Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 134 ya Canton (#CantonFair) umefanyika leo katika hoteli ya Westin iliyopo pembeni mwa viwanja vya maonesho hayo vya Guangzhou Canton Fair Complex. #134thCantonFair
Awamu ya kwanza ya maonesho hayo itaanza rasmi kesho tarehe 15 hadi tarehe 19 Oktoba 2023 ambapo Makampuni 600 yataonesha bidhaa za vifaa ujenzi, umeme, bidhaa za kemikali, mitambo na mashine za sekta za kilimo na madini, vifaa vya magari ya umeme nakadhalika. #134thCantonFair