🚨💣 BREAKING: Éderson to Manchester United, here we go!
Deal done with Atalanta for €45m package with add-ons included, agreement now in place.
Medical and formal steps to follow but deal in place.
Éderson will sign a four year deal plus option, as @TheAthleticFC reports.
UDALALI WA KISIASA NA MACHOZI YA MAMBA
Katika medani ya siasa za Tanzania, ni rahisi sana kuwatambua wanasiasa wanaosimama upande wa umma nyakati zote, na MADALALI wanaosubiri upepo uvume ili wajivike koti la ushujaa.
Kauli za hivi karibuni za Zitto Kabwe kuonyesha kuguswa na kusikitishwa na kusota gerezani kwa Tundu A.M. Lissu, pamoja na ukandamizaji wa uchaguzi uliofanywa na CCM, zinaibua hisia nyingi.
Kabla ya kuingia katika uchaguzi uliosababisha maafa, CHADEMA ilisimama ikitaka vyama vya upinzani viungane kudai: Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi na marekebisho ya sheria za uchaguzi.
Hata hivyo, Zitto Kabwe na chama chake walikataa ushirikiano huo. Walichagua kushiriki uchaguzi huo licha ya kuwepo kwa viashiria vingi vya udhalimu. Hawakujali kabisa hisia za watu wengi. Ubinafsi.
Walisaini kanuni za maadili ya uchaguzi, wakatoa dhihaka kwa waliokuwa wakisisitiza msimamo wa “NO REFORMS, NO ELECTION”, na wao wakaamua kusema “TUTAPAMBANA, TUKISHIRIKI”.
Zitto Kabwe alifika hatua ya kusema hao wanaosusia uchaguzi hawajielewi na hawajitambui huku akidai kuwa chama pekee chenye uwezo wa kuitisha maandamano makubwa ni ACT-Wazalendo.
Wakaibuka na kauli mbiu za kitapeli “OKTOBA LINDA KURA”, wakati hawakuwa na mkakati wowote wa kulinda kura zaidi ya kutumika kuhalalisha ushindi wa kishindo wa 98% kwa wapiga kura hewa.
Baada ya mfumo huo huo waliouhalalisha kuonyesha sura yake halisi, leo anasimama kuzungumzia dhuluma za uchaguzi kana kwamba hakuwa sehemu ya waliochangia kuupa uhalali mchakato huo.
Kwa mtazamo wangu, ACT-Wazalendo na Zitto Kabwe walishiriki kuisafisha CCM mbele ya macho ya umma na kuhalalisha ushindi wao. Huu ni usaliti mkubwa kwa harakati za ukombozi wa kisiasa.
Zitto Kabwe ambaye amefanyiwa ‘endorsement’ na mgombea URAIS wa CCM jimboni, na hakuwahi kulitaja jina la mgombea wa CCM, anaibua mashaka makubwa kuhusu dhamira yake wakati huu.
Zaidi ya hayo, tangu Tundu A.M. Lissu akamatwe, kuwekwa rumande, kufunguliwa mashtaka ya uongo ya uhaini na kupelekwa gerezani, Zitto Kabwe hajawahi kuonekana gerezani au mahakamani.
Usiku unakula na watawala, mchana unawatetea wahanga wa mfumo huo. Huwezi kuwa mshirika wa mfumo unaokandamiza haki za wapinzani halafu ukataka kutambulika kama mtetezi wao.
Ndio maana Zitto Kabwe akiongea anaonekana mnafiki, na akinyamaza anaonekana msaliti; Ni matokeo ya kuchagua kuishi katikati ya mstari (playing both sides). Hatakiwi kuaminika.
Kwa nini sasa? Je, ni baada ya kuona mashinikizo mazito kutoka kwa jumuiya za kimataifa, hususani Jumuiya ya Ulaya na Marekani, yakiongezeka dhidi ya ukandamizaji mkubwa wa kisiasa nchini?
Zitto Kabwe ameanza kujionyesha kama mtetezi wa haki mwishoni kabisa. Lakini anapozungumzia matatizo yaliyopo, anaelekeza lawama kwa viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama pekee yake.
Huku akijaribu kuwatenga watawala wa kisiasa ambao kikatiba na kiutendaji wanawajibika moja kwa moja kwa maamuzi makubwa ya nchi. Hili linazua maswali kuhusu dhamira halisi ya kauli zake.
Ni mkakati wa kupunguza makali ya mapambano yanayofanywa na wapigania haki hslisi, kuwatenga watawala wa CCM ambao ndiyo waliotoa amri haramu, na kuharibu uchaguzi hadi mauaji
Hu ni mkakati unaotengenezwa kutusogeza katika meza ya MARIDHIANO kwa kuwatoa kafara wachache katika vyombo vya ulinzi na usalama huku watawala wa kisiasa wakibaki bila kuwajibika.
Katika siasa za mapambano, katika nchi demokrasia bado inapiganishwa kwenye matone ya jasho na damu, hakuna eneo la kijivu (gray area); ama uko upande wa haki au uko upande wa dhalimu.
Watanzania wanaona, wanasikia na wanakumbuka. Ni muhimu kutambua waliosimama katika misingi ya mapambano tangu mwanzo na hawa MADALALI wanaojitokeza baada ya upepo kubadilika.
Waliokuwa mstari wa mbele kubeba gharama za harakati hawapaswi kuruhusu historia yao kutwaliwa na MADALALI wanaotaka kujijengea taswira ya kishujaa bila kubeba gharama za mapambano.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila
@IAMartin_ You can't jump the ship while it's sinking, yet you're amongst its architects, Kabwela atulie hizi lawama hazikwepi kila mtu anakumbuka aliingoza ACT Kushiriki uchaguzi batili.
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Prof. John Ruhangisa amesema hayo wakati akifanya mahojiano maalum ya kipindi cha Katiba Kitaa jijini Arusha.
#KatibaKitaa
@zizujo01 Unaweza kuweka kipaumbele kwenye kuomba misaada iwe material things, pesa angalau zipatikane through izi sherehe za charity...ili tusiache alama za miamala, ndo tujue namna ya kuingiza izo pesa chafu. Mind you FIU nao wapo rada ni kucheza kwa step
Mama asimulia jinsi alivyoshuhudia kijana wake Damour Nyakairo akichukuliwa na watu saba waliofika nyumbani kwao na Landcruiser Nyeupe.
Akizungumza na The Chanzo leo Mei 02, 2026, Lilian Swai ambaye ni mama mzazi wa Damour Nyakairo, ameeleza kuwa kijana wake amechukuliwa asubuhi ya leo na watu waliokataa kujitambulisha, na kumpeleka kusikofahamika.
“Wameondoka naye hatujui kapelekwa wapi. Wametoka huko watu saba wakaja,mimi nashangaa watu wanakimbia mvua au wanakimbia nini? Moja kwa moja wanamfuata Damur na mimi nimekuwa hapa. Wakamshika, wawili wanamshika na mmoja akatoa pingu mfukoni akamfunga. Nikauliza kuna nini [wakasema] tutajua huko huko, nyie nani? Wakasema tutajuana huko huko,” anaeleza Lilian Swai mama wa Damour.
“Kwa hiyo wakambeba watu watatu wakamshika, wakambeba wakamburuza mpaka kwenye gari. Mimi nikawa nataka kuingia na yeye huko, wananivuta wakanitoa nje.”
🎶 ...Vipi kule jikoni si nlisema mchome Nyama,
Mbona haiji, mbona-mbona inachelewa sana,
Hii bar mizinguo kama vipi mi nahama,
Naenda kwa Mfojo yule fundi wa kuchoma Nyama ...🎶
#ChupaNyingine
🎶 ...Vipi kule jikoni si nlisema mchome Nyama,
Mbona haiji, mbona-mbona inachelewa sana,
Hii bar mizinguo kama vipi mi nahama,
Naenda kwa Mfojo yule fundi wa kuchoma Nyama ...🎶
#ChupaNyingine
Ederson tried to get this girl's attention, but Milan Škriniar told him she was deaf, so he immediately switched to sign language instead 🫶🥹
🎥 @ADEM__CAN