Tunajipa msongo wa mawazo sana kwa ajili ya maisha ambayo yanaweza kuisha wakati wowoteโฆmuda na saa yoyote unaweza kuondoka .
Hakikisha unaishi mwanetu. Enjoy ๐ซก๐ซต
Pesa Ina tabia ya kwenda kwa watu makatili na wenye Roho mbaya !!! Usiseme mtu kabadilika baada ya kupata hela Hapana ni kaamua kurudi katika tabia yake asili !!! Vitanda kama Ivi vya v.i.p Vipo 5/6 _ 450,000 tu kw matumizi ya room , lodge ,hotel n.k
Ukiwa mfanya biashara Kuna muda unaweza ukajificha mahali ukapiga tu mayowe bila sababu . Huu ugumu wa biashara ni kwangu tuu au ?? Leo ni siku ya 5 ndio nimeshika Laki tatu kwa pamoja na Nalipa watu hapa naondoka kama nilivyokuja asubuhi ๐ญunatoka kutafta hela unarud na madeni
Pesa Ina tabia ya kwenda kwa watu makatili na wenye Roho mbaya !! Hakuna mtu anaebadilika baada ya kupata pesaisipokua !! Mtu hurudi katika tabia yake halisi baada ya kupata pesa !!!
Hivi Huyo anaejiamuliaga tu kujitangazia maandamano kila akiamua ni Nanii ?? Yani anatufanya tukae nyumbani kila akitaka !!! Na tusifanye kazi akipenda ,anatununulisha vyakula kwa lazima kila akiamua, anatesa jesh kusimama barabarani kilasiku na atakua anafany hivi mpaka linii ?
Hii ni 2022 tukafanikiwa kupata mtoto wetu wa kwanza ambae Alikuja kipindi ambacho Kilikua kigumu sana kwani wakati anazaliwa pale sinza palestina Asubuhi yake nilitoka kumpelekea uji mama yangu mzazi aliekua Amelazwa muhimbili ICU takribani mwezi mzima !!!
Hii ni 2021 Nilipomaliza third year UDSM , hi mama Iliamua kunikubali na tukaanza nayo Maisha kipindi nakaa single room Golani ikiwa na kitanda na Godoro tuu ๐คฃwakati huo pis kibao zilinikataa na kunambia nitafte hela ๐คฃ๐๐
Nakushauri kabla nawewe mwenyewe Hujaitwa baba usije ukamhukumu baba yako kwa namna yoyote ile hata kama utaambiwa au kuona mabaya yake kwa kiasi chochote kile !! Tulia uitwe baba kwanza ndio uhukumu ubaya wa baba yako mwanetu ๐ซต
KATIKA BIASHARA
1.Kuna mwingine anaweza kutafuta pesa ila hawezi kusave.
2.Kuna mwingine anaweza kutafuta na kusave pia.
3.Kuna huyu mwingine akipata pesa tu matatizo yanaanza kuwa mengi.
4.Kuna huyu hawezi kutenganisha faida na mtaji na matumizi yake binafsi; yeye nikutumia tu
Umewahi kufanya maradi au biashara Fulani halafu ikakutafuna na ukasema hutakaa urudie ? Kwa sababu Ukipata hasara na maumivu katika mradi au biashara hiyo ?? Tuambie ilikuaje watu wajifunze na kupata somo ๐๐
Kwa wanangu wa boda boda , kama familia yenu haina uwezo wa kuchanga milion mbili kwa haraka ufanyiwe operation Muhimbili basi hakikisha unavaa helmet muda wote, endesha taratibu na kwa tahadhari na pia zingatia service Muhimu za Chombo chako. Mungu awalinde wanetu !!