WAZIRI MHAGAMA KUSHUGHULIKIA HOJA ZA WAUGUZI.
Na WAF, DODOMA
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Oktoba 17, 2024 amekutana na Uongozi wa Chama cha Wauguzi na Ukunga Tanzania (TANNA) na kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za wauguzi zilizo jitokeza wakati wa mkutano wa mwaka uliofanyika 12 Mei, 2024 ili kuongeza ubora wa Huduma kwa wananchi.
Mhe. Mhagama amesema kuwa anatambua mchango na kazi kubwa inayofanywa na wauguzi na wakunga katika sekta ya afya hivyo anawapongeza kwa kazi nzuri inayofanyika katika kuwahudumia wananchi
Amesema moja ya jukumu kubwa analofanyia kazi kwa sasa ni kuhakikisha wauguzi na wakunga wanapandishwa madaraja kama ilivyo kwa kada zingine.
“Wakati tunafanyia kazi changamoto zenu tusaidieni kusimamia maadli kwa wauguzi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi”, ametoa rai Mhe.Mhagama
Amesema serikali kupitia wizara ya Afya inafanya kazi kuhakikisha inatatua changamoto wanazokabiliana nazo wauguzi na wakunga hivyo waendelee kuchapa kazi kwa kufata miiko na maadili ya taaluma wanapo wahudumia wananchi
Kwa upande wake rais wa Chama cha Wauguzi na Ukunga Tanzania ( TANNA), Alexender Baluhya amesema kuwa wauguzi na wakunga wanaimani na serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani kuwa ni sikivu na itatatua changamoto zao kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi wao
Amefafanua kuwa lengo la kukutana na Mhe.Mhagama ni kufatilia utekelezaji wa hoja za wauguzi zilizotolewa katika mkutano wa mwaka uliofanyika pale Mkoani Tanga- na hoja hizo ikiwemo kupandishwa madaraja.
Chama cha Wauguzi Tanzania, kinawakumbusha wanachama, Wataalamu kada ya Afya na Watanzania wote kwa ujumla juu ya namna Bora ya kujikinga na mlipuko wa Ugonjwa wa Mpox. Kwa taarifa zaidi pitia kipeperushi kilichoambatanishwa hapa chini. Kwa taarifa, Elimu na Ushauri piga 199 BURE
Chama cha Wauguzi Tanzania tunaungana na familia katika jitihada za kumtafuta mwanzachama wetu aliyepotea katika mazingira tatanishi. Aidha tunatoa Rai kwa Wauguzi wote kuendelea kuchukua tahadhari lkn pia kutoa taarifa mapem inapobainika mwenzetu haonekani bila taarifa yoyote.
TANZIA
TANNA tunasikitaka kutangaza kifo cha Muuguzi Elinsia Japhet wa Hospitali ya Wilaya ya Meru aliyetoweka ghafla kuanzia tarehe 27/06/2024 hadi tarehe 04/07/2024 mwili wake ulipoonekana katika maeneo ya mto Nduruma.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. https://t.co/VOg1bPPavd
Happy birthday Rais wetu Dkt @SuluhuSamia . Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu yenye heri, afya njema na maono makubwa zaidi ya kuendelea kuiongoza vyema nchi yetu.
Happy birthday Rais wetu Dkt @SuluhuSamia . Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu yenye heri, afya njema na maono makubwa zaidi ya kuendelea kuiongoza vyema nchi yetu.
Mkazi wa Mburahati, Jijini Dar es Salaam, Bi. Hamisa Tuli ametoa zawadi ya keki kwa Wauguzi wa jengo la wazazi hospital ya Taifa Muhimbil ikiwa ni ishara ya kuwashukuru kutokana na huduma nzuri aliyopewa na kujifungua salama. Mama na mtoto wake tayari wameruhusiwa kwenda nyumban
Ndugu Mwananchi, ungana na Wauguzi nchini kuchangia wahanga wa maafa ya Mafuriko yaliyotokea huko Hanang Mkoani Manyara kupitia njia za malipo zilizopo kwenye tangazo hili nawe utajichotea Baraka kwa kushiriki tendo hili la huruma. Karibu sana.
@ummymwalimu Hongera sana Mheshimiwa Waziri kwa hatua hii kubwa na yenye tija kwa afya nchini na Muswada kupita bungeni kama chama Cha kitaaluma TANNA tunakupongeza sana na wizara kwa ujumla kufanikisha hili