"Kanisa ni Takatifu, sio kwa sababu ya matendo yetu, bali kwa sababu kichwa chake ni Kristo mwenyewe ambaye ni Mtakatifu. Kazi yetu sisi ni kuishi kwa kumfuata Yeye, sio kuunda Kanisa kwa mfano wetu" ~ Papa Leo XIV
UNGAMO LA DHAMBI.
Na tuwaze katika moyo makosa yote ya leo tuliyomkosea Mungu, kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo(β¦β¦β¦)
Namuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu, nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenyeheri, Bikira daima, malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
+Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu na atufukishe kwenye uzima wa milele, Amina.