Don't be a nice person.
A nice person always agrees and approves.
Such persons are not valued for their opinion. Be a kind person who can disagree politely.
Afya ni huduma mahususi, yenye gharama kulingana na umahususi wenyewe, mtoa huduma mpokea huduma hufikia maafikiano ya gharama baada ya kusikilizana na kushauriana. Wanunuzi wa huduma wana mategemeo na matarajio yao ya ama huduma yenyewe ama kinachoandamana na huduma hizo, vikiwemo;- umahiri, upendo, unyenyekevu, kusikilizwa kwa makini, usiri, mazingira, muda kabla ya kumuona daktari, muda wa kukaa na daktari, uharaka na wepesi wa kufikia vipimo, kufuatiliwa baada ya huduma nk. Mamno yote haya na mengine mengi huandaliwa kukidhi haya ya wateja wa makundi tofauti, mahali tofauti na kwa gharama tofauti. Suala hapa ni kuwa kuna gharama tofauti kwa huduma tofauti katika kituo kimoja au vituo tofauti na gharama zenyewe anapaswa kuzilipa mteja. Suala kama mteja analipa zote mwenyewe, analipiwa na wakala wake (dalali wa kukusanya na kulipa) au analipiwa sehemu au zote ni suala la utaratibu tu na ambao haupaswa kuingilia gharama halisi. Kulazimisha kuwa lazima gharama ziwe kiasi fulani ni kujiaminisha kuwa wewe una akili na uwezo wa kujua tabia za ununuzi ( customer needs and buying behaviour) suala ambalo sio tu kujikweza bali ni kuwadharau wanaotafuta huduma wanazozihitaji. Kuondokana na changamoto hizi
;- inashauriwa kuwa uandaliwe utaratibu mahususi ambao kila anayehitaji huduma yenye gharama zaidi ya uwezo anayemlipia apewe fursa ya kulipia gharama za ziada (cost-sharing/topping up) @wizara_afyatz