KWANINI RAIS SAMIA ANATAKIWA KUPEWA MAUA YAKE KATIKA KUIONGOZA TANZANIA?
Kabla ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, Tanzania ilikumbwa na changamoto mbalimbali katika nyanja za kiuchumi, kijamii, na kisiasa. Kulikuwa na hali ya wasiwasi na mashaka kati ya wananchi na serikali, hususani kuhusu uhuru wa vyombo vya habari na haki za kiraia. Uchumi ulikuwa unakua lakini kwa kasi ndogo, na kulikuwa na ukosefu wa uwazi katika sera za serikali. Kulikuwa na migogoro ya kisiasa, ambapo upinzani ulipata wakati mgumu kutokana na hatua kali za serikali zilizokuwa zinatekelezwa dhidi yao.
Tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, kumekuwa na mabadiliko makubwa. Ameimarisha uhuru wa vyombo vya habari, kufungua milango ya mazungumzo na wapinzani wa kisiasa, na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi nyingine. Katika nyanja za kiuchumi, serikali yake imefanya juhudi kubwa kuvutia uwekezaji wa kigeni, kuboresha mazingira ya biashara, na kuendeleza miradi ya miundombinu. Aidha, ameweka mikakati madhubuti ya kupambana na rushwa na kuhakikisha uwajibikaji wa viongozi wa umma.
Moja ya hatua kubwa alizochukua Rais Samia ni kuboresha huduma za kijamii, kama afya na elimu. Serikali yake imeongeza bajeti ya sekta hizi muhimu, kuhakikisha vifaa tiba na dawa zinapatikana kwa wingi, na kuboresha miundombinu ya shule na hospitali. Pia, ameanzisha mpango wa utoaji wa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, hatua iliyowezesha watoto wengi kupata elimu bila vikwazo vya kifedha.
Rais Samia anapongezwa kwa kuleta utulivu wa kisiasa na kijamii, kuongeza uwazi na uwajibikaji wa serikali, na kuendeleza sera zinazolenga kuboresha maisha ya wananchi. Juhudi zake zimeleta matumaini mapya kwa watanzania wengi, na kwa hivyo anastahili pongezi na heshima kubwa kwa kazi kubwa anayoifanya. Matokeo ya juhudi zake yanaonekana katika kuimarika kwa uchumi, kuongezeka kwa uwekezaji, na kuimarika kwa hali ya maisha ya wananchi. Anapaswa kupongezwa na kupewa maua yake kwa kuwa ameonyesha uongozi bora na wenye tija kwa taifa.
Naam kwa haya machache Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anastahili maua yake.
Congratulations to Professor Mohamed Yakub Janabi for being elected the World Health Organization Regional Director for Africa, for the term 2025-2030.
With decades of expertise and experience in the health sector, I have every confidence that you have all that it takes to serve our continent, and steer us all to greater heights.
The United Republic of Tanzania is thankful to every member state that believed in your skills, experience and vision for our continent.
Professor, you have my warmest wishes for a successful tenure.
Ninawatakia kila la kheri wanangu wote wa Kidato cha Sita na Ualimu ngazi ya Astashahada na Stashahada mnaoanza mitihani yenu ya kuhitimu leo. Hii ni hatua kubwa na muhimu katika safari yenu ya kielimu na kimaisha. Serikali imefanya kazi kubwa kisera na kiuwekezaji katika sekta ya elimu ili muweze kuipata katika mazingira sahihi, na ninaamini mmeandaliwa na kujiandaa vya kutosha kwa mitihani hii.
Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwasimamia.
Kheri ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Ninafarijika kuona tumepiga hatua kubwa katika kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza, ambapo mwaka 2025 tumepanda zaidi katika viwango vya uhuru wa vyombo vya habari duniani. Haya ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na kila mdau kwenye sekta hii muhimu.
Ninaendelea kuvisihi vyombo vya habari kutumia weledi katika kazi zenu ili kuendelea kujenga na kuimarisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa, hasa kipindi hiki tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu. Ninyi ni wadau na washiriki muhimu si tu kwa shughuli za Serikali, bali pia kwa uhai wa Taifa letu.
I am saddened by the passing of Dr. Victor Omololu Olunloyo at the age of 89. He was a revered Nigerian Elder Statesman and former Governor of Oyo State. A patriotic and astute leader. A renowned mathematician. Nigeria has lost one of its best minds. May his soul rest in peace.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma mfano wa ufunguo mara baada ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Makazi ya Majaji tarehe 05 Aprili, 2025, Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Majaji, Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Makazi ya Majaji Jijini Dodoma tarehe 05 Aprili, 2025.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Nyumba za Makazi ya Majaji Jijini, Dodoma, tarehe 05 Aprili, 2025.
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia Akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel: Ikulu Tanzania Tovuti: https://t.co/cnxHoY889H
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na Bibi Moza Himid na Mume wake Professa Saleh Idrisa wakati alipowatembelea kuwajuilia hali nyumbani kwao Maisara Zanzibar tarehe 03 April 2025.