Haki ya kuishi ..... Hii haki huwezi kuitenganisha na dhana ya utashi wa mtu katika kuishi......utashi wa jinsi ya kuishi unamthaminisha mwanadamu na kumtofautisha na mwanadamu mwenzake mwisho kabisa tunapata historia yenye kubeba utu wake ....
Njia yeyote itakayo wahakikishia watu wajamii ya kimaasai Haki yao ya Kuishi kwa uhakika katika eneo na ardhi yao ya Asili inatakiwa kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi mema.Njia yeyote ya kuwanyima haki hii ikemewe kwa nguvu zote.
Baada ya kusoma komenti kwa utulivu nimegundua mawazo mchanganyiko ya watu mbalimbali kutokana na imani na malezi yao, pamoja na mazingira yao kabla.
Lakini kuanzia leo mimi ntaanza kuoga kuanzia miguuni!
@KagutaMuseveni I was following your speech mzey @KagutaMuseveni that I learned to deserve you that handout you were talking in speech I wish you to send it to me you could be helping the poor african here
Hichi ni kipindi muhimu sana kwenye hizi harakati. Naweza nisifahamike na wengi lakini imani yangu inaniambia Rais aina ya Kikwete na mama Samia ni hatari zaidi ya Magufuli. Unapokuja na maneno matamu ya kuwahadaa watu bila ya utekelezaji wowote huwa unawadumaza akili. Huku ukipuuza mambo muhimu mkubwa ambayo watu walitarajia yangeleta mabadiliko. Anaewapiga na kuwatesa huwa anawakomaza na kuwajenga kiimani baada ya mateso makali.
Lakini kwa kuwa mimi si Jeshi la polisi bali ni mtu ninayejifanya Askofu wakati hata uaskofu umenishinda, nabakia kutamani kuwa polisi huku nikijua kuna polisi wanatamani kuwa Askofu.
NCHI HII KUBWA: Bora Taharuki kuliko Mauaji.
ANAANDIKA BABA ASKOFU BENSON BAGONZA
Sifa moja muhimu ya kiongozi ni kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa jamii.
Nyumba inapoungua moto, ni bora kuokoa hata godoro moja kuliko kuua panya wanaokimbia moto unaounguza nyumba.
Mitandao ya kijamii usiku wa leo (25/4/2024) imejaa habari za Mwanaharakati wa haki za kijamii Malisa GJ na Mwanasiasa/Mwanaharakati Jacob Boniface kukamatwa na polisi kwa KUSABABISHA TAHARUKI wakati wanaripoti “mauaji” ya mtu mmoja aitwaye Mushi.
Kama ningelikuwa jeshi la polisi ningetafakari haya kabla ya kufanya maamuzi:
1. Nchi hii ni kubwa sana. Jeshi la polisi ni dogo kuliko uhalifu. Wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu ningewafanya marafiki kuliko maadui.
2. Ni kweli Mushi amekufa. Ningeshughulika na wauaji kuliko kushughulika na waliosababisha taharuki.
3. Ningejiuliza; taharuki imesababishwa na ripoti ya kifo au kifo chenyewe? Kifo kisicholeta taharuki si kifo kamili.
4. Malisa GJ ameisharipoti matukio mengi ya kihalifu ambayo jeshi la polisi ama halikujua au lingepata taabu sana kujua. Kwa hili la kifo cha Robert Mushi, Jeshi la polisi lingemzawadia nishani ya utumishi wa kujipendekeza kwa polisi kuliko kumkamata na kumpekua.
5. Badala ya kumpekua Malisa GJ na Boniface Jacob, ningewatumia na mitandao yao kutafuta na kujua gari linalodaiwa kumgonga marehemu Moshi.
6. Kwa kuwa nchi ni kubwa sana; ningetumia muda kuchunguza ndani na nje ya jeshi la polisi kuhusu uwezekano wa polisi vishoka wanaodaiwa kumkamata marehemu Robert Mushi kabla ya kifo chake!
7. Ningeazimia kuwalinda wanaojitolea kutoa taarifa za uhalifu kuliko wanaodaiwa kukosea katika kutoa taarifa za uhalifu ili kwa njia hiyo niongeze wigo wa watoa taarifa za uhalifu.
Lakini kwa kuwa mimi si Jeshi la polisi bali ni mtu ninayejifanya Askofu wakati hata uaskofu umenishinda, nabakia kutamani kuwa polisi huku nikijua kuna polisi wanatamani kuwa Askofu.
Natamani Jeshi la polisi liwaachie huru Malisa GJ na Boniface Jacob ili linufaike na harakati zao katika kukomesha uhalifu wa kidola na kiraia.
“Maneno ya Mwisho ni kwa wapumbavu ambao hawakusema vya kutosha walipokuwa wazima”
Hayo ni maneno ya mwisho ya mjamaa Karl Marx alipoambiwa atoe maneno ya mwisho kabla ya kifo chake..
🤣🤣