Sio kila mtu atafanikiwa ili maadui zake waone ukuu wa Mungu, ila kuna wengine watawaona adui zao wakizidi kufanikiwa ili ujue kuwa Mungu huwapa hata wale usiowapenda.
#chungu_pia_huliwa
Kuwa mtu wa kanisani au msikitini sana hakukupi kibali cha kuwa wewe ni mkamilifu kuliko wengine. Kwani hata magari yaliyochapishwa maneno matakatifu huanguka.
#chungu_pia_huliwa
Moja kati ya kichekesho kikubwa zaidi duniani ambacho hakikuwahi hata kupata tuzo, ni kumkejeli msomi huku ukipambana sana kutafuta ili mwanao au ndugu asiishie ulipoishia kielimu.
Nafahamu changamoto, maumivu na vilio ni ukamilifu wa mwanadamu, lakini nakuombea kila namba iliyoisimamisha kalenda ya 2025 ikawe yenye kheri nyingi zaidi kuzidi mzani wa mapito yako.
Amini usiamini wapo wasiokupenda na wenda ukawa unawakera zaidi ukiwa karibu nao, ila kinachowafanya wacheke na wewe ni mikakati yako inayowafanya kufikiria kuwa mbona huyu kama atakuja kufanikiwa. Hivyo wanayakimbia majuto ya kwanini hawakukuigizia tabasamu hapo awali.
Wizara ya mipango ya maisha ya binadamu iliyochini yake mmiliki wa ardhi na mbingu ndiyo yenye haki miliki ya maisha yako, hivyo hata mwenye PhD ya mipango mibaya juu yako anatakiwa arudi darasani upya kwani haitomfaa elimu yake juu ya mazuri yaliyo kwenye kalenda yako.
Watu sio kwamba wanapenda kurudi makwao wakiwa marehemu au kurudi wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vya miili yao, ila tayari inakuwa ishaandikwa machozi yatengenezwe kwa usafiri walioupanda. TUSIACHE KUWAOMBEA NDUGU ZETU WALIOSAFARINI, KWANI QADARI HUBADILISHWA KWA DUAπ€²
Yawezekana umejaribu sana kuipambania CHANYA lakini majibu huja HASI. Unaumia zaidi kuona unalolihitaji halitimii. Pole sana lakini huna budi kukubaliana na hali, huwezi jua pengine andiko lako mbinguni linasema utakuwa hivyo au hutalipata ulitakalo hadi unaingia kaburini...βοΈ
Amini usiamini, Mungu hajawahi kuruhusu mikono ya mwenye IMANI, mwenye NIA na Mwenye HAKI ishuke mitupu, kamwe hajawahi kuandika iwe hivyo. Haijalishi ni kwa muda gani utasubiri, lakini tabasamu ni haki ya uso wako na utulivu ni haki ya moyo wako. MPE MWENYEZI MUNGU MUDAπ.
Unaona hivyo ulivyo! Tena pengine sio makosa yako,Lakini kuna nafsi zinakucheka chini kwa chini kila wakutazamapo,Tena huenda mbali zaidi na kutafsiri muonekano wako kama aibu kwao. Hakika inasikitisha sana Bunifu na Rizki za Mwenyezi Mungu zinakosolewa na wasio na maarifa ya UTU