Kijana mwenzangu ni kweli maisha ni magumu sana, ajira hakuna, magonjwa yamekuandama na bado madeni, ndoa/mahusiano yanakusumbua lakini hutakiwi kuchukua maamuzi magumu ya kukatisha uhai wako. Lia uwezavyo kutoa sumu, omba ushauri kwa waliokuzunguka na usiache kuomba Mungu.
USIINGIE KWENYE MAHUSIANO NA WAFUATAO
1. Mteja wako.
Mapenzi hisia lakini si kila mahali pakuweka hisia zako utaharibu, mteja wa duka lako (genge) au biashara yako usimpe nafasi akawa mpenzi, badala ya kuwa msaada akakufilisi, anachukua vitu bure, ndugu zake watataka bure, usipojiangalia unapoteza uchumi wako.
2. Mtu aliyekuomba ushauri.
Mara nyingi tunakutana na watu walioumizwa kwenye mahusiano hasa sisi counselors, jiepusha sana kuingia kwenye mahusiano na aliyekuomba ushauri kuhusu mahusiano yake.
3. Mpenzi aliyeachwa na rafiki yako.
Kama mmeshibana sana na rafiki yako basi wakiachana usiwe mwepesi kujiachia ukaingia kwenye uhusiano ya ex wake, itahitaji nguvu kubwa sana kumuaminisha hukuwa sababu ya wao kuachana.
4. Mpenzi wa ndugu yako.
Huwa inatokea ndugu yako kapata mpenzi lakini akaja kukuelewa sana wewe kuliko ndugu yako, usije ukajiroga ukampa nafasi, ni hatari mno, tena ondoa ukaribu (shemeji) kaa mbali naye na ogopa sana.
5. Referee katika issue fulani
Usiwe na mahusiano na mtu aliyekufanyia connection fulani, aidha kwenye kupata kazi, kuingia kwenye mashindano fulani, kupanda cheo nk, utaishia kuumizwa kwasababu kwake penzi lako ni kama mshahara tu
6. Mfanyakazi wako
Kwa maendeleo kwenye ofisi yako, ogopa kuingia kwenye mahusiano na Mfanyakazi, hatakuheshimu tena, kazi atafanya anavyotaka, utapoteza kauli kwake anapofanya tofauti, itakulazimu kumpandisha cheo au kubadili mfanyakazi kabisa.
7. Mtu mwenye kidonda.
Usiingie na aliye na maumivu ya kuachwa na mpenzi wake, unakuwa faraja yake na si upendo, utajitoa ila yote ni 0%, siku akipona hataendelea na wewe.
Ukiona upo naye na haachi kumtaja ex wake jua bado anaumia, wewe haupendwi ila umemhurumia tu.
8. Jirani wa chumba cha kupanga ❤️
9. Mfanyakazi mwenzako wa ofisi moja ❤️
10. Mke au Mume wa Mtu 💔
Repost || Share || comment 📌
Baba ni shujaa namba moja wa mtoto.Mtoto anajifunza zaidi toka kwa baba yake kuliko anavyojifunza toka kwa mtu mwingine yeyote.Daima chagua kuwa mfano bora kwa mtoto.Leo siku ya baba duniani nenda kwa baba au mpigie simu umshukuru kwa yote.Waliotangulia,Mungu awaweke mahala pema.
SALA YA JIONI.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina.
Tunakushukuru ee Mungu kwa mema yote uliyotujalia sikuu hii ya leo.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni, Amina.
SALAMU MARIA.
Salam Maria umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi, Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
UNGAMO LA DHAMBI.
Na tuwaze katika moyo makoda yote ya leo tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo (……ukimya…)
Namuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu: nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria Mwenyeheri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
+Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu na atufukishe kwenye uzima wa milele, Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu, nimetubu sana niliyokosa kwako. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi, Amina.
Ee Mungu mwenye huruma, uwashushie baraka zako, Maaskofu wetu, na mapadre, na mashemasi, na ndugu, na jamaa, na marafiki, na maadui zetu. Uwaokoe wale wasiokujua bado, uwafariji wagonjwa, waelekee wanaozimia, waweze kuona mwanga wa milel, Amina.
Ee Maria uliyeumbwa pasipo dhambi ya asili, utuombee.
Mtakatifu Yosefu mlinzi wa Kanisa Takatifu Katoliki, Utuombee.
MALKIA WA MBINGU
•Malkia wa Mbingu furahi, Aleluya
~Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya
•Amefufuka alivyosema, Aleluya
~Utuombee kwa Mungu, Aleluya
•Furahi, shangilia Ee Bikira Maria, Aleluya
~Kwani hakika Bwana amefufuka, Aleluya.
Tuombe:
Ee Mungu uliyependa kuifurahisha dunia, kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, fanyiza twakuomba kwaajili ya Bikira Maria Mamaye, tupate nasi furaha za uzima wa Milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.
Bikira Maria Malkia wa amani ~ Utuombee!
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina🙏
Hakuna mtu yoyote mwenye hati miliki ya Huruma ya Mungu. Ipo wazi kwa watu wote wanaomtafuta Mungu kwa moyo wa toba na wongofu wa ndani. Mwisho wa siku mwana mpotevu anakuwa yule kaka mkubwa aliyejihesabia haki, anayekataa upatanisho wa Baba na ndugu yake.Tusiwazue wengine wokovu
SALA YA ASUBUHI
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.
Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni.
Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia; na kwa Yesu Kristo Mwanae pekee, Bwana wetu, aliyetungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu; siku ya tatu akafufuka kutoka wafu, akapaa mbinguni; ameketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu Katoliki, ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili, na uzima wa milele. Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama; upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya Majivu; usile nyama siku ya Ijumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Pasaka.
5. Saidia Kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.
Ee Maria Bikira Mtakatifu, Mama wa Mungu na Mama yangu, nawe Mtakatifu Yosefu, Nawe Malaika Mlinzi wangi, Nanyi watakatifu somo wangu, nanyi Watakatifu wote, Niombeeni nipate kuacha dhambi, nilindeni siku ya leo na siku zote, na saa ya kufa kwangu, Amina.
MALKIA WA MBINGU
•Malkia wa Mbingu furahi, Aleluya
~Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya
•Amefufuka alivyosema, Aleluya
~Utuombee kwa Mungu, Aleluya
•Furahi, shangilia Ee Bikira Maria, Aleluya
~Kwani hakika Bwana amefufuka, Aleluya.
Tuombe:
Ee Kungu uliyependa kuifurahisha dunia, kwa kufuguka kwake Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, fanyiza twakuimba kwaajili ya Bikira Maria Mamaye, tupate nasi furaha za uzima wa Milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utuombee
Moyo safi wa Bikira Maria, Utuombee
Mtakatifu Yosefu, Utuombee.
Roho za waamini marehemu wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani.
+Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
Dachi_Company ni mafundi wa finishing za nyumba kwa ubora wa hali ya juu.
•Blandaring
•Plaster
•Gypsum board
•Wering na taa
•Skimming na upakaji wa rangi.✅
👉Follw acount yetu @Dachi_company
Ujiomee kazi nyingi za finishing
0783 688 197 karibu tujenge pamoja. 💥💥
"Ukitaka kuishi vizuri hapa duniani, wewe onyesha kuwatambua watu, jali hisia zao, heshimu imani zao, hifadhi aibu zao, linda faragha zao na epuka kukanyaga rizki zao. Kisha ongeza matumizi ya maneno samahani na shukrani katika kauli zako. Ni mambo madogo yenye matokeo makubwa!"
Serikali imeanza awamu ya pili ya ujenzi wa makazi ya watumishi wa nyumba 3,500 eneo la Nzuguni ‘B’ jijiini Dodoma.
Changamoto ya makazi kwa watumishi inafanyiwa kazi.
#MamaYukoKazini
TUTORIAL ASSISTANT MATHEMATICS @UdsmOfficial hakuna hata mmoja aliepita wote wamelata below 50 ndo tuseme vijana wa siku hizi ni viazi au? How come mtu anakosa 50 tena mathematics?
Mwenyezi Mungu wewe ni mwingi wa Rehma.
Asante kwa Baraka zako kwetu waja wako.
Tunakukwaza na mengi ila huchoki kutubariki,huchoki kuturuzuku,huchoki kutukinga na hasadi,huchoki kutuepusha kwa maradhi....huchoki kutuepusha na misala ya kila aina.
Alhamdulillah 🙏
Utofauti wa mpangilio na mandhari ya makazi toka angani, kwa maeneo yanayopakana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni sehemu ya eneo la Msasani na kulia ni sehemu ya eneo la Oyster Bay. Maeneo haya mawili hutenganishwa na barabara ya Ali Bin Said.
📸Google Earth/Maxar Technologies
Hivi ndivyo Waombolezaji, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Mtangazaji wa Wasafi FM, Khadija Shaibu (Didah) walivyofika Msikiti wa Maamur, Upanga Jijini Dar es salaam kwa ajili ya Dua ya kumuombea Didah kabla ya kwenda kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele katika makaburi ya Kisutu.
#MillardAyoUPDATES
Haya ndiyo maeneo ya nje ya mji ya mkoa wa Dar es salaam.
1)kiluvya(Mbezi mwisho).
2)Bunju &Mabwepande
3)chanika
4)mbagala
5)pembamnazi(Tundwi &kimbiji&buyuni)
6)Mbweni
7)mwasonga
Maeneo haya ni umbali wa chini 50km kutoka mjini(posta).
Je ni kweli huku ni mbali..? Kuna mtu hana kiwanja Huku kwasababu eti ni mbali😁. Wengi mtajuta sana mbeleni huko kwakuto miliki viwanja kwenye haya maeneo. @lapexproperties
Kitunda, jimbo la Ukonga, manispa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam, na mbunge wa jimbo hili la Ukonga ni Jerry Silaa (@JerrySilaa) ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika serikali hii.
Kutoka Banana hadi Kitunda ni umbali usiozidi kilometa 3 tu, lakini unatumia dakika 30 hadi 40 kwa kutumia gari. Barabara jimbo la ukonga kata 4 za Kitunda, Mzinga, Kivule na Msongola ni majanga.
Barabara ya kutoka Kitunda hadi Mwanagati kuunganisha kwenda kwa Mparange (wilaya ya Temeke) haijawahi kuwa na hata tone la lami tangu nchi ipate uhuru. Hapa ni Dar es Salaam.
Wananchi wanatumia gharama kubwa kufika mjini. Mtu mmoja anatumia karibu shilingi elfu tatu akiwa anatumia zile gari ndogo za watu binafsi wanaoamua kutusaidia asubuhi wakiwa wanaenda mjini.
Wanatumia magati hayo kwa sababu daladala hazipo kwa ubovu wa barabara. Wamiliki wa Daladala wameamua pamoja kutokupeleka gari zao huko kutokana na ubovu mkubwa wa barabara za huko.
Brigedia Mtikila, MMM.