Mithali 31:8_9..." Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; uwatetee watu wote waliioachwa peke yao; fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; uwapatie maskini na wahitaji haki yao"
‼️HAWA WATU NDO WALIUWA NDUGU ZETU WA OPERESHENI YA MKIRU, HUKO KIBITI‼️
Mwaka 2017 wakati wa Magufuli iliundwa Kanda Maalum ya Kipolisi ambayo ilipewa jina la MKIRU yani Mkurunga, Kibiti na Rufiji.
Wakati huo IGP alikuwa Simon Sirro na Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Mwigulu Nchemba.
Serikali ilianzisha Operation ya MKIRU lengo lilikuwa ni kupambana na Magaidi ambao walikuwa wanatoka Msumbiji na kujificha kwenye msitu wa Kibiti ambapo kwa wakati huo walikuwa wakiuwa Viongozi wa Serikali za mitaa/Vijiji Wenyeviti, maafisa watendaji na Polisi.
Kwenye operesheni ya MKIRU kwa upande wa TISS kikosi chao kilikuwa kinaongozwa na Fadhili Saga huyu wa kwanza kwenye hii picha.
Kwa upande wa Jeshi la Polisi kikosi chao kilikuwa kinaongozwa na Faustine Mafwele ambae alikuwa anasaidiana kwa karibu na George Bagyemu, huyu wa tatu kwenye hii picha.
Upande wa JWTZ walichukuliwa Makomandoo kutoka kambi ya Ngerengere ambao walikuwa wanaongozwa Msindai (Huyu ni mdogo wa Mgana Msindai yule Mwanaccm wa Singida)
Hivi vikosi vitatu vilitengeneza kikosi kimoja ambacho kilikuwa kinasimamiwa na Fadhili na Mafwele wengi walidhan kinaenda kudeal na Magaidi lakin walipoanza operation yao mambo yalikuwa tofauti maana waligeuka na kuanza kuuwa raia.
Hii operesheni ilikuwa ni ya mauaji dhidi ya Wananchi wasiokuwa na hatia ambao ni wakazi wa Kibiti, Rufiji na Mkurunga, hawa wauaji na vikosi vyao walipofika tu Kibiti walianza kuteka Wananchi wasiokuwa hatia, walikuwa wanavamia makazi ya wananchi wakikuta Vijana wa kiume/Baba zao walikuwa wanawabeba wote na kwenda nao msituni ambako kwa mujibu wa Uchunguzi ambao alifanya Azory Gwanda walikuwa wanawatesa sana huku wakiwahoji, wakimaliza kuwatesa wanawauwa.
Wahanga wa kubwa wa Operesheni ya MKIRU walikuwa ni Wanachama wa Chama cha CUF na Waislam ambao walikuwa na Imani kali na wengine walikuwa ni wanaccm ambao waliangukia kundi la Waislam wenye Imani kali.
Wakati operesheni hii inaendelea Wizara ya Habari iliwaandikia memo wamiliki wa vyombo vya Habari kwamba hawatakiwi kuandika chochote kuhusu mambo ambayo yalikuwa yanaendelea huko Kibiti kwenye Operation ya MKIRU, Wananchi walikuwa wanapaza sauti zao kuhusu Mauaji ya kinyama dhidi ya ndugu zao lakin sauti zao zilikuwa hazisikiki kwasababu Serikali ilikuwa imefanikiwa kudhibiti taarifa.
Ndipo Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi Azory Gwanda akajitoa muhanga akaenda Kibiti alifanya Uchunguzi akabaini mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea huko ikiwemo Mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia ambapo badae Mwananchi wakawa wanachapisha Habari kuhusu mambo yaliyokuwa yanaendelea huko Kibiti.
Waliokuwa wanaendesha Operation hiyo walipoona mambo ya Kibiti yameanza kuandikwa na mjadala umeanza kushika kasi kwenye mitandao, waliamua kumteka na kumpoteza Azory Gwanda na aliyeongoza kikosi hicho ni Fadhili Saga na kwa mujibu wa mtoa taarifa Fadhili Saga yeye ndo aliyempiga risasi na kumuua Azory Gwanda baada ya kumuuwa walimzika kwenye msitu Kibiti pamoja na miili ya watu wengine.
Ndani ya msitu huo kuna kuna makaburi mengi ya halaiki ya watu waliouwawa kwenye operation hiyo ambapo Idadi ya watu waliouwawa inakadiliwa kuwa zaidi ya elfu mbili.
Baada ya Operation ya MKIRU Fadhili alipandishwa cheo na kuwa Mkuu wa Operation wa TISS.
Mafwele alipandishwa cheo na kuwa Zonal Criminal Officer na George Bagyemu akapandishwa cheo kuwa na Deputy Zonal Crime Officer.
Hawa watu ipo siku watatuonyesha Makaburi ya ndugu zetu waliowauwa na kuwazika kwenye msitu wa Kibiti.
Siku ikitokea tukapata Rais mpenda Haki ambae anathamini uhai wa watu, halafu akaunda Tume ya kuchunguza kuhusu operation ya MKIRU tutajua mengi zaidi ya haya.
Dear Augustino Lissu, stay stronger and thank you for showing up to demand your father’s liberty. SC Tundu Lissu is extremely proud of you. Stay vigilant & unbowed, son. Wear that AURA and walk his talk, young🐐!
🚨 LEO APRILI 23 NI SIKU KUU KWA TANZANIA!
Baada ya siku 153, ushahidi kutoka kwa Watanzania zaidi ya 63,000, Mohamed Chande Othman atakabidhi ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Mauaji ya Oktoba 29 kwa mtuhumiwa number 1, @SuluhuSamia , ripoti iliyopambwa vizuri inayowalaumu waathirika na upinzani huku ikiwalinda wahalifu halisi. Na kumsifia aliyetoa amri ya kuuwa @SuluhuSamia .
Chande amesema wamehoji watu 63,000, ili tume yake batili ionekane imefanya kazi vizuri kupitia hata viwango vya kimataifa.
#RipotiYaChande #MauajiYaOktoba29 #HakiKwaTanzania #GranHermanoGeneraciónDorada
Leo nitarejea kutazama picha na video za mauaji ya Oktoba 2025 ili nisiwasahau Watz wenzangu waliouawa na watu wenye uchu wa fedha na madaraka. Nafsi yangu inakataa kulishwa ajenda za wauaji.
As long as hakuna uwajibikaji kwa wauaji, nitakuwa mpumbavu kusikiliza chochote.
Mnakumbuka gari lililobeba wauaji?
Hebu mniambie hii gari ya T555EZP si ndo yenyewe? Maana hii wheelcover na muundo ni samesame!
Wanadunda tu mtaani bila woga!
Alafu litume lije kutuambia eti fyokofyoko!
Hili gari tunataka kujua ni ya nani, idara gani
We need answers!
#TutaelewanaTu
#SamiaMustGo
#TanzaniaMassacre
Tulisema TUTAANDAMANA.
Ukasema hakutakuwa na nywinywi wala nywinywinywi.
TULIANDAMANA kuzuia upumbavu wenu mlioita uchaguzi.
Ultimately, hakukuwa na uchaguzi.
Kwanini unalazimisha Chande aseme tulichochea vurugu?
Truth is, and we all know; TULIANDAMANA kuzuia upumbavu wako!
Hawa ni vijana wa MAFWELE wanaitwa "Tembo SABA" na kambi yao ilikuwa CHANG'OMBE POLICE STATION-Walifunga hadi Turubai.
Siku ya MO29 hawa walikuwa na kazi moja tuu-kupiga RISASI ZA VICHWA watanzania. Hapa walipigwa risasi mpaka watoto wa miaka 7 eti nao wanataka kupindua nchi.
Gari hii ambayo walikuwa wanatembelea ilijaa "RISASI" Kwenye kindoo cha lita 20. Wote tunajua Risasi za askari zinahesabiwa, hawa vibaka walitoa wapi silaha zote hizi na kwa kibali cha nani?
Nategemea kesho CHANDE na ripoti yake aje na majina ya hawa VIBAKA maana boss wao ni MAFWELE anawajua vizuri. Pale CHANG'OMBE POLICE STATION ndio ilikuwa kambi yao.
Waliuwa watanzania kwa maelfu na walionekana wakishirikiana na POLISI wenye uniform mara kwa mara (VIDEO ZA USHAHIDI ZIPO).
Kesho chande jua unaongea na taifa la vijana wenye IQ KUBWA sana na kumbu kumbu zetu zipo mtandaoni.
Kuna uwezekano baada ya Ripoti yako ukaibua vuguvugu jipya la MAANDAMANO-bado vidonda vyetu ni vibichi usilete ripoti ya kutuvuruga kabisa.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Hii video mpya ya Oktoba 29, Wananchi wanasikika wakisema Serikali inavunja Katiba.
Halafu Nduli Idd Amin Mama anasema waliondamana walikuwa hawajui kwanini wameandamana kwamba hawakuwa na sababu walifuata mkumbo.🚮🚮
Kwamba Jeshi la Polisi mnataka mie nifike kwa DCI?
Mnataka nijilete kwenu nyie ambao April 24, 2025 mliniteka pale Mahakama ya Kisutu mkakaa na Mimi Central Police kisha mkanijazisha na kunisainisha fomu ili nijidhamini halafu nimetoka tu nje mkanigeuka, Mkanikamata tena na kuniweka lockup. Nijilete tena?
Nijilete kwenu nyie ambao Oktoba 29 mmeuwa kwa risasi Watanganyika wenzangu zaidi ya elfu kumi na wengine mmewapa vilema vya maisha na wengine mpaka leo wanauguza majeraha ya risasi?
Nijilete kwenu nyie ambao mpaka leo mmeshindwa kuwakamata watu waliofanya jaribio la kumuua Mhe. Lissu kwa risasi 37 September 7, 2017 kule Dodoma.?
Yani mimi na akili zangu nijilete machinjioni si hata mtoto angu atanishangaa?😂😂😂
Labda niwambie tu kwasasa nna kazi kubwa ya kupigania ukombozi wa Taifa letu, tupate Katiba Mpya, Tume huru ya Uchaguzi tuwe na mifumo Imara ya utoaji Haki ili wote tuishi kwa usawa kila Mwananchi aifurahie nchi yake na ahisi kuwa salama.
Baada ya hapo ndio tunaweza kuombana ushahidi wa andiko langu au mimi kujileta kwenu kwasasa acha niwasaidieni kwanza kupambania mifumo ibadilike na kazi yenu itakuwa rahisi. Hata mimi nitawapa ushirikiano huo muda ukifika. Tofauti na hapo sijileti machinjioni ng'o.
Huyu aliyebeba bendera yetu ni Daniel aka Lissu wa Kitaa. Alipigwa risasi akauwawa akiwa anadai uadilifu wa bendera yetu. Mdogo wake pia aliuwawa.
Samia atalipia haya mauwaji ya halaiki. Sisi hatuko bound na blah blah za Chande aka Kiande.
RIP Daniel aka Lissu wa Kitaa!!
Yani njaa zitawatokea puani! Yani waandishi uchwara mmejikusanya kujifanya manahamu na kipeperushi cha Chande!
Tanzania ya sasa sio ya zamani ya kuendeshwa kwa propaganda! Fanyeni kazi ya uandishi acheni ushenzi!
HABARI:
Serikali ya Malaysia imetangaza kuwa watumishi wa umma katika wizara, taasisi za serikali, mashirika ya umma pamoja na kampuni zinazomilikiwa na serikali wataanza kufanya kazi wakiwa nyumbani kuanzia Aprili 15, 2026.
Hatua hiyo inalenga kupunguza matumizi ya mafuta huku nchi ikianza kuathiriwa na mgogoro wa nishati unaosababishwa na vita vya Mashariki ya Kati.
Akizungumza Aprili 1, 2026, Waziri Mkuu Anwar Ibrahim alisema uamuzi huo umeidhinishwa na Baraza la Mawaziri ili kusaidia kudhibiti matumizi ya mafuta na kuhakikisha upatikanaji wa nishati unaendelea kuwa thabiti. Hata hivyo, alibainisha kuwa maelezo zaidi kuhusu utekelezaji wa mpango huo yatatolewa baadaye.
Malaysia ni miongoni mwa nchi zinazotoa ruzuku kubwa ya mafuta, ambapo wananchi wanaostahili hulipa takribani ringgit 1.99 (sawa na dola za Marekani 0.49) kwa lita moja ya petroli.
Hata hivyo, kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani na hali ya sintofahamu katika usambazaji wa nishati, serikali imepunguza kiwango cha mafuta ya ruzuku kutoka lita 300 hadi lita 200 kwa mwezi kwa kila mnufaika. Bei ya mafuta yasiyo na ruzuku itaendelea kuendana na soko la dunia.
Hatua hizi zinachukuliwa wakati Iran ikiendelea kudhibiti kwa karibu Mlango wa Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani, hali inayochangia kupanda kwa bei na kuathiri upatikanaji wa nishati katika nchi mbalimbali.
Wakati huohuo, serikali ya Malaysia imesema meli zake za mafuta zitaendelea kuruhusiwa kupita katika eneo hilo kutokana na uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Malaysia na Iran.
Waziri Mkuu Anwar pia alimshukuru Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, kwa kuruhusu meli za mafuta za Malaysia na wafanyakazi wake kuendelea na safari zao kwa usalama.
PONGEZI PONGEZI PONGEZI
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali @MsigwaGerson 👇 TANZANIA ndiyo NCHI PEKEE DUNIANI kwa sasa, ambapo RAIS aliamua KUONDOKA IKULU na KWENDA PORINI KUREKODI FILAMU. Inabidi MARAIS wengine waje KUJIFUNZA Tanzania namna ya KUREKODI FILAMU PORINI.
Serikali ya Namibia imeidhinisha punguzo la asilimia 50 la ushuru wa mafuta kwa miezi mitatu kuanzia Aprili ili kuwalinda watumiaji kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta Duniani kunakosabanishwa na kuongezeka kwa gharama za uagizaji zinazohusishwa na vita vinavyoendelea Kati ya Marekani, Israel na Iran. ya Kati.
Waziri wa Viwanda, Madini na Nishati wa Namibia, Modestus Amutse amesema Serikali ya Nchi hiyo itatumia takriban dola milioni 500 za Namibia kutoka Mfuko wa Nishati wa Kitaifa ili kupunguza athari kwa watumiaji
Amutse amesema hatua hiyo imekuja baada ya baraza la Mawaziri kulijadili suala hilo na kuazimia kuingilia kati ipasavyo ili kutoa unafuu kwa watumiaji wa mafuta Nchini humo na kubainisha kwamba wizara itaendelea kufuatilia maendeleo na kutekeleza hatua inapowezekana ili kuwalinda watumiaji huku ikihakikisha usalama wa usambazaji wa mafuta.
Kiongozi huyo amesema kuanzia Aprili 01, 2026 bei za petroli zitaongezeka kwa dola 2.50 za Namibia (karibu dola 0.15 za Marekani) kwa lita, huku daraja zote mbili za dizeli zikiongezeka kwa dola 4 za Namibia kwa lita.
#KitengeUpdates