2 Corinthians 5:10
For we must all appear before the judgment seat of Christ, so that each one may receive good or evil, according to what he has done in the body.
"Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.” Mathayo 6:1
Saa Tisa Alasiri
SAA YA HURUMA YA MUNGU
Kwaajili ya Mateso Makali ya Bwana wetu Yesu Kristu, Utuhurumie sisi na dunia nzima
Baba wa Milele, tunakutolea Mwili na Damu, roho na umungu wa Mwanao mpenzi sana Bwana wetu Yesu Kristu, kwa kulipia dhambi zetu na dhambi za dunia nzima!
Ni rahisi kuwapenda watu wanaotupenda.
Ni rahisi kuwaheshimu wanaotuheshimu. Lakini tunafanyaje tunapokutana na watu wanaotuchukia, wanaotusema vibaya au wanaotamani tushindwe?
Vipimo hivi uwa vizito sana 🤭
Jenga maisha yako kabla hujashughulika sana na maisha ya wengine. Usiishi kwa kushindana na watu, usikate tamaa kwa sababu ya kuchelewa kufanikiwa, na usikubali chochote kikutoe kwenye kusudi lako. Jifunze kupenda bila kupoteza mwelekeo, kufanya kazi bila kuchoka na kusubiri bila kukata tamaa.
🌹🙏 OKTOBA, MWEZI WA ROZARI TAKATIFU📿
Mwezi huu wa kumi, tumrudie Mungu kwa njia ya Rozari Takatifu. Kwa njia ya Bikira Maria, tutafakari mafumbo ya maisha ya Kristo, tuimarishe imani yetu na kuziombea familia, Kanisa na ulimwengu mzima.
#RozariTakatifu#MweziWaRozari
"Mambo haya nimekuomba usininyime kabla sijafa: Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu. Nisije nikashiba nikakutukana nakusema Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini nikaiba na kulitaja bure jina la Mungu wangu" (Mith 30:7-9)
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina🙏
Ee Bwana unifanye niwe chombo cha amani yako,
• Palipo na chuki nilete mapendo
• Palipo na makosa nilete msamaha
• Palipo na shaka nilete imani
• Pasipo na matumaini nilete tumaini
• Palipo na giza nilete mwanga
• Palipo na huzuni nilete furaha
Mwezi Oktoba ni mwezi wa Rozari Takatifu.🌹🙏
Tusiuache mwezi huu upite bila kujenga upya au kuimarisha utamaduni wa kusali Rozari. Katika kila fumbo, tunatafakari maisha ya Kristo kwa macho ya Bikira Maria, tunaimarisha imani yetu na kujifunza kuyakabidhi maisha yetu kwa Mungu.
Usishindane na mtu aliyekuzidi uwezo. Kuna vita ambavyo ukivipigana huwezi kupata ushindi, bali maumivu, hasara na majuto. Na vita nyingine usipigane maana hupigani na unayemuona, unapigana na asiyeonekana/wasioonekana. Jua mipaka yako, chagua vita zako kwa hekima.
Today is the feast of St. Padre Pío of Pietrelcina.
Padre Pio was an Italian Capuchin Friar who was known for his piety and charity, as well as the gift of the stigmata.
He is the patron of civil defense volunteers and adolescents.
May he continue to intercede for us🙏🏽
Mt. Mathayo anatukumbusha kuwa Yesu hamwiti mtu kwa sababu ya ukamilifu wa maisha yake, bali kwa sababu ya upendo na neema yake. Mathayo aliacha meza ya ushuru na kumfuata Kristo. Nasi tukubali bila kusita pale neeema yake inapotujia.
Mt. Mathayo, Mtume na Mwinjili, utuombee. 🙏