Tuzo hizi ni matokeo ya utekelezaji wa mradi wa Safe Schools Africa, unahusisha utoaji ushauri wa kitaalamu katika miradi ya barabara barani Afrika, inayofadhiliwa na serikali na benki za maendeleo ili kuboresha usalama katika barabarani hizo.
Mnamo tarehe 10 Disemba 2024, shirika la Amend lilipokea tuzo mbili za Prince Michael International Road Safety (PMIRSA) na Premier Award 2024 kutoka kwa Mwana Mfalme Michael wa Kent, Uingereza.
#FIAFOUNDATION#FIAF#AFD#WorldBank#World#EIB#ITF
Sehemu ya mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Uswiss nchini Tanzania @SwissDevCoop na kuratibiwa na @Amend ulihusisha machapisho yenye jumbe za usalama barabarani pamoja na Kanuni na maadili kwa vijana wa wapo barabarani kupitia kampeni ya #UjanjaniKuaSalama
Uzinduzi rasmi wa mindombinu Salama barabarani kwa shule za Azimio na Makorora, unao fadhiliwa na Ubalozi wa Uswiss Tanzania na kuratibiwa na @amend_tz ndani ya mkoa wa Tanga.. Mgeni Rasmi Ndugu Dalmia Mikaya alishiriki kumuakilisha mkuu wa Wilaya ya Tanga. @Amend@SwissDevCoop
Maafisa usafirishaji wakipatiwa vyeti na viakisi mwanga baada ya kupatiwa mafunzo ya Msasa ya usalama barabarani na utoaji wa Huduma ya kwanza. Zaidi ya vijana 700 hadi sasa wameshiriki mafunzo ndani ya mkoa Tanga & Dodoma katika wilaya na kata mbali mbali. @SwissDevCoop@Amend
Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa Be Road Safe Africa, unaofadhiliwa na Puma Energy katika nchi 4 Barani Africa unao lenga kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi.
@Amend#BeRoadSafeAfrica#Tanzania#Zimbabwe#Botswana#Zambia
Mategemeo ya mradi huu ni kuzifikianchi nyingi zaidi barani Afrika ili kuhakikisha wanafunzi wengi wanakuwa salama na kuwaepuka na ajali za barabarani".
Wiki hii, timu ya Amend inayoratibu mradi wa Safe Schools Africa imekutana jijini Arusha kwa lengo la kupanga mikakati itakayoboresha zaidi usalama wa wanafunzi watumiapo barabara. Kwasasa, mradi huu unahusisha nchi za Tanzania, Ghana, Msumbiji na Zambia.
Muendelezo wa mafunzo ya usalama barabarani yanayo fadhiliwa na ubalozi wa Uswiss @SwissDevCoop kwa vijana wasiopungua 500 waendeshao bodaboda ndani ya mkoa wa Tanga yameanza rasmi pamoja na programu mbalimbali zitakazo jumuisha na kuifikia jamii kwa ujumla @tanpol@TaruraTz
Madereva 253 wapokea mafunzo ya usalama barabarani jijini Dodoma kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uswisi. Kupitia mafunzo haya, Ubalozi wa Uswisi kwa kushirikiana na Amend, wanalenga kuboresha usalama wa madereva, abiria na watembea kwa miguu nk. @SwissDevCoop@tanpol#SwissEmbassyTZ
Wazazi, wazee, watendaji kata, maafisa maendeleo ya jamii, wanafunzi na @tanpol wakishiriki majadiliano yenye lengo la kutengeza kanuni za maadili kwa waendesha pikipiki kibiashara (Bodaboda) ndani ya @TangaCC kwa ufadhili wa @SwissDevCoop na kuratibiwa @Amend#SwissEmbassyTZ
Shirika la @Amend likishirikiana na @tanpol limeanza kutoa mafunzo ya msasa ya usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda 250 Jijini Dodoma. Mafunzo haya yanaambatana na elimu muhimu ya huduma ya kwanza #RoadSafety#RoadsafetyTz#savelives