Siku nzima ya leo magari mawili ya polisi na polisi wakiwa wameziba nyuso zao na silaha kubwa kubwa, wamenifuatilia tangu nikiwa Urambo kwa kupokezana mpaka nafika Kigoma.. njiani nimesimama mara mbili kuwauliza shida yao ni nini kwangu hawakuwa na majibu ya maana.
Nimefika hapa Kigoma kila ninakopita na hapa Hotelin kwangu wamejaa maafisa wakiwa na nguo za Kiraia..
Mimi ni Mwanasiasa wa upinzani ninaetimiza wajibu wangu wa kikatiba… Chama chetu ni chama cha siasa ambacho kimesajiliwa na chenye haki zote katika Nchi hii.
Nimepokea taarifa nyingi kwa watu wema wakitaka niwe makini, wengine wanasema mimi na familia yangu tumetolewa maelekezo mabaya.
Nitatimiza wajibu wangu bila uoga wala hofu, hakuna mtu anaweza kuniondoa kwenye haki na wajibu wa kutetea Nchi yangu na watu wetu.
Ninawashauri watawala dhalimu kuacha kucheza na utulivu huu uliopo . Hofu haijawahi kuzaa amani, hofu huzaa hofu zaidi.
Hakuna siku nitakimbia Nchi yangu.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Askofu Benson Kalikawe Lwekandila Bagonza, amechapisha andiko lenye mtazamo mkali kuhusu mchakato wa maamuzi ya serikali na mjadala unaoendelea kuhusu uhalali wa mikutano ya vyama vya siasa nchini.
Katika andiko hilo lililosambaa mtandaoni, Askofu Bagonza amesisitiza kuwa baadhi ya viongozi hawapaswi kubebeshwa lawama binafsi katika maamuzi yanayohusisha taasisi mbalimbali za dola, akitolea mfano mjadala unaomhusisha Mbunge na Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Patrobas Katambi.
“Katambi asilaumiwe peke yake katika jambo hili; kuna mnyororo wa maamuzi unaohusisha taasisi zaidi ya moja.” amesema
Katika ujumbe wake huo, Askofu Bagonza ameibua maswali kuhusu namna maamuzi ya kisiasa na kiutawala yanavyopitishwa na kutekelezwa, hasa pale yanapogusa haki za kikatiba za wananchi.
"Tatizo siyo Katambi. Tuna mgongano sugu kati ya Majasusi Wanasiasa NA Wanasiasa Majasusi. Hawa ni watu wawili tofauti. Nitaeleza siku nyingine. Mnaoogopa kuchanganya Dini na Siasa, ogopeni pia kuchanganya Ujasusi na Siasa. Zuio la mikutano likatolewa bungeni. Tuseme ni bunge limezuia mikutano? IGP kaagizwa kukiuka katiba. Atatii? Akitii, nani mkosaji? Aliyeagiza au aliyetii?"
"Kwa nini Waziri hakusubiri Waziri Mkuu ndiye atoe zuio hilo kwa niaba ya serikali wakati anaahirisha bunge? Kwa nini serikali isitumie TCD au Msajili wa Vyama, wakaitwa wadau na kushawishiwa wakubaliane kuvunja katiba? Je ili zuio/katazo la mikutano au zuio/katazo la kutumia katiba; yaani kwamba imeenda likizo kwa muda?! Hatua hii hufanyika nchi ikiwa vitani au wale jamaa zangu majirani wa Wajaluo wanapoamua kuchanganya cha Arusha na siasa." Amesema Askofu Bagonza.
Askofu huyo pia amegusia suala la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, akitilia shaka utaratibu wa kuwekewa vikwazo bila uwazi wa kikatiba.
“Mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatiba au ni fadhila zinazoweza kutolewa na kuondolewa kwa maamuzi ya kiutawala?”
Katika andiko lake, pia ameibua maswali kadhaa kuhusu nafasi ya Bunge, Wizara, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Waziri Mkuu katika mchakato wa maamuzi yanayohusu mikutano ya kisiasa na utekelezaji wake.
Kihistoria muda wa kitu ukifika hauwezi kubadili tena.
Tangu zamani..
Muda wa biashara ya utumwa kukomeshwa ulipofika haikuwezekana kuzuia tena.
Muda wa uhuru ulipofika wakoloni walilazimika kuachia hizi Nchi, hata walipojaribu kutumia mabavu haikuwezekana..
Moyo wa wananchi umeishakataa CCM, Muda wa ccm umekwisha, bunduki, mabavu, mauji na utekaji haviwezi kubadili hali hiyo.
Kucheza na hisia za wananchi na mioyo ya watu ni kucheza na moto.
Uhalali wa serikali dhalimu hauwezi kuletwa na bunduki.
Tume ya Udanganyifu Mkuu chini ya Jacobs Mwambegele ndiyo iliyompigia kura Samia Suluhu Hassan na kumkabidhi uongozi wa nchi hii.
Wananchi wenyewe ndio hawa wapo kwetu.
Ushuru wa Mabango ya Matangazo kwa sheria yetu yanalipiwa, kwa kila mita square ni zaidi ya 7,000…
Kuna Mabango ya kampeini za Samia kwenye kila Halmashauri ya Nchi hii.
Tunataka kujua fedha ambazo zimelipwa na ccm kuendelea kuweka Mabango ya uchaguzi katika maeneo ya umma.
Kumshambulia Msigwa kwa kuikimbia CCM kumetatuaje tatizo la Oktoba 29, 2025?
Je, kumjadili Msigwa mchana na usiku kumerudisha imani ya wafadhili waliogoma kutoa fedha?
Je, kumlaumu Msigwa kumeshusha bei ya mafuta na gharama za maisha?
Je, kumshambulia Msigwa kumezuia au kupunguza ufisadi unaolalamikiwa na wananchi?
Je, kumerudisha ajira, kuimarisha uchumi na kurejesha heshima ya Tanzania kimataifa?
Hakuna taifa linalotatua matatizo makubwa kwa kutafuta adui wa kisiasa wa kumlaumu. Matatizo ya taifa yanahitaji majibu ya sera, uwajibikaji na uongozi, si propaganda.
Badala ya kujadili kwa nini mtu alihama chama, swali muhimu zaidi ni:
Nini kifanyike kurejesha imani ya wawekezaji na wafadhili?
Nini kifanyike kupunguza gharama za maisha?
Nini kifanyike kupambana na ufisadi?
Nini kifanyike kuponya majeraha ya kisiasa na kujenga maridhiano ya kitaifa?
Historia haikumbuki sana waliotumia muda mwingi kuwashambulia watu; historia huwakumbuka waliotatua matatizo ya watu.
Matatizo ya Oktoba 29, 2025 na athari zake kwa taswira ya Tanzania na uhusiano na washirika wa maendeleo yameendelea kujadiliwa kimataifa.
Haya magari na hawa watu wanaokuja kwenye mikutano yetu kwa njia za kufuatilia kwa njia zisizo za wazi..
Wanapaswa kujua Tunajua na tunawaona.
Sisi tunafanya siasa na tunafanya kazi yetu ya kikatiba, hatuwezi kukubali kutishiwa wala kuogopeshwa.
Acheni uhuni huu.
Many thanks to you @rodneycloete and the @IPC Party for your unwavering support and solidarity with the people of Tanzania during this difficult chapter in our country's political history. We are deeply grateful to the people of Namibia for consistently standing with Tanzanians in their pursuit of justice, democracy, and human dignity. Your party’s statement is a powerful testament to that enduring solidarity and commitment to the values that unite our peoples. #FreeTunduLissu #SamiaMustGo @NamPresidency@SADC_News@ECN_Namibia@HecheJohn
@NNNandiNdaitwah
Jana tarehe 18 Juni 2026 barabara zote za kuelekea Makao Makuu ya UMOJA WA ULAYA (European Union), mjini BRUSSELS, UBELGIJI, 👇zilikuwa ZIMEFUNGWA, halafu watu walionekana wako “BIZE SANA”. Sijui kulikuwa kuna nini kinaendelea😂😂