#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 19
Mahakama Imerejea.
Majaji wameingia.
Wakili wa Serikali amesimama kujitambulisha anaitwa Narindwa Sekimanga.
Shaidi Mkuu wa Gereza nae yuko pale kizimbani yeye muda wote amekaa tu pale kizimbani.
Hajajihangaisha kusimama labda kwa vile ni mrefu na hicho kitambi anachoka kusimama pengine.😂
Jaji Mruma: Shaidi nakukumbusha bado uko chini ya kiapo.
Mhe Lissu: Sasa turudi kwa viongozi wangu wa Chama uliowakatalia wasije kuniona kule Gerezani. Angalia majibu yangu na uangalie kiapo kinzani kuhusiana na kiapo kinzani nilichomjibu Kisabo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ametoa macho. Hafanyi lolote.
Mhe. Lissu: Mawakili wa Serikali mnafanya nini si mumsaidie shahidi wenu azione hizo nyaraka naona ananiangalia tu.
Wakili wa Serikali anaenda.
Mhe. Lissu: Hizo aya kwenye kwenye kiapo changu kinzani zinaonesha namna ulivyowazuia viongozi na wanachama ikiwemo mashahidi na mawakili watatu ambao ni Dickson Matata, Deogratias Mahinyila na Gaston Garubindi. Swali langu waeleze majaji kama umewahi kupinga haya maelezo yangu yaliyopo kwenye kiapo changu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waheshimiwa Majaji nimeshalijibu hilo.
Jaji: Umeelewa swali lake kweli.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Nalo ni jibu pia. Haya kwenye aya ya nne wewe umefanya kampeni ya muda mrefu ya wewe na mlalamikiwa wa pili kamishna mkuu mmehakikisha nashindwa kujitetea wala kuandaa utetezi wangu na matukio nimeyasema kwenye para H na Y. kwamba umewazuia mawakili wangu watatu ambao Ni Mahinyila, Matata na Garubindi kama umewahi kujibu hili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli nimewazuia.
Mhe. Lissu: Je umeleta supplimentary affidavit? Au majibu yoyote kwenye jambo hilo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : anatoa macho. Anashika makaratasi na kuyaacha.
Jaji: Umeelewa swali?
Mhe. Lissu: Ulileta counter affidavit mara ya kwanza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Baadae ukaleta suplimentary affidavit?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Sasa kwenye hizo nyaraka zako mbili kuna mahali kokote ulijibu tuhuma za kuwa umewazuia mawakili wangu na viongozi wa Chama?
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijajibu.
Mhe. Lissu: Tuhuma dhidi yako na maafisa wako kusearch mawakili na nyaraka zao kisheria. Jibu swali kwamba waleta maombi wote watatu wamesema wanasearchiwa, wanakaguliwa na kusomwa hizo nyaraka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Reg. 17(2) ya kanuni za Magereza inasemaje?
Anatafuta hiyo kanuni.
Mhe. Lissu: Ni kweli mgeni anayekuja Gerezani kutembelea mfungwa atasachiwa endapo atakuwa na wasiwasi na huyo mgeni?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Haya isome sasa
Ntamamiro (Bwana Jela) : A prison officer when has any ground suspiciously may direct to search that visitor. Anasoma kingereza kibaya sana.
Mhe. Lissu: Any ground for suspicion may search or cause to search. Kumbe ataamuru asachiwe kama atakuwa na sababu za kumshuku?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Mgeni ataambiwa aondoke akikataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa mujibu wa kanuni hii ni kweli.
Mhe. Lissu: Anayemfukuza atatakiwa kuandika sababu za kumfukuza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : yuko kimya tena. Hebu rudia swali.
Mhe. Lissu anarudia swali. Si ni lazima uandike sababu za kumfukuza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Siku mjibu maombi wa Kwanza alipokataliwa kuingia gerezani tar. 28/11 alipokataliwa kuingia gerezani iliandikwa sababu kuwa amekataa kusachiwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kwa kanuni hii.
Mhe. Lissu: Tutajie kanuni hizo zingine tuzione? Kwenye kanuni kuna sababu yoyote nyingine kwa mujibu wa kanuni?
Bwana Jela: Sijaipitia kanuni yote.
Mhe. Lissu: Sasa mimi niliyepitia kanuni zote na hakuna sababu nyingine unasemaje?
Bwana Jela: Sina jibu.
Part 20 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 15
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Je askari magereza ambae hasikii au hauoni atashuhudiaje mazungumzo ya mfungwa na ndugu zake watakapokuja kumtembelea
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayo ni masuala ya kidaktari.
Mhe. Lissu: Sasa Bwana Jela hujui kama wasaidizi wako wote hao kuwa hujui kama wanasikia au hawaoni wewe ni mkuu wa gereza wa aina gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sik daktari.
Mhe. Lissu: Wewe ni Mkuu wa Gereza wa aina gani? Usiyejua afya za wasaidizi wako?
Ntamamiro (Bwana Jela): Nastahili kuwa kwenye nafasi hii.
Mhe. Lissu: Ndio maana nchi imekwama. Kama watu wenyewe ndio nyie na akili hizi
Mhe. Lissu: Umekuwa Officer incharge tangu lini pale Ukonga?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sept. 2025.
Mhe.Lissu: Ulihamishiwa Ukonga ukitokea gereza kuu la maweni Tanga?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio.
Mhe.Lissu: Ulikuja ukonga kuchukua nafasi ya Juma Mwaibaku?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli.
Mhe. Lissu: Ulipohamishiwa Ukonga mimi tayari nilishakuwa mahabusu ukonga toka April 2025?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Wakati unahamia Ukonga ulikuta nakaa kwenye special wing pale ukonga?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli
Mhe. Lissu: Wakati unahamia pia ulinikuta naishi huko pamoja na wafungwa wa adhabu ya kifo 100?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sikuwakuta.
Mhe. Lissu: Je ulinikuta nakaa peke yangu au sio peke yangu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio peke yako.
Mhe. Lissu: Wafungwa gani hao?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mmoja.
Mhe. Lissu: Je kwa miezi 5 ambayo hukuwepo nilikuwa naishi na wafungwa wa kifo takribani 100?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sifahamu.
Mhe. Lissu: Umeona record ya maandishi ya waliokuwepo special wing umeiona au hujaiona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijapitia hiyo records.
Mhe: Lissu: Hili suala nilishalilalamikia na lipo kwenye nyaraka za mahakama.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sifahamu. Tuendelee na maswali mengine.
Mhe/ Lissu: Utaratibu wa wageni kuja kuniona ni weekend?
Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli
Mhe. Lissu: Utaratibu wa wageni wangu kuja kuniona weekend ni kwamba siku moja wanakuja ndugu zangu na siku nyingine wanakuja viongozi wa Chama.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sifahamu.
Mhe.Lissu: Wakati unahamia Ukonga ulikuta utaratibu wa kutembelewa na mawakili wangu ilikuwa nimepeleka orodha kwa mkuu wa Gereza kwa mkuu wa gereza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Orodha ya kwanza uliiambatanisha kwenye hati yako ya kiapo kinzani ile ambayo nilikuwa na mawakili 10.
Ntamamiro (Bwana Jela): Orodha hiyo hiyo moja.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hakukuwa na orodha yenye jina la Deogratias Mahinyila, Paul Kisabo na Dickson Matata na Mary Stephano.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuna hiyo.
Mhe. Lissu: Angalia kielelezo SUPP 1. Ukishakiona niambie.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Anapekenyua hapa..
Mhe. Lissu: Jina la Nashon Nkungu limo kwenye hiyo orodha lipo au halipo? Ambae ni mleta maombi wa pili.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio lipo.
Mhe. Lissu: Je jina la Kisabo na Maduhu mawakili wangu yapo au hayapo kwenye hiyo SUPP 1
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hawa hawapo kwenye hii orodha.
Mhe. Lissu: Sasa hao wawili wamesema kwa kiapo na kusema hapa Mahakamani kuwa kabla hujahamia ukonga walishaingia gerezani kuonana na mimi walishaingia karibia mara tatu. Wewe unasemaje? Yaani wakati ACP Juma Mwaibako akiwa Mkuu wa Gereza walihudhuria
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ulikuwepo wakati huo?
Bwana Jela: Sikuwepo wakati huo. Ila nyaraka zinasema.
Mhe. Lissu: Nenda kielelezo ambacho ni SUPP 2 hapo.
Jaji: SUPP 2 ni nini?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hiki ni kiambatanisho na. 2 kinahusu orodha ya wageni na mawakili waliotembelea gereza la Ukonga.
Part 16 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 14
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza, Ntamamiro (Bwana Jela)
Mhe. Lissu: Mmeleta PSO hapa?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio mawakili wangu waliileta.
Jaji: Wakili wa serikali nenda kaongee na shahidi wako anajua.
Mhe. Lissu: Sasa Shahidi nataka tuzungumze juu ya utaratibu wa mazungumzo kwa wafungwa au mahabusu? Tuanzie hapo. Soma kanuni ya 9(h) ya kanuni za usimamizi wa magereza. Je ni kweli wafungwa wana haki ya kutembelewa gerezani?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli.
Mhe. Lissu: Wafungwa watatimiza haki hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 12 ya kanuni hizo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni kweli
Mhe. Lissu: Soma kanuni ya 12(5) inasemaje? Je kwa kanuni hiyo wafungwa wanapotembelewa na wageni wao mazungumzo yao yatafanyika kwa kuona na kusikilizwa na afisa gereza mmoja?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sawa kwa kanuni hii.
Mhe. Lissu: Inahusu wageni wote wa wafungwa?
Ntamamiro (Bwana Jela): inategemea.
Mhe. Lissu: Utaratibu wa kutembelea wafungwa wa kifo na wa kawaida ni tofauti?
Ntamamiro (Bwana Jela): Inategemea.
Mhe. Lissu: Je askari mmoja kwa wafungwa wa kawaida na askari wawili wa wafungwa wa kifo. Utaratibu wa kutembelewa kwa wafungwa na watu wa kawaida na mawakili wao ni sawa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa mawakili askari ataona lakini hatasikiliza.
Jaji Rumisha: Si unaona tunaenda vizuri sasa Lissu.
Mhe. Lissu: Vizuri kabisa sasa shaidi tuambie mkuu wa gereza la ukonga una matatizo ya kusikia au hauna?
Ntamamiro (Bwana Jela): niko vizuri mimi. Nasikia.
Mhe.Lissu: Assistant Commisiomer on Prison Recha. Ana matatizo ya kuona na kusikia au hana?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui.
Watu wanacheka kimya kimya. Boss hajui kama msaidizi wake anasikia vizuri au laa😂
Mhe. Lissu: Je ACP Mumbii nae ana matatizo ya kusikia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sio Daktari sijui.
Mhe. Lissu: Je ACP Mohamed nae?
Ntamamiro (Bwana Jela): nae pia sijui kama ana matatizo ya kusikia.
Mhe. Lissu: SGT. Hamisi vipi nae anasikia au hasikii?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui.
Mhe. Lissu : Insp. Stima legal officer nae vipi anasikia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nae pia sijui.
Mhe. Lissu: Wale akina mama watatu wanaofanya kazi admission office wana matatizo ya kusikia na kuona au hawana?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui.
Kwa Kifupi kesi imeanza sasa.😂😂😂
Mhe. Lissu: Koplo Dani mtunza fedha nae vipi ana matatizo ya kusikia au vipi? Maana na yeye mara zote huwa yuko ofisi ya admission?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui.
Mhe. Lissu: Wale maaskari ambao huwa wanatoka na mimi ninakolala na kunileta kwako Insp. Kaisi na Mwingia wakiongoza nao pia huwa wanatatizo la kusikia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji umefanya kazi Magereza kwa miaka mingapi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ni mingi tu.
Mhe. Lissu: Mingapi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Zaidi ya 25
Mhe. Lissu: Uliingia mwaka gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : 1995.
Mhe. Lissu: Kwahiyo ni miaka 31?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Mhe. Lissu: Umepitia mafunzo mbalimbali jadi kufikia cheo ulichonacho sasa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni sahihi.
Mhe.Lissu: kwahiyo wewe ni msomi wa masuala ya magereza hadi umefikia hapo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Mhe. Lissu: Je kwa uzoefu wako jeshi la magereza linaweza kuajiri askari haoni au hasikii?
Ntamamiro (Bwana Jela) : haliwezi kuajiri. Lakini unaweza kuumwa ukiwa kazini.
Mhe. Lissu: akiajiriwa haoni akapofuka ataendelea kuwa askari magereza.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sio daktari
Watu wanacheka.😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Kama atakuwa hasikii je ataendelea kuwa askari magereza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Hata kutokuwa na jibu ni jibu pia.
Mhe. Lissu: Je askari magereza ambae hasikii au hauoni atashuhudiaje mazungumzo ya mfungwa na ndugu zake watakapokuja kumtembelea.
Part 15 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 13
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Ntamamiro (Bwana Jela)
Jaji: Sasa Bwana jela umeulizwa kuhusu kanuni tu. Jibu kwenye kanuni
Mhe. Lissu: Huko tutafika anakotaja anijibu tu ni kanuni gani inasema mfungwa wa kawaida atalindwa na askari wawili?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kwa kanuni hii hakuna kokote.
Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizo wafungwa wamegawanywa kwa makundi matatu? Au unataka nikutajie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nitajie?
Mhe. Lissu: Fungu la tatu soma wapo watoto, wapo wafungwa wanaoitwa star prisoners, na kundi la tatu ni wafungwa wa kawaida?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Hao wanaoitwa young prisoners ni wenye chini ya miaka 21.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli
Mhe. Lissu: Wanaoitwa wafungwa nyota ni wale first offenders? Wamefanya kosa kwa mara ya kwanza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli
Mhe. Lissu: Oridnary ni wale wafungwa wengine wanaobaki wote wasio kundi la kwanza na la pili?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Jana ulimsikia Kalokola wakili wa serikali akisema kuna wafungwa wa umuhimu wa kisiasa au alisema Prisoners of Security Importance Je kwa kanuni hizo wapo?
Ntamamiro (Bwana Jela): Majaji mimi naongoza kwa mujibu wa sheria zingine pia ila Kwa mujibu wa kanuni hizo hawapo.
Mhe. Lissu: Sasa twende kwenye Sheria yenyewe. Soma kifungu cha 29 kinahusu classification of Prisoners.
Bwana Jela anakitafuta kwa muda mrefu sana.
Mhe. Lissu: Hawajakuandaa hawa watu. Unatumia muda mrefu sana kutafuta kifungu. Na niliwaambia.
Sasa nikwambie inasema hivi utatenga wafungwa kama walivyoelekezwa na sheria kwa makundi. Kweli au sio kweli?
Au nikusomeee?
Ntamamiro (Bwana Jela): sikioni.
Jaji: Msajili nenda kamsaidie akione.
Mhe.?Lissu: Ni kweli kifungu hicho kinasema unapaswa kutenga kwa zile classification tatu nilizosema?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli
Mhe. Lissu: Eheeee unawatenga vipi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Nimesema tunaongozwa na kanuni, sheria na miongozo mbalimbali.
Mhe. Lissu: Tulitoka kwenye kanuni sasa tupo kwenye sheria muda huu.
Ntamamiro (Bwana Jela): Naomba nipewe muda.
Jaji: Sasa Wakili wa Serikali ongea na shahidi tunataka kusogea mbele. Msaidie anachotafuta.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni sahihi kuwa sheria inasema kama ulivyosema.
Mhe. Lissu: Je wewe mkuu wa gereza la ukonga au mkuu wa gereza lingine mnaweza kubadili makundi hayo matatu tuliyosoma kwenye sheria. Na kuweka category nyingine nje ya za kwenye kanuni?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina uwezo huo.
Mhe. Lissu: Haya Makanuni hatujayatunga wewe, wewe jibu tu swali chakufia nini? Sasa tuambie Kamishna wa Magereza kama nae ana mamlaka ya ku change category za wafungwa zilizopo kwenye kanuni. Je Boss wako anayo hayo mamlaka? Yaani Principal Commissioner
Ntamamiro (Bwana Jela): Hana uwezo.
Jaji: Hebu tueleze vizuri.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kwa sasa Commisioner General wa magereza anao uwezo wa kutunga kanuni zingine.
Mhe. Lissu: Swali ni je kubadilisha kanuni za Waziri ana uwezo huo?
Ntamamiro (Bwana Jela): nashindwa kuelewa.
Jaji: Sasa Shahidi hizi kanuni narudia tena hukutunga wewe. Jibu tu swali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hana uwezo wa kurekebisha wala ku ammend. Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kifungu cha 105(1) kinasema kwa kifungu hicho ni waziri peke yake ndio mwenye mamlaka ya kutunga kanuni za utekelezaji bora wa kanuni hizi?
Jaji: Lissu endelea kuuliza swali.
Mhe. Lissu: Sasa jibu swali langu la mamlaka ya kutunga kanuni bora za utekelezaji wa kanuni hizo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Haisemi Waziri peke yake.
Mhe. Lissu: Waziri anaweza au hawezi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Anaweza.
Mhe. Lissu: Ni wapi pameandikwa kuwa Kamishna General anaweza kutunga kanuni?
Ntamamiro (Bwana Jela): Sipaoni hapo.
Part 14 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 16
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Mkuu wa Gereza
Mhe. Lissu: Twende Taratibu. Hiki ulicholeta mahakamani ni photocopy?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
Mhe. Lissu: Original unayo ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Angalia Tar. 29 na Tar. 30 Sept. 2025. Kuna majina ya wageni kabla ya Tarehe hizo wapo wageni hawaonekani walikuja tarehe gani?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni kweli
Mhe. Lissu: Hawa watu wanne walikuja tarehe ngapi? Wambie majaji sasa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Haioneshi.
Mhe. Lissu: Wewe unajua sasa? Walikuja tarehe ngapi? Maana original unayo wewe.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Tarehe haioneshi.
Mhe. Lissu: Je katika hao watu wa nne. Mtu wa 10 ni nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Paul Kisabo.
Mhe. Lissu: Alikuja kumuona nani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : wewe hapo imeandikwa. Alikuja kukuona wewe.
Mhe. Lissu: Soma Tar. 30 Sept. Kwenye karatasi hiyo hiyo. Mtu wa kwanza ni Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Tusiende mbali sasa: Tufafanulie jambo hapa kuna sehemu imenadikwa jina la ndugu, ID no. Simu namba, atokapo mgeni na maoni ya OIC. Sasa hiyo OIC ni Officer in Charge yani wewe hapo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Tar. 30/09 kwenye jina la Kisabo uliandika A/Zamu maana yake Afisa wa Zamu. Na kuna mahali umeandika ADM maana yake ni admission office in charge. Na kuna mahali umeandika IO maana yake intelligence officer?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: na kuna sehemu umeandika legal unamaanisha Legal Officer Stima.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
Mhe. Lissu: Hiyo sehemu ya maoni yako ni maelekezo yako kwa hawa niliowataja? Wewe ndio Boss.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kila ofisa ana kazi yake. Kwahiyo ni maelekezo yangu kwao.
Mhe. Lissu: Kwahiyo unakuwa umewapa amri?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
Mhe. Lissu: Nenda Kwenye kilelezo SUPP 3 pia ni orodha ya mawakili waliokuja Ukonga. Nashon Nkungu lipo hapo ambae ni mlalamikaji wa pili. Andrew Mathew Chima pia alikuja kuniona?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Mhe. Lissu: Je Andrew Chima yupo kwenye orodha ile ya mawakili wangu niliowaletea ile SUPP 1?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayupo. Naomba nifafanue.
Mhe. Lissu: Sitaki. Utawafafanulia wa Serikali.
Haya huko mwisho kabisa KULWA MADUHU yupo au hayupo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Yupo namuona hapa.
Mhe.Lissu: Na kule mwisho kwenye maoni yako umesema aruhusiwe mwenye kibali. Maduhu hana kibali huko mbele sioni.
Ntamamiro (Bwana Jela): hayuko kwenye orodha ya mawakili wa mahabusu huyu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kuna sharti lolote la kisheria kwamba mfungwa yeyote mwenye wakili au wakili anapaswa kuwasilisha orodha ya mawakili wake kwa Bwana Jela?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Halipo kisheria. Lakini mfungwa ana haki ya kuchagua nani amtembelee.
Mhe Lissu: Nilichagua kuwa Kulwa William Maduhu na umemkatalia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hakuwepo kwenye orodha.
Mhe. Lissu: Andrea Chima alikuja kuniona yupo kwenye orodha gani?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hayupo.
Mhe. Lissu: SUPP 5 twende sasa tar. 24/12/2025 angalia kwenye entry kuna Nashon Nkungu na Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio wanaonekana wote.
Mhe. Lissu: Je Victoria Mgonja alikuja kumuona Jonson Muhanjo. Uliandkka kwenye maoni yako kuwa Adm. Simamia mazungumzo yao. Na mazungumzo hayo yalifanyikia kwenye ofisi ya Admn
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina kumbukumbu yalifanyikia wapi?
Mhe. Lissu: Kwamba tangu juzi tunazungumza kuhusu mazungumzo ya mawakili yalifanyikia wapi hujaenda kutafuta.
Ntamamiro (Bwana Jela) : sijui inaweza kuwa kwa Mkuu wa Gereza au Adm.
Mhe. Lissu: Mazungumzo na Nashon ulisema asimamiwe kwa Makamu mkuu wa gereza na kuwataka wasaidizi wako wanne wasimamie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Part 17 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 12
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Ntamamiro (Bwana Jela)
Ntamamiro (Bwana Jela) : Lakini suala la searching zipo sheria zingine.
Mhe. Lissu: Sasa huko tutafika. Mashahidi wengine nilikuwa nawambia waache kiherehere sasa unataka na wewe nikwambie hivyo halafu tutaendaje Ukonga baadae, sitaki kukwambia hivyo Afande wangu.
Watu wanacheka. Majaji pia wanacheka sana. 😂😂😂😂
Mhe.Lissu: Sasa soma kifungu cha 105(1)(l) kama hakisemi kuwa Waziri ndio mwenye mamlaka ya kutunga kanuni za management na treatment za prisoners. Ndio au hapana?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Naomba nielezee kidogo.
Mhe. Lissu: Nimesema mimi na wewe kwetu ni ukonga tukitoka hapa. Tukitoboa mtumbwi tutafika? Haya jibu swali tusigombane?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kweli
Mhe. Lissu: Kamishna Mkuu ana mamlaka ya kutunga hizo kanuni za kutunga mambo haya ambayo nimesema hapo juu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Waziri ndio amempa mamlaka kamishna wa magereza.
Mhe. Lissu: kwa kifungu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kile nilichosema cha 5(2)
Mhe. Lissu: Kile hakijataja Prisoners sasa.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kimetaja Prison ndio Prisoners wapo.
Mhe. Lissu: Kasome Definition section kwenye hiyo sheria kuna tofauti kati ya Prison na Prisoners. Havitumiki interchangebly. Gereza na wafungwa ni vitu tofauti.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui.
Mhe. Lissu: Kanuni ya 8 ya kanuni za usimamizi magereza. (Prison Management regulation) je inaeleza utaratibu wa ku search wafungwa.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio lakini zipo na sheria zingine.
Mhe. Lissu: Tutaenda kila mahali. Tutafika kwa hizo sheria zote.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sawa. Nakubali.
Mhe. Lissu: Haki za wafungwa tunaenda kanuni ya 9 hadi ya 11?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli
Mhe. Lissu: Kanuni ya 12 na Kanuni ya 17 je kanuni hizo zinahusu haki ya wafungwa kutembelewa gerezani?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli.
Mhe. Lissu: Soma kanuni ya 13 na useme inahusu nini? Ni kweli inahusu haki ya wafungwa kutembelewa na mawakili au washauri wao wa kisheria?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Kanuni hizo pia zimeeleza hata namna ya adhabu ya kifo ifanyike kwa maana ya kunyonga wafungwa na masuala yote yanayohusu wafungwa wa adhabu ya kifo? Soma kanuni ya 33.
Ntamamiro (Bwana Jela): haeleweki amesoma nini?
Mhe. Lissu: Ngoja nikusomeee. Anamsomea hapa.
Ntamamiro (Bwana Jela): Nilikuwa sijaiona nimeiona.
Mhe. Lissu: Namna ya kunyoa wafungwa si imeandikwa kwenye kanuni?
Ntamamiro (Bwana Jela): Naam
Mhe. Lissu: Mimi huoni nimefuga rasta sio mfungwa ndio hamuwezi niambia chochote unaelewa hilo?
Ntamamiro (Bwana Jela): uko sahihi.
Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizo mahabusu kama mimi napaswa kusimamiwa na askari magereza wawili usiku na mchana.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kuna kipengele cha segregation kwenye sheia zetu.
Mhe . Lissu: Jibu kwa kanuni hizo?
Jaji: Kamishna hakuna mtu atakuadhibu maana kanuni hujatunga wewe. Kwahiyo kama kanuni hazisemi sema hazisemi. Usijipe presha kabisa mzee wangu.
Kumbukeni ana miaka 57 huyu Ntamamiro (Bwana Jela).
Ntamamiro (Bwana Jela): Hakuna hiyo kanuni.
Mhe. Lissu: Ni wafungwa wa adhabu ya kifo tu ndio wanatakiwa kulindwa na askari wawili na wasikilizwa mazungumzo yao ni wa adhabu ya kifo pekee? Kweli au sio kweli.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli
Mhe. Lissu: Inasemaje Baba yangu? Kwanza wewe sio Baba yangu mimekuzidi umri. Si umesema una miaka 57.
Ntamamiro (Bwana Jela): Kwa mujibu wa hiki kifungu ni sahihi wafungwa wa kifo ndio wanapaswa kulindwa.
Mhe. Lissu: Safi tukienda hapa tutafanya vizuri. Kwa hayo ambayo umeyasoma na kwa kanuni hizo. Mahabusu, mfungwa hatakiwi kulindwa muda wote kwa masaa 24 isipokuwa wa kifo kwa mujibu wa kanuni hizo? Kanuni ipi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Nimesema Jeshi la magereza linaendeshwa na kanuni, sheria na miongozo.
Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Tundu Lissu; Je, ni kweli au siyo kweli kwamba uliniita ofisini kwako, ukasema natakiwa kuonana na ujumbe wa Lazarus Chakwera kutoka Jumuiya ya Madola?
Mkuu wa gereza Ukonga; Sina jibu
Tundu Lissu; Je, ni kweli au si kweli kwamba ulisema nipelekwe kuonana na ujumbe huo na Afisa magereza wa mkoa SACP Mangala.
Mkuu wa gereza Ukonga; Si kweli
Tundu Lissu; Kama si kweli, huko kuonana na Chakwera nilipelekwa na nani?
Mkuu wa gereza Ukonga; Sijasema ulipelekwa
Tundu Lissu; Umesema huna jibu
Mkuu wa gereza Ukonga; Nimesema hujawahi kupelekwa
Tundu Lissu; Kwa hivyo nilikwenda kumuona kwa ruhusa ya nani?
Mkuu wa gereza Ukonga; Sina jibu.
Leo Watu wa MBEYA wakishiriki IBADA YA HAKI.
DAMU za ndugu zetu walizomwaga MO29 tutaendelea kuzipigania mpaka HAKI ipatikane.
Chama pekee kinachoongoza mapambano haya na kulia pamoja na wanaolia ni CHADEMA.
Mbeya hatuwezi kuwasahau mashujaa wetu wa MO29 na hatutasahau kwamba DIKTETA JIKE SAMIA aliwauwa watanganyika kwa maelfu ili abaki ikulu.
Kama umeshiriki IBADA HII wanangu wa MBEYA MUNGU awabariki—tuendelee kuwa pamoja tupo mwishoni tunaelekea KUSHINDA.
#FreeTunduLissu
#KatibaMpyaFreeTunduLissu
REPOST 200
Mkutano Mkuu wa 87 wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) [87th Plenary Assembly - Study Session] unaendelea katika ukumbi wa Amecea uliopo ndani ya Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu Kurasini Jijini DSM.
Mkutano huo unaongozwa na Rais wa TEC, Mhashamu Baba Askofu Wolfgang Pisa, OFMcap, na umehudhuriwa na Maaskofu wote wa Kanisa Katoliki Tanzania, Wakuu wa Taasisi za Kanisa, Wakuu wa Mashirika na Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa.
Mada kuu katika mkutano huo ni: Haki za Rasilimali Tanzania. Mada hiyo inatokana na waraka uliotolewa na Baba Mtakatifu Leo XIV kwa Kanisa. Kwa lugha rahisi ni kwamba sehemu ya watu walioelimika zaidi nchini (think tank ya nchi) wamejifungia Kurasini kujadili kuhusu Haki za rasilimali zetu.
Sasa subiria waje na tamko halafu usikilizie "wanyonyaji" wa hizo rasilimali watakavyotoa milio. Roma Locuta causa finita est.!
Nimeamka nakuta Buyobe ametumia screenshot ya akili mnemba ambayo iliyumika na “CHAWA wa Mama” kumuattack Mshabaha.
Sasa nafikiri tumemjua nani alikuwa anawapa info za UONGO wale CHAWA. Acha upepo uendelee KUVUMA tutajua yote.
Mimi naendelea kunote down wanangu.✍️
Mnataka apendwe au aogopwe?
Kauli za vitisho, mauaji, kuteka, kupoteza, kufunga na kuua watu ..
Mnaweza kuzifanya kwenye Nchi ambayo basically haina vyombo vya habari. Mahakama na Bunge vyote vimegeuka sehemu ya serikali.
Kwenye Nchi za watu wastaarabu kila kauli unayotamka itawekwa kwenye mzani na umma utakuona kwa sura halisi.
Asanteni sana ndugu zetu wa Kenya.
Tukikosoa, tukishauri na kuikemea serikali tukiwa mbali, mnasema fimbo ya mbali haiui nyoka.
Wewe ulioko hapo Kongowe umeshaua nyoka wangapi na fimbo yako ya karibu?
So Kenya is the most democratic country in Eafrica. Wametuacha mbali mno na demokrasia yao,although not perfect ila ni mfano wa kuigwa na nchi zingine Africa.
That said, it is shocking to see a sitting Kenyan president affectionately call “dada” a woman who just butchered her own people to hold onto power. It is shocking to watch a Kenyan president enable the killing of Tanzanians and remain silent while Kenyans were kidnapped, tortured and raped in Tanzania. Matter of fact from how Samia speaks around him and how close they appear to be, it’s clear Ruto supported the rape and torture of Kenyans by Samia Suluhu.
After the killing of more than 10,000 protesters, and the kidnapping and rape of Kenyan activists by an illegitimate Tanzanian president , how can a Kenyan president bring himself to refer to Samia Suluhu as his sister? it sends the message that he would do the same if he had the balls. It seems he admires that Samia did on October 29.
Kenyans, whatever you do next year, you must vote Ruto out of office and elect a leader who will stand for democracy across East Africa. Removing Ruto from office and choosing someone willing to publicly condemn the killings in Tanzania and the torture of Kenyans there would be a meaningful step forward for the future of East Africa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa serikali kupuuza madai ya mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi kumesababisha mauji ya tarehe 29 Oktoba.