17/1/1997 yes its my Birthday. ๐๐ช๐งจ
Siku kama ya leo miaka 28 nyuma, saa 4 asubuhi, siku ya IJUMAA kama leo nililetwa duniani.
Ni mara chache sana kwenye hii miaka 28 na sikumbuki ni mara ngapi huwa imetokea SIKU tarehe mwezi na mwaka vikafanana kama mwaka huu.
Yani SIKU Ijumaa, MWEZI wa kwanza, TAREHE 17, inatokea mara chache sana. Naamini huu utakuwa mwaka wangu special kama ulivyokuwa tangu siku ya kwanza niliyoletwa dunia ilivyokuwa Special.
Naishukuru miaka 27 iliyopita imenifundisha mengi, ni miaka aambayo SITAKUJA KUISAHAU mpaka naingia kaburini. Imebadirisha maisha yangu kabisa, mengi nitayaongea mbele ya safari ila naishuru hii miaka 27 iliyopita imenipa DARASA.
Kwakuwa baraka zimejirudia za mwaka 97, basi naamini nimezaliwa UPYA, sio Edger tena, huyu ni SATIVA, nitasimama na wananchi kwenye kupambania HAKI na USAWA kwenye jamii yetu. Najua ni vita ngumu, ndiomaana kila tukizaliwa tunaanza kwa kulia tukijua safari mpya ni ngumu.
Damu yangu iliyomwagika PORI LA KATAVI 27/6 kwa lengo la Kuuliwa na maiti yangu kuliwa na WANYAMA wakali ile ilikuwa ya EDGER wa familia ya MWAKABELA. Huu uponyaji mpya ni wa SATIVA na Familia za WATANZANIA.
Nitashugulika na WAKOLONI WEUSI bila kupepesa macho au kusubiri MAELEKEZO, sitajali nashinda au sishindi ila ninachokijua KUPAMBANA TUU. Haya maisha yangu mapya ni kwaajili yenu WATANZANIA, mlilia sana nilipopotea na kupatikana MAHUTUTI, mlinipigania sana kuhakikisha nakuwa salama tena.
Nawaahidi nitajilinda kwa WIVU MKUBWA SANA, nitaishi ndugu zangu, tutawashugulikua hawa VIBAKA kwa nguvu zote Siku zote, siamini kama nitakengeuka siku moja, hiyo nafasi haipo.
Natamani kuandika mengi juu ya haya maisha yangu mapya ila itoshe tuu kusema hayo na kujitakia HERI YA SIKU YA KUZALIWA MUNGU NI MWEMA SANA.๐๐ฟ๐๐พโโ๏ธ
SATIVA17๐ซก
@Skypixel_45 Bila kufikiria,Hii meseji imekaa kiume ila ukiisikiliza vizuri ina sauti kama ya mama wa kiswahili inayosema "Vunja tu sahani mwanangu Baba ako ana kiwanda cha vyombo ataleta kabati zima"
Kuna ONYO la kiume na KARIPIO la kike
Mazee Uchunge! na Kabla ya kuchunga,Uchunge Zyaidiii