Kwenye safari ya maisha lazima ujue Kuna muda utafika Kuna njia itakubidi upitie wewe peke yako na Mungu wako tu hakuna mtu yoyote ambaye ataweza kukushika mkono.
Wakati mwingine watu wanasamehe sio kwa sababu hawaoni ukubwa wa kosa walilokosewa na sio kwamba hawajui ukubwa wa kosa hausameheki bali wanasamehe kwa sababu maisha yao yanahitaji amani zaidi kuliko kubeba chuki mioyoni.
Kuwa makini na unaoanza kujenga nao maisha usije jikuta ulitumika kwenye ramani na msingi tu halafu finishing wakafanya wengine.
Usitumike kwenye ramani na misingi tu halafu kwenye finishing ukawa mtazamaji wakati huko ndio kwenye matunda yenyewe ya jasho lako.
Kabla ya kumfanyia mtu ubaya hakikisha hakuna siku utamuhitaji tena kwenye maisha yako
Dunia ina tabia ya kurudisha watu kwenye maisha sasa siku usije jikuta uliyemfanyia ubaya ndio anatakiwa kukusaidia wewe na hapo ndio utaanza kujuta kwa ubaya uliomfanyia.
Usiwa block maadui zako wote bakiza japo wawili au watatu ili wawe wanapeleka taarifa kwenye makao yao makuu kwamba ni kiasi gani uadui wao haujamzuia Mungu kukubariki.
Ukiona mtu ambaye ulikuwa unamuamini na kumthamini amekusaliti basi jua ni wakati sahihi ambao ulifika wa Mungu kukuonyesha uhalisia wa mtu huyo baada ya kukaa na wewe kwenye uigizaji kwa muda mrefu.
Ukiona mtu amekusaliti jua huyo hakuwahi kuwa mwema bali aliigiza wema wake.
Usijutie kupoteza mtu ambaye uliamini anakujali na kukuthamini bali jutia kwa wewe kupoteza utu wako juu ya mtu ambaye uliamini anakupenda na kukuthamini.
Utu wako una thamani kubwa saana dhidi ya mtu ambaye wewe unaamini unamjali na kumthamini.
Kidole kimoja ambacho kinakufuta machozi wakati wa mapito magumu kina thamani kubwa kuliko mikono 1000 ambayo inakupigia makofi wakati uko kwenye kipindi Cha mafanikio.
Kuna watu kwenye maisha hutakiwi kuwapa nafasi ya pili kuwa karibu yako mana ni sawa na kuwapa risasi nyingine wakati unajua ya kwanza ilikukosa na lengo lao ilikuwa sio kujeruhi bali kuua kabisa.
Wapo wa nafasi ya pili lakini wapo ambao unatakiwa kabisa kuvunja system yao.
Ushawahi muambia mtu nakupenda sana halafu akajibu "THANK YOU" yaani Kuna kama ka hasira flani unasikia hivi mana jibu linakuwa kama kinafiki nafiki hivi.
Sasa nimejua kwanini inauma baada ya kuona hizi "THANK YOU" za wachezaji.
Unaachwa halafu "THANK YOU" daah.
Kinachounguza mshumaa sio moto wa nje bali ni utambi ule ule ambao uko ndani ya mshumaa ndio unashiriki kuunguza mshumaa mpaka uishe.
Ndio hivyo hivyo binadamu wa ndani yetu kabisa tunaowaamini ndio wanaotusaliti na kutuombea mabaya ili tufeli wao nafsi zao ziridhike.
Jitahidi saana kujua thamani ya mtu ambaye anakuthamini Kwa sababu ipo siku unaweza kusema kuna watu wamemlisha maneno ili asikupe thamani tenaa kumbe ni matendo yako tu ndio yamebadilisha kila kitu.
Ukiona kuna mtu anakuthamini na aameamua kukuweka karibu yake basi jitahidi kujua mipaka na usijenge mazoea ipo siku mazoea yako yatakufanya uvuke mipaka na ndio hapo atakuweka mbali na hutokaa uwe karibu yake tena.
Wenye akili hawajengi mazoea na watu wenye thamani kwao.
Siku hizi wanawake hawana machozi ya kulia tenaa siku za ndoa zao sababu mpaka wanafika kwenye ndoa washapitia maumivu ambayo yamewatoa machozi kweli kwelii.
Wengine wametoka kwenye familia ambazo hata ndugu kukuachia kiatu tu ni mpaka kiwe hakimtoshi kinambana la sivyo bora atembee peke kwa hiyo ukiona mtu anajipambania kujikwamua usimuharibie.
Watu wanapambana ili kujizuia kuendelea kutegemea vya ndugu.
Jamanieeh viongozi wa @yangasc1935 hebu maalizeni hizo "THANK YOU" zilizobaki tukae na amani.
Yaani Kila saa mtu unapita kwenye page kuchungulia kwamba nani kaambiwa "THANK YOU"
Halafu tunaotaka muwaambie hivyo hamuwaambii mnawaambia watu wa maana.
Tunapambana sana na maisha sio kwamba hatuna ndugu wenye mali wapo ila tunapambana ili tukiwapigia simu wapokee wasijekudhani tukipiga ni kwa ajili ya kuomba hela tu.
Kuvunja urafiki wangu na wewe haina maana kwamba unatakiwa kuniongeza kwenye kundi la maadui wako.
Mimi sio adui yako na ukweli bado natamani kukuona unakula ila tu sio kwenye meza yangu.
Naweza nisiwe rafiki yako lakini sio adui yako.