#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 27
Anaendelea Wakili wa Serikali wakuitwa Wisdom.
Wisdom : Ulipokuwa unasema wasaidizi wako watekeleze kwa mujibu wa sheria? Maana yake nini?
Bwana Jela: Kufanya kwa mujibu wa sheria tu. Kama mchungaji anaingia kwa mambo ya kiroho peke yake.
Wisdom: Uliulizwa umeleta kiapo kinzani kujibu majibu ya mjibu maombi wa nne. Ukasema hujaleta? Kwanini.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sikuleta kwasababu yeye ni mjibu maombi kama mimi.
Wisdom: Ulisema mawakili wote lazima wakaguliwe maana yake nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): kufuata sheria tu. Kuandika comment au kutoandika kunazuia sheria.
Wisdom: hebu eleza huwa mnakaguaje nyaraka?
Ntamamiro (Bwana Jela : mfano kitabu tunakagua kuangalia kuna kitu chochote hatari ndani yake.
Wisdom: Nimemaliza.
Anasimama Narindwa Wakili wa Serikali.
Wakili wa Serikali Narindwa: Kwani walioleta maombi ni akina nani?
Ntamamiro (Bwana Jela: Kulwa Maduhu, Nashon na Kisabo.
Wakili wa Serikali Narindwa: Kwani Maduhu mlimzuia asiingie?
Ntamamiro (Bwana Jela: Hakuwepo kwenye orodha na pia hakukuwa na ombi kutoka kwa Lissu.
Wakili wa Serikali Narindwa : Nimemaliza na tumemaliza, hatuna la ziada.
Majaji wanaandika.
Jaji Rumisha Anamuuliza Seka. Mnataka kusema kuwa mnahitaji mawakili wawe na chumba chao au mnahitaji haki ya msingi ya faragha ya mawakili inalindwa?
Wakili John Seka : nafikiri tudeal na soft part of it. Haki ya msingi ni nini sio lazima chumba kiwepo.
Anasimama Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji msiwe na shaka vyumba vinaweza kuwepo.
Mimi naishi Ukonga na pale ukonga kuna vyumba havinaga kazi kabisa. Mfano viko vyumba viwili vya Mahakama ya mtandao. Huwa sio kila siku kuna kesi kama waliweza kuwa na Mahakama ya mtandao pale na vyumba vyake vipo kwanini chumba maalumu kabisa cha mawakili kisiwepo?
Jaji Rumisha: Nafikiri tutajielekeza kwenye kuhakikisha haki inalindwa sio lazima majengo.
Jaji Mruma anasemam sasa Maombi ya Msingi tulisema yatasikilizwa kwa njia ya maandishi.
Na scheduling order itakuwa kama ifuatavyo.
Submission za petitioners zitakuwa ni kabla ya Tarehe: Watajibu PO na kufile submission in chief yao. Kabla ya Tar. 24/08/2026. Rejoinder ya Petitioners kwenye majibu yao 07/09/2026.
Respondets Submission zao zitakuwa ni Tarehe: Submission P.O before 10/08/2026. Wataleta rejoinder ya PO na reply yao 07/09/2026.
Mention kabla ya uamuzi ni 16/09/2026.
Mhe. Lissu anasimama anasema na mimi mseme naleta majibu yangu lini?
Jaji Rumisha: Sasa na wewe kwenye PO ambayo wamewekewa waleta maombi unataka kujibu kama nani wakati wote ni washitakiwa au wajibu maombi?
Jaji Mruma: Amedakia, Mimi nakuelewa Lissu hata kwenye kesi za kawaida za madai defendants wanaweza kuwa na madai dhidi yao wenyewe na ikasikilizwa. Kwahiyo Lissu uko sahihi na tutakupatia haki hiyo hakuna shida.
๐๐๐๐Kwa kifupi Mruma ameingilia show. Naambiwa huyu Mzee ni miongoni mwa Ma Jaji senior sana wa Mahakama Kuu na uwezo wake ni mkubwa sana. Serikali imeshindwa kumpandisha cheo kwenda Mahakama ya Rufani kwasababu yeye huwa sio Chawa kabisa. Ni Mzee anayejielewa sana na yuko serious.
Tumekuwa tukishuhudia kesi nyingi hapa Mahakama kuu kwa mara ya kwanza tumeshuhudia Jaji ambae kwakweli anajua kazi yake.
Anasimama Wakili Ukashu anasema Mh. Jaji na mimi interested party hujatutaja kabisa? Tunafile lini?
Anasimama Narindwa anasema hata sisi tunashangaa huyu Ukashu na TLS wanataka kujibu PO wao ni akina nani?
Jaji Mruma: Sasa sikilizeni msichanganyikiwe. Sisi wengine tumekaa humu miaka 30. Mimi nimefanya hizi kazi mwaka wa 30 huu. Hakuna jipya. Wewe Ukashu utatumia tarehe za 4th Respondent kujibu. Msichanganyane kabisa.
Naahirisha kesi kwa tarehe nilizosema.
NB. Nakuomba usisahau kuchangia #ToneTone ili kufanikisha BARAZA KUU.
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 26
Tumerejea baada ya Mapumnziko ya nusu saa.
Anaanza Wakili wa waleta maombi Adv. Emmanuel Ukashu kumuhoji Maswali Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana Jela)
Adv. Ukashu: shahidi umewahi kuisikia TLS?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio naifahamu.
Adv. Ukashu: Ili mtu aingie Gerezani inahitajika wewe ndio umruhusu aingie?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Adv. Ukashu: Ni sahihi ukipewa maelekezo yoyote lazima utekeleze na Kamishna General?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sahihi
Adv. Ukashu: Maelekezo kutoka juu maana yake nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni maagizo ya kiutendaji unayopaswa kutekeleza.
Adv. Ukashu: Usipoyatekeleza unaweza kufukuzwa kazi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : kwa mujibu wa sheria.
Adv. Ukashu: Unaweza kumbishia Boss wako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Siwezi kufanya hivyo.
Adv. Ukashu: Soma SUPP 4 tar. 12/03/2026 entry no. 8 hebu isome hapo.
Ntamamiro (Bwana Jela): Huruma Tehejas mfungwa aliyekuja kumtembelea ni mfungwa na shida ya kisheria. Maoni hapakujazwa. Na sahihi hamna.
Adv. Ukashu: Sasa alienda wapi huyu Wakili kama hakuna uliposaini na maoni hukuweka.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nilisahau kujaza na naamini hakukataliwa pia.
Watu wanacheka. ๐๐๐๐
Adv. Ukashu: Kwanini usifukuzwe kazi kwa uzembe wa aina hii? Maana haijulikani alikuja kufanya nini?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nifukuzwe tu kazi kama unaweza kunifukuza. Fanya hivyo ila mimi nimesema nilijisahau.
Adv. Ukashu: Unafahamu kazi ya uwakili ina maadili yake?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kila kazi ina maadili.
Adv. Ukashu: Maadili ya magereza tumeshayaona hapa hujajaza nyaraka na hujui wakili alipoingia alielekea wapi? Sasa tuzungumze maadili ya mawakili.
Ntamamiro (Bwana Jela) : siyajui mi sio wakili.
Adv. Ukashu: Unaijua Mandela Principle?
Ntamamiro (Bwana Jela): yes
Adv. Ukashu: soma hapa inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Mfungwa atazungumza na wakili wake kuwa atazungumza bila kikwazo.
Adv. Ukashu: Umeitekeleza?
Ntamamiro (Bwana Jela): Inasema nizingatie sheria za ndani pia?
Adv. Ukashu: Sasa tuambie ni kifungu gani cha sheria ya ndani ambacho kiko kinyume na Mandela Principle.
Ntamamiro (Bwana Jela): Hakipo.
Adv. Ukashu: Nimemaliza. Naomba Wakili Neema aendelee.
Anasimama Wakili Neema Saruni.
Adv. Neema Saruni: Nitakuwa sahihi nikisema mtu anayekuja kumuona mfungwa anapaswa kuwa na sababu ya msingi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ni sahihi kwa mujibu wa Sheria.
Adv. Neema Saruni : Ulisema mjibu maombi wa nne alikuwa na orodha yake hivyo basi alipotokea hayupo mlimrudisha?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio tulifanya hivyo.
Adv. Neema Saruni : Nitakuwa sahihi nikisema hamkumpatia haki yake ya kusikiliza.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sahihi.
Adv. Neema Saruni: Nilipokuja mimi kumuona Lissu nilikuwa kwenye orodha yake?
Ntamamiro (Bwana Jela): Haukuwepo.
Adv. Neema Saruni : Nilipofika ikawaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): tulienda kumuuliza lissu.
Adv. Neema Saruni : akasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Akaruhusu ukamuone.
Adv. Neema Saruni: Kwanini huyo mwingine mlimrudisha bila kwenda kuuliza Lissu anasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Hapo sasa ndio kuna utata.
Watu wanacheka ๐๐๐
Adv. Neema Saruni: Nimemaliza.
Haya wanasimama mawakili wa Serikali, anaanza Wakili wa Serikali anaitwa Wisdom
Wakili wa Serikali Wisdom: Ulitekeleza majukumu yako kwa mujibu wa nini?
Ntamamiro (Bwana Jela): masharti yapo kwenye sheria ikiwemo PSO.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji naomba asitaje kabisa PSO maana jana haikuwepo na hatukumuuliza. Asiulize. Sect. 156(3) ya Evidence Act iko wazi kuhusu Re- examination.
Jaji: Sasa Wakili wa Serikali Wisdom uko tayari kuendelea na njia hiyo ili tumruhusu Lissu nae aanze kuuliza kwenye PSO.
Wakili wa Serikali Wisdom: Naomba tu niishie hapo. Sitaendelea mbele.
Watu wanacheka ๐๐๐๐
Part 27 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
โผ๏ธHABARI MBAYAโผ๏ธ
Nimepewa taarifa kwamba yule Mwalimu wa UDOM ambae alikamatwa kwa tuhuma za Maandamano ya 7/7 na kushikiriwa kinyume cha sheria.
Baada ya Mahakama kuamuru apewe dhamana, Serikali ya Nduli Idd Amin Mama imembambika kesi ya Ugaidi.๐ฅน
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 25
Wakili wa Waleta maombi Edson Kilatu anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana Jela)
Adv. Kilatu: Ni sahihi ili tujue maduhu ni muongo anasema alifika Ukonga lakini hakufika kumbe ulipaswa kuleta kitabu cha watu wanaohudhuria ukonga wakifika pale getini wanaandika.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi
Adv. Kilatu: Umeleta?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijaleta.
Adv. Kilatu: unakumbuka kuhusu huwa hamsomi nyaraka anazopelekewa Lissu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
Adv. Kilatu: umeleta kiapo chochote cha unaowatuma kusimamia kuwa wanasema hatujawahi kusoma nyaraka za Lissu tukitekeleza majukumu yetu.
Ntamamiro (Bwana Jela): nimeleta mimi kwa niaba yao.
Adv. Kilatu: Lissu alipeleka orodha ya mawakili wa kumtembelea?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi.
Adv. Kilatu: Kuruhusu watu kumuona sio lazima wawepo kwenye orodha?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio kuna mazingira alikuwa anaomba Lissu mwenyewe.
Adv. Kilatu: Umeyasema mazingira hayo kwenye kiapo chako au kuna siku Lissu aliomba mtu ambae hayupo kwenye orodha ili amuapishe aingie.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijasema kwa kiapo changu.
Adv. Kilatu: unajua maana ya retainership ya mawakili kwa mteja uliyoisema kwenye kiapo chako.
Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui ila uliza swali tu.
Adv. Kilatu: Basi tutarudi hapo kama hujui.
Soma paragraph nyingine hapo umesema shauri hili lilipaswa kuwa judicial review sio la kikatiba?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sahihi.
Adv. Kilatu: Una uelewa wowote kuhusu Judicial Review?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Sina uelewa wa hili.
Adv. Kilatu: Basi sitakuuliza kwenye hilo nikuache.
Sasa nenda kwenye originating summons soma ibara za Katiba zilizotajwa humo.
Ntamamiro (Bwana Jela) : zipo ibara ya 13 na zingine.
Adv. Kilatu: Asome ibara ya 30 aielewe halafu nimuulize swali.
Jaji: Asome au ajisomee?
Adv. Kilatu: Ajisomeee mwenyewe aelewe halafu nimuulize swali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Tayari
Adv. Kilatu: Je ibara hiyo inasema mtu anaweza kuja kwa judicial review mahakamani kupitia ibara hiyo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hapana.
Adv. Kilatu: Soma para 4 ya kiapo chako kuwa ulimkataaa Kisabo kwasababu sio wakili wa Lissu?
Ntamamiro (Bwana Jela): lakini baadae lissu alileta ombi maalamu.
Adv. Kilatu: Sasa muambie Jaji hiyo paragraph nyingine uliyosema kulikuwa na ombi maalumu ni paragraph ya ngapi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Haipo.
Adv. Kilatu: Sasa ili wakili aingie gerezani ni lazima kuwepo na orodha ya mawakili iliyoandikwa na mfungwa.
Ntamamiro (Bwana Jela): Utaratibu ni kukagua kitambulisho na kumruhusu.
Adv. Kilatu: Sasa kwenye kiapo chako ukimjibu Maduhu unasema kulikuwa hakuna proof of retainership? Hiyo ndio requirement ya sheria?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nafikiri sifahamu.
Adv. Kilatu. Nimemaliza. Mh. Jaji.
Jaji twende mapumnziko kwa nusu saa.
Tukutane hapa baada ya dakika 30.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 24
Anaendelea John Seka
Seka Anamuongelesha anasema unanisikia au hunisikii. Anatumia sauti ndogo sana. Umenisikia?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nakusikia
John Seka: Pale ofisi ya Admission si kuna Meza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ukubwa wa meza zilizopo hapo admission ukoje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sikumbuki.
John Seka: Katika maisha yako uliwahi kumuona wakili na mteja wake gerezani wanaongea?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Huwa wanakaaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wanakaa kutazamana katikati yake kuna meza?
John Seka: Sasa narudi hapo. Kabla ya kesi hii uliwahi mfahamu Nashon Nkungu, Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nimewahi kukutana nao.
John Seka: Ulikutana nao wapi? Katika mazingira yapi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Akija kuongea na mteja wake gerezani.
John Seka: Ulituambia stage za wakili akifika. Anaandika jina nje, kitabu kinaletwa kwako. Unaruhusu. Sasa tuambie unamuona wakati gani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ofisi zote ni zangu.
Jaji: Jibu ni wapi hapo Gerezani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nilikutana nae Kwa Recha.
John Seka: Kumbe hata Kisabo ulimfahamuje?
Ntamamiro (Bwana jela) : hivyo hivyo kumuona akizungumza na mteja.
John Seka: Umewahi kuwaona wakifanya mahojiano?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Umekumbuka wakati Lissu anafanya mahojiano nani na nani anakuwa ndani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wanakuwa nje wote. Lakini wanachungulia kwa mlangoni.
John Seka: Unakumbuka tarehe ipi na ipi ulikuwepo na ipi haukuwepo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Siwezi kukumbuka.
John Seka: Sasa nitakupitisha tarehe moja hadi nyingine?
Jaji: Amesema hakumbuki nafikiri huko muache acha libaki hivyo.
John Seka: Nitakuwa sahihi nikisema wewe hujawahi hudhuria majadiliano kati ya Lissu na mawakili wake?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Mengi yaliyotokana na hayo wewe hukuwa unahusika moja kwa moja zaidi ya mrejesho.
Ntamamiro (Bwana jela): sio lazima feedback
John Seka: wewe hujawahi hudhuria mazungumzo ya Lissu na wanasheria wake. Huwa unapita tu. Unayoyaona.
Ntamamiro (Bwana jela) : nakagua napita.
Jaji: Hebu sikia kati ya wewe na hao akina Recha, Mumbii anaeweza kuelezea?
Ntamamiro (Bwana jela): Ni sahihi.
John Seka: Sasa tutajie majina yake.
Ntamamiro (Bwana jela): Siwakumbuki.
John Seka: Wakati wote maelekezo yako yalikuwa yanafuatwa ukiwaagiza kwenda kusimamia?
Ntamamiro (Bwana jela) : Mimi ni Mkuu wa Gereza sio lazima niambiwe feedback naweza kujua kwa namna nyingine.
John Seka: Kumbe ulijua kuwa mahojiano na Lissu na mawakili wake yamefuata taratibu kupitia mbinu zako zingine.
Ntamamiro (Bwana jela) : ndio
John Seka: Hao waliokufikishia hizo taarifa au hizo mbinu zako zingine umezielezea kwenye kiapo chako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hapana.
John Seka: Paul Kisabo na Nashon Nkungu. Wakiwa kwenye mahojiano kunakuwa na askari wanakaaa kulia na kushoto kwa Lissu na Kwa Nashon na kisabo nyakati zote.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
John Seka: Ulikuwepo muda wote mahojiano yanapofanyika?
Ntamamiro (Bwana jela) : Napata taarifa kupitia vyanzo yangu.
John Seka: Nimemaliza Majaji. Aendeleee Edson Kilatu.
Anasimama Wakili Edson Kilatu
Adv Kilatu: Ukifika ukonga getini kuna kitabu cha ku register magari?
Ntamamiro (Bwana jela): Sahihi
Adv Kilatu: Anayeshughulikia registration zote sio wewe kwenye vitabu vya kuingia vya magari, raia wa kawaida na kitabu cha mawakili?
Ntamamiro (Bwana jela): Ni sahihi
Adv. Kilatu: Ni sahihi hakuna kiapo cha mtu anayesimamia hizo registration pale Ukonga? Hakijaja hapa mahakamani.
Ntamamiro (Bwana jela) : Hakipo.
Adv. Kilatu: Hii Register book uliyoileta hapa Mahakamani SUPP 1,2,3 ni nyaraka ya magereza hakuna sahihi za mawakili mle. Ni nyaraka yenu tu.
Ntamamiro (Bwana jela): sahihi
Part 25 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 23
Wakili wa waleta maombi John Seka anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Andrew Shaban Ntamamiro (Bwana jela)
John Seka: Moja ya sheria ni sheria ya magereza ambae umeisomea na kuibobea?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Kanuni za magereza je?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nazo ni muhimu sana. Zinatumika.
John Seka: Kwenye kanuni hizo unapaswa kutii kanuni ya 13 ya uendeshaji wa kanuni za Magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ibara ya 29(1) inasemaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Kila mtu anayo haki ya msingi ya kufaidi haki za binadamu kama zilivyofafanuliwa ibara ya 12 hadi 28 ya Katiba hii.
John Seka: Ni nani na nani wana haki ya kufaidi haki mbalimbali?
Ntamamiro (Bwana jela) : Watu wote.
John Seka: Hata wewe?
Ntamamiro (Bwana jela) : hata mimi.
John Seka: Hata Tundu Lissu:
Ntamamiro (Bwana jela) : Hata Lissu.
John Seka: Hata Kisabo?
Ntamamiro (Bwana jela): Hata Kisabo
John Seka: Hata Maduhu na Nashon
Ntamamiro (Bwana jela) : Hata Maduhu
John Seka: Nashon Je?
Ntamamiro (Bwana jela): Hata Nashon.
Watu wanacheka. Wanamuona zamwamwa sijui ๐๐๐
John Seka: Haya rudi ibara ya12 sasa kule.
John Seka: soma ibara 29(2) na useme inasemaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : kila mtu ana haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria.
John Seka: Hadi Lissu akiwa mikononi mwako Ukonga?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sahihi
John Seka: Nenda Kanuni ya 13 ya kanuni za Magereza na utuambie miaka 31 ya uzoefu wako ni lini uliifahamu kanuni hii?
Ntamamiro (Bwana jela) : Tangu nilipoanza Kazi.
John Seka: Isome kwanza.
Ntamamiro (Bwana jela) : mfungwa atapewa haki ya kuongea na wakili wake kwa faragha lakini awe anaonekana lakini sio kuwasikiliza.
John Seka: Umeielewa kweli hicho kifungu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio mfungwa atapewa nafasi ya kuongea na wakili wake na kufanyika kwa kuona lakini sio kusikiliza.
John Seka: Kuna haki ya mfungwa na kuna haki ya mshauri wa kisheria kwenye kanuni hiyo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Haki ya mfungwa kusaidiwa kupewa nafasi ya kuongea na mshauri wake wa kisheria yaani Wakili.
Ntamamiro (Bwana jela): Ndio
John Seka: haki ya pili ni ya mawakili kupata fursa ya kuongea na mfungwa kwa faragha bila ya kusikilizwa ni kutazamwa tu.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Hii haki huwa unasomewa au ni uzoefu? Hii kanuni ya 13.
Ntamamiro (Bwana jela): Sijaelewa swali.
Seka: ili uwe na ujuzi huo wa kutazama bila kusikiliza kuna chuo kinachofundisha? Au ni uzoefu wa kazi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Katika uzoefu wa kazi unasema hapa natazama na sisikilizi.
John Seka: Kwahiyo utekelezaji wa jambo hili unategemea mtu na mtu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hakuna standard zilizowekwa.
John Seka: Kwenye nyaraka zako na maelezo yako ulikuwa unasema simamia? Maana yake ulikuwa unasema simamia lakini wasisikilize.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ukubwa wa Chumba cha Ofisi yako ukoje?
Ntamamiro (Bwana jela) : wakutosha tu.
John Seka: Huwezi kukadiria?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
Jaji: Ofisi yako hujui ina ukubwa gani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wakutosha.
Jaji: Tunatosha wote humu ndani tukija ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hamuwezi kuingia.
Jaji: Bado unasema ni ukubwa wa kutosha?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio
Jaji: Haya jibu swali sasa.
Anasimama Nalindwa Sect. 93 ya Prison Act inasema ramani ya gereza isitolewe. Ukubwa wa hizo ofisi ni hatari.
Jaji Mruma: Hakuna ramani ya gereza wala kifungu hakisemi hivyo. Shahidi jibu swali tunataka sana kujua ukubwa wa ofisi yako ni jambo muhimu sana.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni ofisi iko umbali kutoka hapa nilipo hadi hapo kwako.
John Seka: Sasa ofisi yako ya kaimu wako Recha ni ofisi ya nani kubwa?
Ntamamiro (Bwana jela): Yakwangu ndio kubwa.
Part 24 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Leo July 23, 2026
Jana tuliishia part 21 so leo tunaendelea na-;
Part 22
Majaji wameingia.
Mawakili wapande zote mbili wapo na Mhe. Lissu nae yupo.
Karani anasoma maombi hapa.
Leo tunaendelea na Maswali ya Dodoso kwa Shahidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga ambae Andrew Shabani Ntamamiro (Bwana Jela)
Jaji anauliza kama pande zote ziko tayari. Wanakiri wako tayari.
Jaji sasa na nyie watu wa TLS ninawaruhusu mtapata nafasi ya ku cross.
Anaanza John Seka Wakili wa Waleta maombi.
John Seka : Umekuja kwa niaba ya Gereza la Ukonga
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
John Seka: Una muwakilisha pia kamishna wa magereza Tanzania.
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
John Seka: Unamuwakilisha pia Mwanasheria mkuu wa serikali.
Ntamamiro (Bwana Jela) : ndio
John Seka: Wameona unafaa kabisa kuwawakilisha wewe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
John Seka: Unafahamu Katiba ya Tanzania na haki inazotoa zile za Binadamu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
John Seka: Soma ibara 13 inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Watu wote ni sawa mbele ya sheria
John Seka: Watu hao ni pamoja na Lissu hivi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
Jaji mbona hatumsikii.
John Seka: Afande tumia MIC halafu tumia ile sauti yako ya kijeshi.
John Seka: Jeshi la magereza lina wajibu wa kulinda raia pia?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
John Seka: Jeshi la Magereza ni miongoni mwa vyombo vya serikali vinavyopaswa kulinda haki za binadamu
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Pia haki za mawakili zinatakiwa kulindwa na kuamuliwa?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Msimamizi wa gereza za Ukonga wewe ndio msimamizi mkuu wa haki hizo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Wajibu huo wa Kikatiba umeutekeleza umeutekeleza kipindi chochote ambacho sisi tunakilalamikia hapa mahakamani?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
John Seka: Kifungu cha 13(6)(a) inasema kuhusu haki ya kusikilizwa unafahamu?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio.
John Seka: Kumbe kwa mujibu wa Katiba hii unapaswa kutoa fursa ya kumsikiliza mtu kabla ya kufanya maamuzi?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
John Seka: Wakati unatekeleza majukumu yako, Bwana Tundu Lissu alikuwa na haki ya kusikilizwa kwa ukamilifu?
Ntamamiro (Bwana Jela): Ndio
John Seka: je hawa waleta maombi watatu walikuwa na haki hiyi?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Ibara ya 16 inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Utaratibu wa sheria utawekwa kuhusu hali ya mtu ya faragha na mambo yake ya faragha bila kuathiri sheria.
John Seka: Kwa mujibu wa ibara hiyo mamlaka mbalimbali zinazoweza kuingilia faragha ya mtu kwa kufuata taratibu?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Je mawasiliano binafsi ya mtu ni faragha pia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Wakati wote wakati mtu atamnyima mfungwa haki ya faragha anajua kama anaingilia na kuvunja ibara ya 16?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
John Seka: Je wakati unashugjulika na Tundu Lissu ulijua ibara hii ipo?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Nimetekeleza hilo.
John Seka: Ibara ya 22(1) ya Katiba ya Tanzania inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela): Kila mtu ana haki ya kufanya kazi.
John Seka: Wewe kazi yako unayoifanya ni haki yako?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Kumbe na Mawakili pia wana haki ya kufanya kazi yao vilevile hadi ndani ya Magereza?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Na mawakili hawa walalamikaji kuja ukonga ni kuja kazini kwao pia?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio.
John Seka: Soma ibara ua 26(1) inasemaje?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Kila mtu ana wajibu wa kufuata sheria
John Seka: Kila mtu maana yake hadi wewe? Au wewe haupo kwenye kila mti.
Ntamamiro (Bwana Jela) : Hadi mimi.
John Seka: Una wajibu wa kuheshimu sheria za nchi kumbe?
Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio
Part 23 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
ASANTENI WATANZANIA!
TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 177.8
TUENDELEE KUCHANGIA BARAZA KUU LA UMMA.
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Imagine kama ACT na Vyama vingine vina nguvu kwanini hawajafanya mazungumzo mpaka sasa , hata chauma si chama ila tangu October hawajazungumza .
Ule muungano wa vyama 13 je ? . Nao hola hawawezi kuzungumza na CCM .
Maigizo yanaweza kufanyika kote mpaka kwenye time ya chande ila kwenye meridian hakuna Maigizo .
Keupe katabaki kuwa keupe
Today was a very emotional day. It was good to meet my friend and CHADEMA Chairperson, Tundu Lissu, at the High Court in Dar es Salaam during the hearing of his case. Seeing him in person reminded me that true leadership is often tested in difficult moments. I was grateful for the opportunity to embrace him and show my solidarity. May truth, justice, and the rule of law always prevail.
#TANZANIA: HECHE AMVAA VIKALI MZEE WASIRA, HATUTAFANYA MARIDHIANO YA MAIGIZO
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Julai 22, 2026 akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi ya chama hicho Kanda ya Pwani amesema hawako tayari kufanya maridhiano ya maigizo na wamepewa maagizo na Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu kufanya kazi.
Zaidi: https://t.co/JDaXRPRsUa
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 21
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Ntamamiro (Bwana jela)
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kuwa maafisa Magereza. Wanapaswa kukagua barua inayotoka ndani au kuingia ndio inapaswa kusomwa.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 46 Cha Sheria na kanuni ya 10 na 11 ya kanuni za Magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Anahangaika haoni.
Mhe. Lissu: Sasa wambie majaji kama kanuni ya 10 na 11 inahusu barua wanazoandika na wanazoandikiwa wafungwa.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na wanaosoma ni wewe au maafisa wako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe, Lissu: Ukiikataa barua unamrudishia na kumwambia sababu. Na kama ikikataliwa kwa aliyemletea pia unamrudishia na kumpa sababu. Na kama barua ni ndefu sana na huyapendi ni sahihi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama nje ya barua kwa wafungwa au kutoka kwa wafungwa una mamlaka ya kukagua na kusoma nyaraka nyingine yoyote.
Ntamamiro (Bwana jela) : Naomba soma Section 12 ya Prison Act.
Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizi unaruhusa ya kusoma nyaraka nyingine.
Ntamamiro (Bwana jela) : Soma kifungu cha 12 cha Sheria ya Magereza
Mhe. Lissu: Unauwezo wa kusoma nyaraka za mawakili wanaokuja nazo magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sipaswi kusoma.
Mhe. Lissu: Hicho kifungu cha 12 unachosema kinahusiana na upekuzi wa magari na kumkagua mtu sio nyaraka ndio maana sitaki hata kukisoma. Hakikusaidii chochote.
Mhe. Lissu: Kisabo alisema wakiwaambia muondoke ili azungumze na mimi mteja wake mnakataa. Kweli au sio kweli.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Na mimi nimesema kwenye viapo vyangu kuwa alikuja Wakili Alute Lissu. Na kusema nina ujumbe muhimu kutoka serikali nataka niongee nae Faragha. Mkamkatalia. Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana jela): Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Umekuwa unaendeshwa na rimoti na Kamishna Mkuu na wanasiasa walioko serikalini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kuna siku umeniita ofisini kwako kuwa kuna ujumbe wa jumuiya ya madola napaswa kupelekwa mjini? Kweli au sio kweli?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sina Jibu.
Mhe.Lissu: Siku hiyo aliyekuja kunichukua ni Mangara?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: sio kweli nini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hujawahi kupelekwa.
Mhe. Lissu: Siku nyingine ulinifuata na kusema Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge Duniani amekuja kuniona anaitwa Martin Chungong na nikapelekwe mjini na Senior Mangara.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli
Mhe. Lissu: Kuna siku Heche, Amani na Mnyika uliwaruhusu kutokana na kulikuwa na maelekezo kutoka juu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kabla hujaja walikuwa wanaruhusiwa na ulipokuja ukawazuia hayo mamlaka ulitoa wapi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nimeshajibu.
Jaji: Ulijibuje
Ntamamiro (Bwana jela): Sikuwakataza.
Mhe. Lissu: Alipokuja Lema Godbless, wewe ulipokuja na kutukuta ulimfukuza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
Mhe. Lissu: Kama sio kweli kwanini haya yote hukuyajibu kwa nyaraka wakati mimi nimeyasema kwenye nyaraka zangu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sina jibu.
Mhe. Lissu: Sasa kama umewazuia walalamikaji watatu, mashahidi wangu, umewazuia mawakili wangu. Unanitakia nini kwenye kesi ya uhaini inayonikabili ambayo adhabu yake ni mimi kunyongwa?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nilishajibu.
Jaji Mruma: Umejibu nini?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sijamzuia mtu yeyote kuja kuonana na Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Sina swali lingine.
Majaji wanamuuliza Wakili wa Serikali.
Anasema naomba tuahirishe tuendelee kesho.
Wakili John Seka: Naomba tuendelee bado muda tunao.
Jaji Mruma: Sasa hoja ya kuahirisha na logistics zilivyo, TLS nao kupewa nafasi wamuhoji shahidi. Sisi tunaomba kusema yafuatayo.
Leo tutaahirisha kutokana na sababu kama za jana, tunaamini leo tumefanya kazi kubwa, kesho tutasema mengine.