Huyu ngombe ana-trend sana ranch za Marekani. Ni Brahman. Wengine wanamwita American Brahman. Ana masikio marefu kumzidi Boran. Yeye kuvuka 1000kgs ni kama utani
Hivi ushajiuliza, Kwanini Kinyesi Cha Tembo wanasema ni Dawa ya Magonjwa Mengi Sana.
Jibu ni kwamba yule mnyama anakula asilimia 90 ya miti unaijua wewe pamoja ma matunda yake.
Ikawe Asubuhi Njema kwako, kula Matunda ya Asili Sana.
Huyu ni kijana wa Kitanzania akipigwa na vijana wa Afrika Kusini..
Huyu ameenda kutafuta maisha kwasababu hapa kwetu haoni kesho yake..
Ameacha Nchi pekee yenye Tanzanite Duniani, Nchi ya tatu kwa dhahabu, Nchi yenye gesi, makaa ya mawe, chuma na ardhi ya kutosha, ameacha maji na mbuga za wanyama..
Leo anafanyiwa hivi na watu ambao walipata hifadhi yao hapa wakati wakipigania Uhuru wao..
Leo Nchi yetu iko mikononi mwa kikundi kidogo na wachina huku vijana wetu wakifanywa kama mbwa kwenye Nchi za wageni.!!!
Nimeumia sana
Tuliokulia hii "breakfast" kwa sasa legally ni wazee. Chai na mikate ilikuja baadae sana tena sio kwa kila familia. Huku Kanda Maalum (Mara), hiyo togwa inaitwa OBHOSARA. Ina virutubisho usipime! Bado ni kinywaji pendwa. Huko kwenu togwa mnaiitaje kiasili?