One country. One foreign policy. One diplomacy.
The boundary between what is bilateral and what is multilateral is often blurred. I therefore paid a courtesy call to Her Excellency Elsie Kanza, our Ambassador to the @UbaloziUSA, to discuss ways and modalities of working together to advance Tanzania's interests in the United States and the United Nations.
WU®Media | Rome Italy
_Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy Mhe. *Mbarouk Nassor Mbarouk* amekutana na wadau kwenye kikao cha kwanza mbapo walijadili kwa mapana dhamira yao kuu ya miradi katika sekta ya elimu,biashara ...
Link: https://t.co/LzIrB7TBAz
Ikulu, Dar es Salaam, Aprili 23, 2026
Hotuba yangu leo nilipopokea ripoti ya Tume niliyoiunda kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.
Tupoendelea kushughulikia na kuyapatia majawabu yaliyotokea, ninawasihi tuongozwe na maneno haya kutoka katika vitabu vitakatifu:
2 Mambo ya Nyakati 7:14
“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.”
Surah Al-A'raf (7), Aya ya 23
"Mola wetu Mlezi! Tumejidhulumu nafsi zetu, na usipotusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara.”
Mungu Ibariki Tanzania.
🇷🇺🇹🇿 Pembezoni mwa Kongamano la pili la Mawaziri Urusi-Afrika linalofanyika sasa jijini Cairo, Misri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Mhe. Sergey Lavrov amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
🚨 HONORING LEADERSHIP IN AFRICAN FOOTBALL
Under the guidance of CAF President Dr. Patrice Motsepe, the Presidents of Kenya, Uganda and Tanzania have been recognized for their outstanding contributions to football development. 🌍⚽
These nations hosted the most successful CHAN tournament, setting new standards for excellence on and off the pitch.
#CAFAwards2025 #AfricanFootball
Bonanza la Mpira wa Miguu la Serengeti Lafana Antwerp, Ubelgiji
Bonanza la Soka la Serengeti ambalo lilifanyika jijini Antwerp, Ubelgiji tarehe 15–16 Agosti 2025 limefanikwa kuvuta watu wengi zaidi nchini Ubelgiji na nchi za jirani. Tukio hilo la kimichezo liliwaleta pamoja zaidi ya Watanzania 600 waishio Ulaya na timu za mpira wa miguu 14 zinazoundwa na diaspora wa kitanzania kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya ikiwemo Ubelgiji, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Uholanzi, Luxembourg, Sweden na Denmark. Aidha, timu rafiki kutoka diaspora wa Burundi na Somalia nazo zilishiriki ikiwa ni kielelezo cha mshikamano wa kijamii na kikanda.
Akihutubia washiriki na wageni waalikwa, Balozi Jestas Abuok Nyamanga, alisisitiza dhamira ya dhati ya Serikali kuendeleza michezo ndani na nje ya Tanzania ikiwemo kwa diaspora. Halikadhalika, alieleza kuwa Bonanza hili si tu jukwaa la kuibua na kukuza vipaji, bali ni jukwaa muhimu la kujulisha mikakati ya Serikali kwa diaspora . Alishukuru wadhamini ikiwemo NBC na ASAS na kutoa wito kwa wadau wa michezo wakiwemo diaspora kuendelea kushiriki ipasavyo katika matukio ili kuendeleza mshikamano na maendeleo ya Watanzania popote walipo.
Viongozi wengine waliojumuika katika tukio hilo ni pamoja na Bw. Salvatory Mbilinyi, Mkurugenzi wa Masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mheshimiwa Caroline Chipeta, Balozi wa Tanzania, The Hague; Mheshimiwa Mobhare Matinyi, Balozi wa Tanzania, Stockholm; pamoja na maafisa kutoka ubalozi wa Tanzania Paris na London. Bonanza hilo lilihudhuria pia na Mabalozi kutoka nchi jirani akiwemo Mheshimiwa Prof. Bitange Ndemo, Balozi wa Kenya, Brussels na Mheshimiwa Luate Samuel Lominsuk, Balozi wa Sudan Kusini, Brussels na Mwakilishi wa Balozi wa Somali, Brussels.
Zaidi ya michezo, Bonanza hili pia lilitumika kama jukwaa la utoaji wa huduma kwa Diaspora. Taasisi muhimu kutoka Tanzania zikiwemo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na NBC Bank ziliungana na washiriki kutoa huduma, kusikiliza changamoto na kuwahamasisha Watanzania wa Diaspora kushiriki katika fursa za kifedha na elimu zinazopatikana nyumbani.
Katika mashindano haya yenye ushindani mkubwa, Timu ya Soka ya Kilimanjaro Football Club kutoka Sweden iliibuka mabingwa wa mwaka 2025 huku Timu ya Leeds FC kutoka Uingereza ikishika nafasi ya pili.