Nimetoka Ukonga kumuona Mwenyekiti, Yuko imara na anawasalimia wote.
Anatoa pole kwa Watanzania wote waliopoteza maisha, familia ndugu na marafiki.
Anatambua watu waliopoteza viungo na kubaki na ulemavu.
Ametoa pole kwa wote waliopoteza mali pia.
Damu ya wenzetu haijamwagika bure na hakuna atakaefunika jambo hili bila uwajibikaji.
Msimamo wa Mwenyekiti uko thabiti, Yuko imara na mwenye afya njema.