Emmanuel, ahsante kwa dua njema kwangu na nchi yetu. Wasaidizi wangu watawasiliana nawe kuhusu ombi la kuchangia ujenzi wa Kanisa, na kukupa mchango wa shilingi milioni ishirini. Nawatakia kila la kheri katika kukamilisha ujenzi na kutoa huduma mkizingatia sheria, mila na desturi za nchi yetu.