#VIDEO Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa alivyokula kiapo cha kuingia kwenye uchaguzi wa Papa mpya, ambao unafanyika leo Mei 7, 2025.
Uchaguzi wa kumpata Papa mpya unafanyika katika Kanisa la Sistine (Sistine Chapel) lililoko ndani ya Jumba la Kipapa (Apostolic Palace) katika mji wa Vatican.
Katika kiapo hicho Kardinali Rugambwa amesema, "Mimi Protase Kardinali Rugambwa naahidi, naapa kwamba nitaheshimu kikamilifu na kwa uaminifu masharti yote yaliyowekwa katika katiba ya kitume Universi Dominici Gregis, na nitadumisha usiri kamili kuhusu yote yanayohusiana na uchaguzi wa Papa mpya. Mungu anisaidie na hivi vitabu vitakatifu vya Injili ninavyovigusa kwa mkono wangu."
#EastAfricaTV