Msaani wa Nigeria 🇳🇬, Akiendelea na tour yake nchini Marekani, Davido alishangaza wengi baada ya kusimamisha show kwa dakika moja huku akiwaomba mashabiki wake walio jitokeza kuiombea Tanzania kutokana na machafuko yaliyojitokeza siku chache nyuma. Show hiyo iliyoenda Kwa jina la Atlanta Concert ilihudhuriwa na mashabiki wengi, na bendera ya Tanzania ilipeperushwa muda huo.
#ThankYou @davido
Dada wa Taifa @mangekimambi ametupa assignment
Kasema tuingie World trade database (https://t.co/ZS2vtSp3Pt) halafu tuingize jina la kampuni ya Magmop Company Limited ili tuone magari ambayo hii kampuni imeingiza nchini ndani ya mwaka mmoja.
NB. Hii kampuni ni ya Angela Kiziga
Tukiamka asubuhi tuanze na hii
Video mmesema ni FEKI ila chaajabu watumishi wanasumbuliwa sana leo.
Madaktari na manesi wanapokonywa simu zao na kukaguliwa kama watoto wadogo. Acheni kuendesha nchi kama mnaendesha wanafunzi wa bweni.
Sasa ni hivi ingieni kwenye page ya Hilda Newtown. Lazma utype jina la account yake zima kwenye search ndo account inakuja.
Angalieni hiyo number ya simu ya Angela Kizigha. Sasa fanya kama unataka kutuma pesa Kwenye hiyo number, utaona imesajiliwa kwa jina la kampuni inaitwa Magmop Company Limited. Sasa ingia kwenye website za world trade databse alafu ingiza jina la hii kampuni, inakuonyesha magari yaliyoingizwa nchini na hii kampuni.
Ndani ya mwaka mmoja hii kampuni imeingiza magari yenye thamani ya $ milioni 19. Mpaka Bugatti Cheron wameingiza, na maRolls Royce na na Bentley na ma ferrari.
Ndugu zangu ndio maana serikali hiii iko tayari kuuwa wananchi kuliko kutoa haki na kuachia madaraka.
Tarehe 9 December nchi nzima lazima tuingie barabarani tuwaondoe hawa watu. Maandamano no ya amani, kila mtu atoke na bango lake.
Nilifanikiwa kurejesha mawasialiano yangu kupitia line yangu ya @VodacomTanzania .
Bado naendelea kusisitiza nijulishwe, sababu hasa ya mawasialiano yangu kuzuiliwa kwa siku kadhaa.
Huyu naitwa Renatus Charles Hangaya ambaye ni mmoja wa walinzi wa Mhe. Lissu alitekwa usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 09/11/2025.
Watu waliokuwa na magari na silaha za moto ambao walijitambulisha kuwa ni Askari Polisi, walifika nyumbani kwake usiku na kuondoka naye.
Familia yake imezunguka vituo vyote vya Polisi lakin hawajafanikiwa kumpata.
#FreeHangaya
REPOST 200
#TUTAKUWEPO🫵😎
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tundu Lissu amewasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuwa ajumuishwe kama mdaiwa katika kesi ya Mgawanyo wa Mali inayokikabili chama chake.
Jambo TV imezungumza na Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi akatueleza kuwa maombi hayo yaliwasilishaa Novemba 10, 2025 na tayari taratibu zote za kimahakama zimefanyika ikiwemo kuwasilisha maombi hayo katika mfumo wa mahakama pamoja na kulipia. Hivyo kwa sasa kilichobaki ni Mahakama kuyapangia tarehe maombi hayo ili yaweze kusikilizwa.
"maombi yamewasilishwa ni kweli yameshasawasilishwa na yamelipiwa ada kinachosubiriwa ni ofisi ya Jaji Mwanga kutokana na kalenda ya mahakama atapanga utaratibu kutoa wito na maombi yatasikilizwa" amesema Wakili Garubindi
Katika shauri hilo la msingi la madai lenye namba 8323/2025 wadaiwa ni Bodi ya Wadhamini wa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, hivyo maombi ya Lissu yakikubaliwa atakuwa mdaiwa wa tatu.
Shauri hilo limefunguliwa na Said Issa Mohammed na wenzake wakidai kuwa kumekuwa na upendeleo kwenye ugawaji wa rasilimali za chama huku upande wa bara ukipendelewa zaidi kuliko Zanzibar.
Tangu nitoke mahabusu ya polisi leo ni siku ya 6 line yangu @VodacomTanzania haifanyi kazi.. Hakuna simu inayoingia wala mimi siwezi kupiga simu ikatoka, hata namba 100 ya huduma kwa wateja haitoki:
Nimekuja Voda shop kujua na wao wanasema hawaoni shida au nisubiri masaa 24.
Kuna uwezekano mkubwa yakawa yale ya ndugu yetu Erick.
Voda ni muhimu mkaniambia kuna tatizo gani.
Nimeweka kwenye public ili kila mtu ajue.
Kadri ninavyoendelea kumsikiliza Mhe. @TunduALissu hapa mahakamani nazidi kujiridhisha sio tu anajitetea kama mtuhumiwa bali pia anafundisha sheria kupitia ubobezi wake kitaaluma na kiuzoefu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 150
Anaendelea Mhe. Lissu
Hivyo naomba sheria hii kama Jaji Mtembwa aliitumia, naiomba Mahakama hii isiendelee kukosea, isiendelee kuitumia.
Waheshimiwa Majaji mkiangalia sheria namba 7 ya 2018 utaona imeandikwa kwenye header note kuwa sheria hii imetolewa kwenye gazeti maalum la Serikali la tarehe 15 Septemba 2018, waheshimiwa majaji huo ni uongo.
Uthibitisho kuwa ilichapishwa kwenye gazeti la serikali ni kulitoa gazeti lenyewe, proof sio what the law says, bali ni physical existence or electronic existence.
Nawaomba waheshimiwa majaji msiitumie hii sheria, msipoitumia maana yake mashahidi waje watoe Ushahidi hadharani, hii ya kufichaficha mashahidi gizani haitakuwepo kabisa na haitakiwi kabisa kuwepo.
Anasimama Wakili wa Serikali Nassoro Katuga yupo kama amechanganyikiwa au ametoka kubeba gunia la mchanga ni mdogo kama Pilton.
Amesimama akiwa amenywea sana na kusema,
Kwa hoja nyingi zilizoletwa tunaomba muda wa kujiandaa kujibu hoja nyingi sana ambazo mshtakiwa amezisema.
Tunaomba tarehe ambayo tutapangiwa kwaajili ya kuja kujibu.
Lissu hajapinga ila ameomba tarehe ya karibu zaidi wapewe.
Kesi imeahirishwa kwa muda usiojulikana hadi pale ambapo Mahakama itatoa Notisi ya siku ya kusikilizwa kwasababu notisi ya awali ilionyesha mwisho wa kusikiliza kesi hii ni leo Novemba 12, 2025.
Naomba Repost yako.
Leo tarehe 12/11/2025 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam.
Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo itaendelea hapa.
Leo kuna kila dalili kesi itaendelea. Kwasababu Mhe. Lissu ameshafikishwa asubuhi ya leo na maandalizi yanavyoonekana hapa Ukumbi namba 1 wa Mahakama kuu, shauri litaendelea.
Maandalizi yapo kama ambavyo huwa yanafanyika siku kesi inasikilizwa.
Wafuatiliaji mbalimbali wanaendelea kufika mmoja mmoja na pia amefika Naibu Katibu Mkuu wa Chama, Amani Golugwa, yupo pia Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" na Godbless Lema pia wamefika hapa Mahakamani.
Muda wowote kuanzia sasa shauri linaweza kuanza kusikilizwa.
VIDEO:
Mbunge Mteule wa Viti Maalum kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo, amesema hajafurahishwa na uteuzi wake wa nafasi hiyo, akidai kuwa alinyang’anywa ushindi wa Ubunge wa Jimbo na kupewa nafasi ya ubunge wa Viti Maalum.
Mligo ametoa kauli hiyo leo, Novemba 10, 2025, katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mara baada ya kujisajili kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13, unaotarajiwa kuanza Novemba 11, 2025.
Mligo amesema hajafurahishwa na namna alivyoteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Mkoa wa Njombe, hasa katika kipindi ambacho Watanzania wanapitia hali ngumu ya Kisiasa na Kijamii.
"Wakati mimi naapishwa, kuna watu Mtaani wamezika ndugu zao, watu wamekufa. Taifa liko kimya. Mimi sijafurahia kuwa Mbunge katika Bunge ambalo taifa linavuja damu,” amesema Bi. Mligo.
Aidha, ameeleza kuwa ataingia Bungeni kama Mbunge wa Kitaifa mwenye dhamira ya kuwasemea Wananchi wasio na sauti, akisisitiza kuwa atapigania demokrasia, haki na utawala wa sheria, badala ya kufuata maagizo bila kuhoji.
🚨BREAKING NEWS🚨
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara John Wegesa Heche ameachiwa na Jeshi la Polisi jioni ya leo Jumatatu Novemba 10, 2025.
Kwa mujibu wa wakili Hekima Mwasipu amesema Heche ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi tangu Oktoba 22, 2025 alipokamatwa katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.
Heche ameachiwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara Amani Golugwa, Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani Boniface Jacob na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema.
Viongozi wote hao wameachiwa katika kituo cha polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam.