Hizi ni kodi na ushuru wa serikali kwa gari ndogo tu Crowne.
Fikiria kijana ambae ameanza maisha hapa Dar, kutokana na adha ya usafiri anajibana ananunua kagari ka usd 6,000 ambazo ni sawa na 14 m.
Hiyo gari ikifika inatozwa ushuru mwingine wa 14 m, yaani fikiria ushuru unalingana na ununuzi wa gari!!!
Yaani gari Machuma yote, engineering iliyopo pale kwenye gari unanunua bei sawa na ushuru wa mtu ambae amekaa ofisini tu na anakuchaji hela yote hiyo!!!!
Wakati mwingine kodi zinakua bei juu kuliko manunuzi!!!!
Huyu kijana awe mkulima au mfanyakazi, anafanya kazi ngumu sana kupata hiyo fedha, then inachukuliwa hiviโฆ
Alafu baada ya mda CAG anasoma ripoti kwamba uwanja ulitakiwa kujengwa kwa bilioni 187 baadae ukajengwa kwa bilioni 337..
Mara umekaa unaambiwa kuna eti Waziri anatumia gari binafsi ya bilioni 2, unajiuliza mtumishi wa umma ametoa wapi bilioni 2 kununua gari na mshahara wake unafahamika, au anamiliki nyumba tano za thamani ya bilioni tatu, nne au tanoโฆ aniliki mashamba ya mabilioni, amempa mama mkwe wake nyumba ya bilioni tano na gari la kutembelea la milioni 500.
Pesa zote hizi za mlipa kodi anaeumizwa kiasi hiki na mzigo wa kodiโฆ
Hapa nimesema magari tu, Ukienda kwenye kila kitu kinachoingizwa na kutoka Nchini ni mzigo wa kodi na maumivu kwa Mwananchi..
Na mwisho wa siku badala hizi fedha zitumike kwaajili ya maendeleo yetu zinaishia kwenye mifuko ya vibaka.
Hakuna barabara, hakuna maji, hakuna umeme.. Maisha magumu , mishahara duni hasa kwa walimu na manesi.
Hatuwezi kukubali kuwa watumishi wa vibaka wanaopora mali za umma.