‼️TAARIFA YA KUTEKWA KIJANA WA NCHIMBI‼️
Huyu kijana ni Mwanachama wa CCM anaitwa Mussa Ismail Badi ni mmoja kati ya vijana wa Emmanuel John Nchimbi.
Alitekwa na watu wasiojulikana wakati anatoka kuswali Msikiti wa Manyema, Kinondoni Mkwajuni ila hata wanaccm wenzake wanaogopa kumpazia sauti.
Ukiachana na kwamba ni Mwanachama wa CCM lakini pia ni mwana kikundi wa Lumumba Alliance Club (LAC) na tangia atekwe mpaka sasa ni miezi minne imepita hakuna anayejua taarifa zake lakini pia huyu kijana anaundugu na aliyewahi kuwa Katibu wa Wizara ya Afya Blandina Nyoni.
Kila mtu atafikiwa kwa wakati wake, tuungane kupigania Haki na kukemea hivi vitendo viovu.