maombi haya tutakwenda kuamua kwanza kuhusu pingamizi la awali kama tutakuwa tumekubali basi itaishia hapo kama pingamizi litakataliwa basi tutaendelea.
Tutawajulisha tarehe ya uamuzi.
Inapigwa Court ya kinyonge ni kama jamaa mchana umepita kama upepo.
Nawatakia Ijumaa njema.
Julai 7, 2026 tukutune barabarani, usihau kubena bango lako lenye ujumbe wa madai yetu ya msingi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Anasimama Mhe. Lissu.
Anasema baada ya kusikiliza hoja za Wakili wa mleta maombi naomba nianze kwa kunukuu maneno ambayo Mahakama hii iliyasema kwenye kesi ya Commissioner General of TRA Criminal case namba 62/2022 pale ambapo maombi ya mdaawa yamezuiliwa na sheria, hawezi kufanya drafting ya kuhadaa Mahakama.
Wanasema uamuzi ulifanyika bila wao kusikilizwa, mgogoro ulianza 19 February 2026 ukurasa 391 wa record, Ugomvi ambao umetuleta hapa ulianza siku Tano kabla ya maamuzi ya Mahakama.
Wakili wa Serikali mkuu Renatus Mkude alisema "waheshimiwa Majaji tuko tayari kuendelea na mashahidi 3 lakini kabla ya kuendelea tuna notice of additional substance of evidence, ambayo imejazwa electronically siku ya Jana"
Katika ukurasa wa 392 Mahakama ikaamua kuwa tuendelee na mashaidi kwanza baadae tutarudi kwenye hoja za notice.
February 20, 2026 ukiangalia ukurasa wa 405-419 utayaona maneno niliyoyasema.
Mahakama ikaamua tumesikiliza sehemu zote kesi hii anahairishwa hadi jumatatu ilikuwa 23 February 2026 kuanzia ukurasa 420 unaonesha hayo.
Mkude akasema wako tayari kuendelea na Katuga akafanya submission in chief pg 421, 423 Katuga akajibu PO, nikafanya rijoinder, pg 428 kuna ruling of the court.
Baada ya submission ya Renatus, submission in chief ya Katuga, rejoinder yangu na reexamination in chief ndipo Mahakama ilitoa uamuzi.
Kwa record hiyo yote nguvu ya kusema hawakusikilizwa wanaitoa wapi?
Kwasababu ya maombi haya leo ni siku ya 139 kesi haiendelei kwa sababu ya uongo wao kwamba hawakusikilizwa.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba ni kweli sasa kwa ushaidi huu wanawezaje wakasema hawakusikilizwa?
Mmemsikia Wakili Katuga akisema Mahakama ilikosea ilipaswa iangalie reasonablity ya hiyo notice, ipokee ushaidi, iangalie competence kisha iamue.
This is an appeal under 6.3 wanayoitaja, it's only clever drafting inayolenga kuiadaa Mahakama.
Iangalie TRA vs New Musoma textile industry kwenye orodha yangu ni kesi namba 7 hawaruhusiwi kuleta malalamiko kuhusiana na hiyo notice kwenye Mahakama hii. Kifungu 6.3 cha AJA mamlaka ya Mahakama hii siyo hiyo wanayoiomba wao.
Ukurasa wa 21 unaonesha mjadala mpana wa ninachokisema sasa na inamaliza huu mjadala, hamuwezi kuanza kuangalia hiki kilicholetwa ni kitu gani mnapaswa kutazama je huu uamuzi ni legal.
Wanasema hawakusikilizwa mnaangalia kwenye record, Je ni kweli hawa watu hawakusikilizwa, hamuendi kwenye huu usikilizwaji ulikuwaje, Mahakama hii haiangalii mambo superficial.
Waheshimiwa Majaji mleta maombi alisikilizwa hivyo ruling ya mahakama ni legal, imeandikwa na Majaji wenye mamlaka baada ya kusikiliza pande zote hata kama hauwafurahishi wanapaswa kukubaliana nao.
Waheshimiwa Majaji waleta maombi hawana hoja yeyote ya maana on the basis of this record. Section 308 ya CPA imetajwa kwa lengo la kuwaalika mtengue kilichoamuliwa na Mahakama kuu nawaombeni msiende huko.
Nitasema kwa kifupi sana juu ya section 308 ya CPA na nini Mahakama ilisema inakataa kuongezwa kwa ushahidi mpya inadeal na Shaidi mpya tu.
Inazungumzia ni katika mazingira gani shaidi ambaye hakutajwa kwenye commital proceedings anaweza kuongeza kwenye trial, mleta maombi hapa analeta ushahidi mpya wa shaidi ambaye ametajwa kwenye commital na siyo shaidi mpya kama Sheria inavyotaka.
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye uamuzi huu hakuna sehemu ambayo Mahakama imesema ushaidi huo haufai bali imesema ni ushahidi mpya na haufai kisheria.
Hii clever drafting in order to avoid the legal power, kama wanataka kupinga uamuzi huo wasubiri kesi iishe kisha wakapinge uamuzi huo.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 228
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba nimalizie nisiwachoshe.
Hoja yangu inahusika na maamuzi ambayo hayamalizi kesi, kesi bado ipo na tutakapoenda kwenye substance nitawaoneshe Majaji kwenye hicho walichokileta wao wenyewe ambavyo kesi bado inatusubiri.
Kwa bahati mbaya wametupotezea muda sana hivyo nawaombeni Waheshimiwa Majaji mkatae maombi hayo.
Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji maombi yetu yameletwa chini ya kifungu cha 6 kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya mamlaka ya rufaa ya mahakama hii na kanuni ya 65 kanuni ndogo ya 1. Waheshimiwa Majaji ukisoma notice yetu inataja kifungu cha 6 cha Sheria ya mamlaka ya rufaa ya mahakama hii, Waheshimiwa Majaji lalamiko la mjibu maombi lisingekuwepo kama angeipitia kanuni ya 48.
Jaji anamwambia Katuga ulishamaliza usilete jambo jipya nenda moja kwa moja kwenye maombi.
Katuga anaendelea
Waheshimiwa Majaji maombi yetu yamejikita kuiomba Mahakama hii tukufu iweze kuangalia uhalali na usawa wa muenendo wa shauri lililoko mbele ya Mahakama kuu.
Maombi haya yametokana na mzizi wa upande wa Jamhuri kuleta notice ya kuongeza ushaidi ambao haukusomwa wakati wa commital na upande wa Jamhuri ulifanya vile kuendana na kifungu cha 308 cha CPA, kifungu hiki Waheshimiwa Majaji kinaweka zuio kwamba hakutakuwa na ushahidi ambao utaongezwa Mahakamani kama ushahidi huo haukusomwa hautaruhusiwa kuongezwa unless upande wa Jamhuri utatoa notice ya kuongeza ushaidi huo.
Tunatakiwa kutoa notice ili mshitakiwa asikutane nayo by surprise, kifungu hicho kinaitaka Mahakama wakati inafanya reasonablity ya notice ifanye vitu gani.
Mahakama wakati inatakiwa kutambua reasonablity ya notice inapaswa kuzingatia kifungu cha 308 kifungu kidogo cha 3 inatakiwa kuuchambua ushaidi wenyewe.
Naona Job Mrema ni kama kambonyeza Katuga ameinama sijui wanaongea nini na wenzake,
Halafu sio mara moja kila baada ya sentence kadhaa vikao vinakuwa vingi.😤
Anaendelea Katunga
Mahakama ilienda kuangalia huo ushahidi katika ukurasa wa 431 wa muenendo wa Mahakama kuu na kuita ni ushaidi mpya umekusanywa baadae na hivyo wamekataa.
Ushaidi unakatakiwa pale ambapo unakuwa umefikishwa Mahakamani baada ya kuwa umepimwa ndipo Mahakama inaamua uingie au usiingie, upokelewe au usipokelewe lakini hauwezi kuamuliwa wakati unakuwa introduced.
Kifungu cha 308 kimetoa nini Mahakama inafanya, ndo maana kwenye maombi yetu tunasema tumenyimwa haki ya kusikilizwa in relation na huo ushahidi.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba, maana ya hii haki ya kusikilizwa ni kumpa mtu haki ya kumsikiliza full kwa utimamu ndo maana Mahakama ina vitu vitatu vya kupima.
Ushaidi unapimwa unapokuwa umefika Mahakamani, kusema ushaidi ni mpya usiletwe ni kuukataa ushaidi kabla hata haujafika Mahakamani.
Mahakama hata haikuusikia ushaidi lakini ikaenda kusema ushaidi huo ni irrelevant.
Utaratibu wa proceeding ulikuwa umekiukwa na ukiukaji ambao unaenda kwenye shauri yenyewe na ndiyo maana upande wa Jamhuri tukaona kwa busara zenu muangalie hizo proceedings hatuwezi kuendelea na hizo illegalities.
Anaendelea Katuga
Tunataka Mahakama iangalie ni kwa namna gani kwa muda gani ushaidi unaangaliwa na kuwekwa kama ushaidi.
Kwenye kifungu hakuna sehemu tuliposema Mahakama iende ikaupime huo ushahidi ilikuwa ni notice tu, ushaidi kuja Mahakamani na kufukuzwa kabla ya kusikilizwa huko ni kutunyima haki.
Ni vigumu kupima ushaidi ambao hauko hata mahakamani.
Ukurasa wa 431 wa proceedings naomba muuangalie waheshimiwa Majaji, jambo hili lilikiuka taratibu za mienendo ya proceedings.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya rufani tunaomba maombi yetu yaangaliwe na yakubaliwe.
Waheshimiwa Majaji ya kwetu ni hayo tu.
Part 229 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema changamoto anazopitia zina mwisho, akizungumza na Viongozi na Wafuasi wa chama hicho waliofika katika Mahakama ya Rufani kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo leo Julai 3, 2026.
Kauli hiyo imekuja baada ya Mahakama ya Rufani kusikiliza maombi ya marejeo yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na kuahirisha shauri hilo, ikieleza kuwa itatoa taarifa baadaye kuhusu tarehe ya kutolewa kwa uamuzi.
#MillardAyoUPDATES