Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA):
Walipakodi
👥 Mwaka 1995/96: 75,000
💶 Mwaka 2025/26: Milioni 8.4
Mapato
👥 Mwaka 1995/96: Bilioni 297
💶 Mwaka 2025/26: Trilioni 37.9
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amepasua jipu kwa kuichambua vipande vipande Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027, akidai kuwa nusu ya bajeti hiyo ni "utapeli" na haina uhalisia wa kiuchumi mtaani.
Akizungumza katika mkutano maalum wa chama hicho na wanahabari kuchambua bajeti leo Jumanne, Juni 23, 2026, mkoani Dar es Salaam, Mpina amefichua kuwa matumizi halali na ya lazima ya nchi hayapaswi kuzidi shilingi trilioni 30, na kwamba mabilioni yaliyobaki yamerundikwa ili kugharamia safari za viongozi, malipo ya faini za mikataba mibovu, na kufadhili "machawa" wa kisiasa.
Mpina amebainisha kuwa nchi ina uwezo mkubwa wa kukusanya hadi shilingi trilioni 46, lakini mkwamo mkubwa upo kwenye nidhamu mbovu ya matumizi ambapo Bunge limegeuzwa kuwa sehemu ya kuidhinisha fedha za kwenda kuibiwa.
Kwa mujibu wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuboresha sekta ya afya nchini, idadi ya vituo vya afya imeendelea kuongezeka kutoka vituo 847 mwaka 2021 hadi zaidi ya vituo 1,300 mwaka 2025.
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametangaza rasmi barabara sita za kimkakati ambazo Serikali imezifungua kwa wawekezaji binafsi kupitia Mpango wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), akisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuharakisha maendeleo ya miundombinu nchini.
Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 23, 2026, Ulega amesema tayari Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umetoa tangazo rasmi la kuwakaribisha wabia kushiriki utekelezaji wa miradi hiyo.
“Naomba kuliambia Bunge lako tukufu kwamba mpango wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuifungua nchi na kuona hakuna anayeachwa nyuma unaendelea,” amesema Ulega.
Barabara zilizotajwa katika mpango huo ni Morogoro–Dodoma yenye urefu wa kilomita 246 itakayojengwa kwa njia nne, Chalinze–Segera–Tanga, barabara ya haraka (Expressway) kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Kibaha, Handeni–Kiberashi–Chemba–Kwamtoro–Singida yenye kilomita 384, mchepuko wa eneo la Kitonga mkoani Iringa wenye kilomita 27 pamoja na barabara ya haraka ya kilomita 10 itakayorahisisha safari kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
#MillardAyoUPDATES
@Castojr4@swahilitimes Unaona sasa hujui unaloongea ,wewe nakuona kama mvuta bangi wa vijiweni hujui unaongea nini hujui unabisha nini hujui ulipo huna hoja,hio ndio mihemuko sasa