Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amewataka vijana wa kizazi cha sasa (Gen Z) kuishi maisha yao kwa ujasiri na kuyafurahia kwa kuwajibika. Amesema ujana ni kipindi cha kujifunza, kufanya kazi kwa bidii, kutimiza ndoto na kufurahia kila fursa inayopatikana, badala ya kuishi kwa hofu ya mitazamo ya wengine.
"Gen Z, enjoy maisha. Ujana haujirudii; ishi kulingana na umri wako huku ukijenga kesho yako."
#SikuYaVijanaDuniani
#FreeTunduLissu
#KijananaKatiba
#Tukutane Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), akiambatana na mume wake,Wakili Mathusela Gwajima wakiwasili katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma tarehe 1 Juni, 2026 kwa ajili ya kuwasilisha Hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Kyela, Victoria Swebe, ametoa tamko kali dhidi ya kile alichokiita "siasa za mateso" na kesi za kutengenezewa, huku akitaka mamlaka kukomesha vitendo vya utekaji na mauaji nchini.
Akizungumza wilayani humo jana, Aprili 21, Swebe ameweka wazi kuwa chama hicho hakiwezi kufurahia uhuru wa kisiasa uliotangazwa huku viongozi wake wakuu wakiendelea kusota gerezani kwa tuhuma zisizo na mashiko.
"Tunajua haki imetendeka kwa CHADEMA kuruhusiwa kufanya siasa, lakini furaha yetu haijakamilika. Tunatamani kusikia kesi ya Lissu imefutwa na Mwenyekiti wetu yuko huru. Huwezi kuwa na kesi ya uhaini au ugaidi ya mtu mmoja; hizi ni kesi za mchongo zinazomlenga mtu anayepigania haki ya chama chake," alisema Swebe.
Kiongozi huyo, akionekana kuguswa hisia, amekumbushia matukio ya Oktoba 29, 2025, akijitaja kama mhanga wa moja kwa moja wa machafuko ya kisiasa yaliyopelekea vifo na upotevu wa wapendwa wake ambao maeneo yao ya maziko hayajulikani mpaka leo.
"Kama mzazi, moyo wangu unauma sana. Kila siku tunasikia watu wanatekwa na hawaonekani. Watawala lazima wapaze sauti kukemea mauaji na utekaji huu. Mungu aishie anajua, na kila mmoja atavuna kile alichokipanda," ameongeza.
Swebe alirejea uzoefu wake wa kukamatwa mara kwa mara, ikiwemo kuwekwa kizuizini kwa siku 15 kwa tuhuma za uongo na hata kuswekwa ndani kwa siku nne kwa kuvaa sare ya CHADEMA kanisani. Amesema vitendo hivyo vimeimarisha uthabiti wake badala ya kumvunja moyo.
Alimalizia kwa kusisitiza: "Imani yangu ni CHADEMA. Watauumiza mwili wangu lakini si imani yangu. Sisi tunahubiri haki na tunatenda haki, na ndiyo maana kila mara kesi zetu zinaishia kwenye haki. Hatutaacha msimamo huu."
Nimepata morali zaidi. ✊🏾
Mwenezi wa wahuni wa mbogamboga anapiga marufuku Watanzania wasituchangie, sisi tunaongeza kasi. Usiku huu nimebarikiwa chochote kitu na kuchangia Tsh 100,000 kuunga mkono harakati za ukombozi wa kweli.
Ikiwa 'Tone Tone' inawanyima usingizi kiwango hicho, basi tujue tuko kwenye mstari sahihi. Ungana nami kuwezesha mabadiliko leo. Kama unaguswa na mustakabali wa nchi yetu, usisite kutoa ulichonacho.
Uhuru wa Kifedha: Chama cha siasa kinachofadhiliwa moja kwa moja na wananchi wenyewe kinawajibika moja kwa moja kwa wananchi, si kwa wafadhili wakubwa au mifumo ya siri. CHADEMA ni mali ya Watanzania.
Ujumbe wa Kisiasa: Kuchangia harakati za kisiasa ni kura halali ya maoni kabla ya sanduku la kura. Michango ya fedha na mali ya hiari inatuma ishara kwamba kuna watu wako tayari kugharamia kile wanachokiamini.
Nguvu ya Umma: Dhana ya ‘Tone Tone’ inajenga bahari kubwa. Shilingi 1,000 kutoka kwa watu milioni moja ni nguvu kubwa kuliko bilioni moja kutoka kwa mtu mmoja. Tusiogope. Tuchangie wengi. Wameogopa.
Kila tone linahesabika. Namba ya Kuchangia: 0744446969 (CHADEMA HQ).
Viongozi na wanachama wameitumia siku ya leo April 16, siku moja baada ya kufunguliwa shughuli za chama kuendelea na madai ya kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa chama Mh Tundu Lissu.
#FREE LISSU