Wizara ya Fedha na Mipango imesema deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.
Aidha, taarifa inaonesha kuwa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 31.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameachiliwa huru baada ya muda wake wa kutumikia kifungo jela kumalizika kwa makosa ya kudharau Mahakama.
Zuma alihukumiwa miezi 15 jela mwaka jana baada ya kupuuza maagizo ya kushiriki kwenye uchunguzi kuhusu ufisadi.
#KitengeUpdates
Mtu mmoja mwenye silaha alivamia benki jijini Beirut na kulazimisha apewe pesa zake ili aweze kwenda kulipia matibabu ya baba yake.
Kutokana na hali ngumu sana ya kiuchumi nchini Lebanon,benki zimeweka vizuizi vikali haswa kwenye utoaji wa fedha za kigeni.
Bunge la Urusi limepiga kura kuunga mkono marekebisho ya sheria ambayo yatawezesha kutozwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka 15 gerezani, kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kuhusu vikosi vya Jeshi la Nchi hiyo.
#MillardAyoUPDATES