Ukisoma Story ya Nabii Eliya katika Biblia baada ya kushinda vita dhidi ya karmel (1 Wafalme 19) Malkia Yazebel alimtishia kumuua😂akapata hofu kubwa akakimbilia Jangwani huko
Akiwa amechoka na kukata tamaa akamwambia Mungu “Yatosha sasa chukua Roho yangu” 😊 akiwa na uchovu mzito akalala, Malaika Bwana akamtokea na kumwambia “Amka ule maana una safari ndefu” kuna muda hata uwe umechoka kiasi gani Piga Msosi Lala mengine yatakuja tu 🚶♀️Nisikie Amen huko nyuma 🙏
Niwape story nyingine ya Nabii AYUBU? 😂
Ukisoma Biblia AYUBU 1:1, Biblia inasema Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyoofu. 😎
Unajua kuwa mnyoofu wewe! Mungu alikuwa proud naye sana. Lakini kulikuwa wanoko 😂 wakasema, Mungu huyu unamuona yuko hivyo kwa sababu umempa kila kitu.
Chukua hivyo vitu vyake uone kama bado atakuwa mwaminifu kama unavyosema, Mungu akaona isiwe kesi ngoja tuone
Ghafla utajiri ukaondoka, mali zikapotea, watoto wakafa, na Ayubu akapata maradhi makali ya mwili.
Halafu wale wale Ma snitch wakaanza kusema, Hapana, lazima huyu kuna dhambi kubwa amefanya, Lakini pamoja na yote hayo, Ayubu aliendelea kushikilia imani yake.
Ndipo katika AYUBU 1:21 tunapata maneno haya
“Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana libarikiwe.” 🙏🏾
Guess what 😂 Baada ya kipindi chote cha mateso na maumivu, Mungu alimrudishia Ayubu kila kitu, tena zaidi ya alichokuwa nacho mwanzo. Hapo ni AYUBU 42:10.
Wakati mwingine hali ngumu tunazopitia kwenye maisha yetu si kwa sababu tunastahili, hapana. Wakati mwingine ni kwa ajili ya kutujenga, kutufundisha, na kutuandaa kwa kile kinachokuja mbele yetu.
Usikate tamaa katikati ya story yako. Mungu bado hajaandika mwisho wake. ☺️
Nisikie Amen kutoka huku nyuma.
@Roma_Mkatoliki Baada ya kusitisha masomo ya advance na kwenda kijijini kumuuguza Mzee wangu, kwa miezi kadhaa,wakati ananiruhusu kurudi masomoni alisema 👇
"Mzee hata ukiuza nyasi zitanunuliwa,asante sana nenda shule"
Iko hivi…….
Umri unaenda pengine hata uzee unakaribia…..but kuna ndoto na goals haujazi-accomplish.
Wakati umri unavyozidi kukua ndivyo maradhi nayo yanazidi kukunyemelea, changamoto zinazidi kuwa nyingi na kubwa!!
Majukumu yanazidi, family issues, kids, ndoa/mahusiano, na unakuwa financially unstable.
The course ambayo ume-stick nayo kwa muda mrefu haijakupa matokeo yoyote, sana sana imekuletea changamoto zaidi na kukukosesha opportunities!!
HAPA SASA NDIO MTU ANAFIKIA MAAMUZI YA KUUZA SOUL!!
LIWALO NA LIWE POTELEA PWETE!
Very few of us….ndio tunaweza kushikilia bomba mpaka mwisho!!
No matter how tough the situation is!
Sio rahisi sana, wengi wanashindwa njiani katikati ya safari!
So far tumeshawapoteza wengi katikati ya hii safari….tuwaombee wanaoendelea kushikilia bomba Mungu awape imani na ustahimilivu!
@chapo255@SwahiliKid22 Mkubwa hakuna risk na makosa tunafanya kama ku engage na wana, its a human nature, huwa inashusha value na kuchukuliana oya oya automatically
@MarekaMalili@Mwinshehe07 "Matokeo hayawezi kudanganya."
Hayaangalii unaongea nini, unapanga nini, au unataka nini — yanaangalia ulichofanya kila siku kwa Uthabiti.
Hautengenezi Maisha yako kwa siku moja kubwa, unatengeneza kwa Maamuzi madogo ya kila siku.
Kuna kitu kinaitwa routines,nidhamu ya kufanya mambo sahihi kila siku,hata kama hujisikii.
Hakikisha unaweka kwenye ratiba yako yale yanayokujenga kimwili,kiakili na kinafsi.
Maana ukweli ni huu,matokeo hayawezi kudanganya, yanaakisi kile unachofanya kwa uthabiti kila siku.🤛🏼🙏🏼
Kuna wakati unapitia nyakati ngumu kiasi cha kutotamani kabisa mtu mwingine yeyote apitie magumu kama hayo.
Maumivu, machozi, aibu, fedheha na hata kuhisi kama hauna thamani tena katika maisha. Hizi ni nyakati ambazo hautamani hata adui yako apitie.
Lakini Mungu ameumba Dunia kwa namna ya tofauti sana, Hata katika nyakati hizo kuna muda lazima tu ukubali kumshukuru yeye kwa kila jambo.
Kipindi hiki utatambua na kukutana na watu wengine wanaopitia kama yakwako au hata zaidi yako. Hapo unajikuta unapata nguvu tena hata kama ulikuwa umekata tamaa.
Utagundua haupo peke yako na pengine Mungu anakupitisha katika njia hiyo kwa makusudi ili akurejeshe katika njia zake.
Ninaamini kuna wakati utafika na wote tutasema "Mungu ulinivusha" haijalishi ni gumu kiasi gani.. Tuendelee kuomba na kumshirikisha Mungu katika vita zetu kwani yeye ndie mwenye silaha zote. 🙏🏽🙏🏽