‼️DEREVA WA MHE. HECHE AKUTWA AMEKUFA DAMU DAMU ZIMETAPAKAA SAKAFUNI.‼️
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo Suez Dani Maradufu ambaye ni dereva wa Makamu wa Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche
Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma.
Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi.
Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito.
Taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa.
Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
Rais wa Rwanda Paul Kagame amezungumzia Mapinduzi ya sasa, akisema Mapinduzi zaidi yanaweza kutokea na akizungumzia haja ya kuwazuia Vijana wanaojulikana kwa jina la Gen-Z kutaka kupindua Serikali.
Kumekuwa na Mapinduzi 130 katika nchi 36 za Afrika tangu 1952 muda mfupi kabla ya nchi za Kiafrika kupata Uhuru kutoka kwa ukoloni. Kumekuwa na karibu Mapinduzi 10 katika miaka mitano iliyopita.
Aliulizwa kuhusu suala hilo huku kukiwa na Mapinduzi nchini Madagascar mwezi uliopita na Guinea-Bissau tangu Jumatano, Rais Kagame alisema watu wanachopaswa kujiuliza ni kujua sababu ya Mapinduzi hayo.
Kagame anakiri kuwa nchi za Kiafrika ikiwa ni pamoja na ile aliyokulia ina matatizo mengi, kwamba jinsi Watawala wanavyoyaendesha nchi ndiyo yanaweza kusababisha matatizo ambayo yanapelekea kutokea Mapinduzi.
#KitengeUpdates
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 115
Anaendelea Shahidi namba 3 wa Jamhuri Samuel Elibariki Kaaya
Baada ya hilo kutokea nilienda maabara kwa ajili ya kuandaa vifaa vya uchunguzi.
Barua zote mbili tukianza na ile ya FB/PH/LAB/106/2025 Ilikuwa inahusu jalada la kuchunguza uchapishaji wa taarifa za uongo na lile lenye namba /PH/LAB/107/2025 ikiwa na kosa la uhaini.
Thawabu ; umesema baada ya kuwa assigned ulienda maabara, ieleze mahakama nini ulifanya nini?
Nilifika maabara na kufanya maandalizi ya vifaa vyangu vya uchunguzi.
Maandalizi niliyoyafanya ni kuandaa vifaa chunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya uchunguzi.
Baada ya kumaliza kuandaa computer, printer kwaajili ya uchunguzi.
Tukumbuke kwamba nilikuwa na barua mbili ambazo nilikuwa assigned kuzifanyia kazi hivyo niliamua kusoma barua hizo ili kufaham matakwa ya requesting authority wanataka nini.
Mhe Jaji Barua moja ilikuwa inahusu kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na nyingine ilikuwa inahusu uhaini.
Barua ya uhaini ilikuwa na kumbukumbu namba DA.223/476/01B/169.
Barua hiyo pamoja na muhtasari ilinihitaji kufanya mambo yafuatayo; ilihitaji chanzo cha picha mjongeo inayopatikana kwenye flash disk aina ya XIOXIA, kuchunguza uthibitisho wa uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye flash disk, nichunguze chanzo cha picha mjongeo iliyopo kwenye memory card.
Pia nichunguze uhalisia wa maudhui ya picha mjongeo iliyopo kwenye memory card aina ya Aldeepo, kufanya ulinganisho wa maudhui ya picha mjongeo iliyoko kwenye flash disk aina ya XIOXIA kama yanafanana na maudhui ya picha mjongeo iliyokuwepo kwenye memory card aina ya Aldeepo.
Kiuhalisia huyu shahidi anazungumza jambo hilo hilo moja na Wakili wa Serikali anarudia kuuliza swali hilo hilo mara tatu tatu mpaka mtu unaona uvivu kuandika.
Mfano hiyo habari ya video ilisema nini au Mh. Lissu alisema nini kwenye mazungumzo yake na watia nia kwa namna kesi inavyoenda hata sio tatizo na amekuwa hapingi kuwa maneno yale sio yakwake. Swali lake na hoja yake ni kwamba je hayo aliyosema ni kosa kisheria? Ni Uhaini?
Sasa hawa mashahidi watupotezea muda wa siku kadhaa kutuambia namna walivyochunguza video wakati hiyo video mtuhumiwa hana pingamizi nayo. Nafahamu zipo hatua za kisheria zinapaswa kufuatwa ili exhibits zipokelewe Mahakamani lakini kwa shahidi huyu nimewauliza hata Mawakili wanasema kwa kiasi kikubwa wanapoteza tu muda. Mengine hata sio matakwa ya kisheria.
Acha tuendelee nae na tunasubiri muda wa yeye kuanza kuulizwa maswali ya Dodoso na Mshitakiwa ndio tutaelewana zaidi.
Samuel Kaaya: Pia niliambiwa nichunguze maudhui yafuatayo kama yanapatikana kwenye flash disk hiyo, maudhui hayo ni haya;
"wanasema hivi msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kabisa maana tutazuia uchaguzi, hivyo tutahamasisha uasi, hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko, tunaenda kukinukisha sana sana, uchaguzi huu tutauvuruga maana tunaenda kukinukisha vibaya sana."
Nilifanya uhakiki wa vifaa vya uchunguzi kwa maana ya computer maalumu kwaajili ya kufanyia uchunguzi huo, printer maalum aina ya Epson, nilikagua program endeshi kwa maana ya operating system window eleven, programu chunguzi kwa maana ya forensic software and security software amped five na ampend authenticate.
Waheshimiwa majaji naomba nieleze maana ya amped five na amped authenticate.
Ampend authenticate inafanya basic and advance image analysis, pia inafanya basic and advance video analysis pia inafanya utambuzi wa sura kwa maana ya facial recognition Waheshimiwa majaji nilitazama pia programu linzi kwa maana ya security software.
Hii programu linzi ni Kaspersky antivirus ambayo kazi yake ni kulinda programu endeshi pamoja na programu zote zilizopo kwenye computer hiyo na pia inalinda vielelezo unavyovipokea visiliwe na virus au malware.
Part 116 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 17, 2025
Jana tuliishia part 113 so leo tunaendelea na -;
Part 114
Imepigwa high courttttttt watu wote wamesimama.
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.
Karani anasoma namba ya kesi.
Anasimama Wakili Mkuu wa Serikali anatambulisha jopo lake.
Renatus Mkude anamwambia Jaji anaomba Thawabu Issa aendelee alipoishia jana.
Shahidi ulisema kwamba baada ya kufanya analysis ya picha nini huwa kinafuata?
Baada ya kumaliza kufanya hio analysis kinachofanyika ni kuscreenshot ambako ni kupiga picha kutumia interface ya kioo taarifa za kidigitali kupitia metadata.
Baada ya kuscreenshot nitazichapisha kwa maana ya kuziprint kwa ajili ya kuambatanisha na taarifa ntakayoiandaa kwa ajili ya Uchunguzi.
Baada ya kufikia hio hatua naandaa tarifa ya uchunguzi kwa kurejea uchunguzi niliofanya kwa kuangalia police notebook na taarifa nilizoandika.
Taarifa hio huwa inaenda sambamba na covering letter na covering letter kwa ajili ya kuwajibu requesting authority walioomba niwajibu baada ya kufanya uchunguzi huo.
Baada ya kuandaa tarifa hiyo taarifa ya uchunguzi inakuwa na majina ya mchunguzi, logo ya jeshi la polisi, mchunguzi akishamaliza kuandaa tarifa hiyo ataisign, kugonga muhuri wa commission ya uchunguzi wa sayansi jinai (forensic).
Baada ya kugonga muhuri itasainiwa na mnadhimu wa sayansi jinai kwa niaba ya kamishna wa uchunguzi jinai.
Kama mnadhim hayuko basi afisa kwenye rank ya assistant commissioner ataisign.
Mchunguzi atapaki vielelezo kwenye bahasha, atasign bahasha iliyobeba vielelezo na kugonga muhuri.
Barua na covering letter tunaweka kwenye bahasha na kuandika maeneo zinakoenda, kusign na kuweka muhuri.
Baada ya hapo ofisi itawasilana na requesting authority kupata majibu ya kielelezo cha uchunguzi husika.
Iambie mahakama tarehe 8 Mwezi wa 04, 2025 ulikuwa wapi?
Samwel: Kama afisa mchunguzi wa zamu katika kitengo cha picha nilipokea barua mbili zenye kumbukumbu Na DA. 223/476/01DB/168 nyingine ikiwa DA.223/476/01DB/169 na ikiwa imeambatana na flash disk moja aina ya XIOXIA yenye ukubwa wa GB 8 Na flash disc ikiwa na alama ya DM na Ilikuwa iko attached Na. PF145 (exhibit label)
kielelezo kingine kilikuwa Secured Digital SD Adapter ilikuwa imepewa alama ya X Sticker na adaptor hio ilikuwa ina rangi nyeusi ndani ya SD Adaptor kulikuwa na memory card aina ya aldeepo.
Kielelezo hiko kilikuwa kwenye kibahasha kidogo kilichokuwa attached na PF-145 exhibit level
Waheshimiwa majaji barua hizo na vielelezo hivyo vililetwa na Assistant inspector Michael Gyumi.
Vikitokea ofisi ya mkuu wa upelelezi kanda maalum ya Dar es salaam.
Baada ya kupokea vielelezo hivyo na kusign dispatch book Waheshimiwa majaji nilihakiki vielelezo nilivyoletewa kama vinakidhi matakwa ya uchunguzi.
Nilihakiki vifaa vilivyoletwa kama ndivyo vilivoandikwa kwenye barua ya requesting authority.
Katika kuhakiki nilibaini vinakidhi matakwa ya uchunguzi wa kisayansi.
Katika maabara yetu tunapokea vifaa vibebeshi ni kama vile flash disk, memory card baada ya kujiridhisha na uhakiki wa vielelezo nilivyoletewa nilisajili vielelezo hivyo laboratory book register PF 113.
Nilisajili kwa barua yenye kumbukumbu namba DA. 223/476/01B/168 nilisajili kwa namba FB/PH/LAB/106/2025 na barua yenye kumbukumbu namba DA.223/476/01D/169.
Nilimuandikia hizo namba Insp. Michael Gyumi kwa ajili ya ufuatiliaji.
Zile nambari zinatokana na sequence and series jinsi tupokeavyo vielelezo.
Kikipokelewa cha kwanza January kitaandikwa namba moja.
Tunakwenda hivyo hivyo hadi mwisho.
Nilifungua majalada mawili ya uchunguzi wa kimaabara jalada hilo lilirejea namba nilizosajili kwenye PF 113.
Na baada ya usajili huo nikapeleka kwa Mkuu wa kitengo kwa ajli ya assignment kwa hayo majalada niliyoyafungua kwa ajili ya uchunguzi.
Part 115 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
Nimeumia sana kwakweli toka jana, nimejiona ni kama Underground ninaye anza muziki😁
Eti imagine toka tumetoa huu wimbo hakuna Media hata moja
(Radio wala Online Media) ya 🇹🇿 iliyonivutia konga kwa ajili ya interview😁
Nimefanya na media za Kenya tu!!
Wanangu wamenikaushia kauuuu
kimya kama wanaaga maiti vile!!😁
Ni kama wanaona huu wimbo umekaa kaa kuondoka na wasio na ITHIBATI!!😁
Kweli nyama ngumu sana!!
Keep supporting good music
#ABDUL 🔈🔈🔈🔈🔈
My fellow Democrats, I have decided not to accept the nomination and to focus all my energies on my duties as President for the remainder of my term. My very first decision as the party nominee in 2020 was to pick Kamala Harris as my Vice President. And it’s been the best decision I’ve made. Today I want to offer my full support and endorsement for Kamala to be the nominee of our party this year. Democrats — it’s time to come together and beat Trump. Let’s do this.
Jeshi la Polisi Mwanza limesema ajali ya Basi iliyotokea mapema leo Wilayani Magu Mkoani Mwanza wakati basi la BATCO T 608 DMP likivuka Mto Simiyu katika Kijiji cha Busalaga imesabisha kifo cha Abiria mmoja.
Kamanda wa Polisi Mwanza SACP Willbroad Mutafungwa ambaye alifika kwenye eneo la ajali amesema wanamsaka Dereva wa Basi hilo ambaye alifanya kitu cha ovyo kwasababu hakushughulika kuokoa Abiria wake na badala yake yeye na Kondakta wake wakakimbia.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali ya basi hilo ambalo lilikua na Abiria wapatao 40. #MillardAyoUPDATES
“Kipindi hiki cha usajili nimepunguza sana kumuongelea Rais wetu wa Yanga, watu wanatuma sana vitu inabidi tumlinde sana Rais wetu lazima tumfiche, Aziz Ki hawezi kuondoka Yanga ukitaja neno Azizi Stephan Ki mbele weka Yanga akiondoka nani atawafunga Azam Fc na Makolo?”—Ally Kamwe✍️
KitengeTv imefanya mahojiano na Afisa Habari wa Yanga Sc Ally Kamwe kuelekea Dirisha la usajili linalo karibia kufunguliwa hivi karibuni.
#kitengeSports
DAR: Mdau wa https://t.co/dDd21Ugmlv anasema Wanawake wanapitia Unyanyasaji mkubwa wa Kijinsia wakati wakiwa katika Vyombo vya Usafiri vilivyojaza abiria kama Daladala na Treni ambapo baadhi ya Wanaume wasio wastaarabu hutumia changamoto hiyo 'kuwabambia'
Anasema kero hii ambayo huwa kubwa hasa wakati wa asubuhi na jioni ambapo kuna idadi kubwa ya Wasafiri ni Unyanyasaji kama Unyanyasaji mwingine, hivyo kutoa wito kwa Jamii kukemea vitendo hivi kwa sababu wakati mwingine watu hushuhudia na kukaa kimya
Soma https://t.co/bO1UpvIMV8
#JamiiForums #GBV #EndViolenceAgainstWomen #JFWomen #Accountability
Rashidi Abdallah Mohamed Makwiro (Chid Benz) ana hoja asikilizwe au mnampuuza?
@CloudsMediaLive@babbiekabae kuna ujumbe wenu kutoka kwa Chid Beenz, King Kong, Chuma.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji Mshibe Ali Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Aidha, amemteua Dkt. Emmanuel Jonathan Mpeta kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Kumbe Chuma ilikuwa inatoka Simiyu kwenda Mwanza, mtu mmoja amefariki na mtoto mmoja amepotea na Abiria 25 wamejeruhiwa, hii ni TATA ya kampuni ya BATCO
Poleni sana aisee.
Soure: ITV Habari
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Bodi mbalimbali ambapo miongini mwa aliowateua ni Balozi Adadi Mohamed Rajab kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ulinzi wa Tarifa binafsi na
Fatma Mohamed Ali kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Rais amemteua pia Jaji Mshibe Ali Bakari kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) huku Dkt. Emmanuel Jonathan Mpeta akiteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Theobald Maingu Sabi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Tanzania.
#MillardAyoUPDATES
(𝐈𝐦𝐞𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐰𝐚 𝐍𝐚 𝐒𝐡𝐚𝐛𝐚𝐧 𝐍𝐣𝐢𝐚)
MVUA zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali wilayani kahama mkoani Shinyanga, zimesababisha ng'ombe wawili kufa na watu wawili kunusurika kifo wakati wakijaribu kuvuka barabara na kusombwa na maji katika mtaa wa Mbulu kata ya Mhongolo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Hamza Abdallah ameyabainisha haya leo wakati Mkuu wa Wilaya ya kahama, Mboni Mhita alipofanya ziara ya kukagua athari zilizojitokeza baada ya mvua kunyesha usiku wa kuamkia leo. /https://t.co/73IkB0Ccvm
Marekani imetoa msaada wa dola 100,000 (Tsh. milioni 250.5) katika juhudi za kukabiliana na maafa yaliosababishwa na mafuriko pamoja na maporomoko ya ardhi yaliyotokea Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya zaidi ya Watanzania 70, kuharibu mashamba, na maelfu ya Watu kuyahama makazi yao.
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema msaada huo unaotolewa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), kupitia Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, utasaidia Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na maafa yaliyotokea Manyara ambapo imesema USAID na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) vitaendelea kufuatilia hali hiyo na kutoa usaidizi wa ziada unapohitajika.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle amesema “Tunaomboleza pamoja na Watanzania kote nchini kutokana na mafaa haya yaliyosababisha upotevu wa maisha pamoja na makazi, Wafanyakazi wote kutoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania tunawaombea wale wote walioathiriwa na mafaa haya”
“Marekani inasimama na Rafiki na Mshirika wetu Tanzania wakati huu, Serikali ya Marekani inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa uongozi wao madhubuti na hatua za haraka za kupunguza athari za mafaa na kusaidia Wananchi katika Mkoa wa Manyara.
#MillardAyoUPDATES
#SEYCHELLES: Rais Wavel Ramkalawan ametangaza hali ya tahadhari akiwaamuru Raia wote kubaki Nyumbani, baada ya Mlipuko katika Duka la Vilipuzi na Mafuriko ya Mvua kubwa iliyosababisha Vifo vya Watu 3
Shule zote zimefungwa na Wafanyakazi wa idara muhimu tu na Watu wanaosafiri ndio wanaruhusiwa kutembea
Soma https://t.co/SVe52k6LKw
#JamiiForums #Governance #ClimateChangeCrisis