Bandari yenyewe kwenye picha. Waiting times za meli zimetoka siku 46 hadi 7, mapato yamefika trilioni kwa mwezi. Wageni wakija kuona wenyewe, hadithi za kupikwa hazipati mahali. Hizi siyo ahadi, ni data tunayoiweka wazi.
Banda la “Karibu Tanzania” katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha.
Akiwa katika Banda hilo, Kingi alipata fursa ya kufahamu hatua mbalimbali zilizopigwa na Tanzania katika maendeleo, hususan katika sekta za miundombinu, afya,
@Kilwafinest Mimi sipingi miradi, SGR na Bandari zinaonekana. Ila kuweka 'Democratic Journey' kwenye display ya IPU? Wageni hawaulizwi kwanini hatuchagui hata mwenyekiti wa kitongoji. Bandari: waiting time siku 46 kwenda 7. Data halisi, siyo PROPAGANDA.
Washiriki IPU wajionea miradi ya maendeleo katika Banda la Karibu Tanzania
Wageni mbalimbali wanaoshiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wametembelea Banda la “Karibu Tanzania” jijini Arusha, ambako wamepata fursa ya kufahamu historia ya Tanzania, safari yake ya demokrasia na hatua mbalimbali za maendeleo.
Katika banda hilo, wageni wamepata maelezo kuhusu miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa nchini, pamoja na hatua zilizopigwa katika sekta mbalimbali zikiwemo miundombinu, afya, elimu, uwezeshaji wa wanawake na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
#IPU153Tanzania
@Thommunkondya Karibu sana Mkuu. Point ya Mzee kuhusu Competence ni LAZIMA. Tunaacha wenye uwezo tunaweka ukaribu na uchawa, ndiyo maana mipango haifiki. Na mkulima: bei nzuri ndiyo motisha pekee, pembejeo bure bila soko ni mapambo tu.
Wanaonyesha wageni 'TANZANIA'S DEMOCRATIC JOURNEY' kwenye slideshow, ila hapa nyumbani hata mwenyekiti wa kijiji hachaguliwi huru. IPU ikiisha, katiba mpya ipo wapi?
Spika wa Maldives atembelea Banda la Karibu Tanzania
Spika wa Bunge la Maldives, Abdul Raheem Abdulla, ni miongoni mwa wageni waliotembelea Banda la “Karibu Tanzania” katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha.
Akiwa katika banda hilo, Mhe. Abdulla amepata fursa ya kufahamu safari ya Tanzania katika demokrasia na maendeleo, huku akieleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), Bwawa la Julius Nyerere, Daraja la Busisi (Magufuli), uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, pamoja na miundombinu inayoandaliwa kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
#IPU153Tanzania
@mariam255_ Hii ni nzuri. Ila tukutane kuzungumza AJIRA, skills na ufumbuzi halisi, siyo chakula na picha tu. Vijana 800,000 wanaingia sokoni kila mwaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Tedros Ghebreyesus, ameshiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaoendelea jijini Arusha. Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 2,000 kutoka mataifa 184 duniani.
#IPU153Tanzania
@Aduiwayanga Maono ya umeme kutimia? Vijijini umeme ni 4%. Tunatuma nishati Malawi na Kenya ilhali vijiji vya Mtwara na Kigoma vina giza. No wonder, takwimu za kufurahisha genge ndiyo kazi kuu.
@imaaJr01 Kuuza umeme kwa Malawi ni hatua nzuri. Ila kwanza hapa nyumbani: vijijini umeme ni 4% tu. Solar ya 2GW iliyosainiwa na wawekezaji wa Dubai ndiyo itabadilisha hilo. No country can industrialize in the dark.
@imaaJr01 Kushirikiana ni sawa, ila cooperation yenye tija ndiyo muhimu. Bandari yetu, ship waiting times zikishuka kutoka siku 46 hadi 7, throughput imeongezeka mara mbili. Hapo ndipo unapojua partnership ya kweli inafanyaje kazi.
@Deviant_Space Kwa maoni yangu hii ni stori ya kubembeleza tu. Mtaani huoni IPU wala tuzo, mtaani unaona Polisi, TISS na vijana wanaotekwa bila jibu. Mfano wa kuigwa kwa nani hasa?
@bbcswahili Anatishia kufunga Horomuz, dunia nzima inalipa, halafu anajionea mwathirika. Hili ni DHAHA. Mkulima wa Dodoma analipa bei ya mbolea kwa sababu yake. Nchi hii inataka njia iko wazi, mafuta zishuke bei.
Amani na utulivu huo wenyewee. Wajumbe wa IPU hawajui kwamba mtu hawezi kusimama Arusha akapige konde bila TISS kumsikiliza. Maandamano hayaendelei kwa sababu yameZUIWA, halafu wanawacheka kuwa wamehangaiwa 😅
MKUTANO WA IPU NI KIELELEZO CHA AMANI NA UTULIVU ULIOPO TANZANIA
JANA tumeshuhudia mkutano mkubwa sana wa 153 mabunge duniani ukizinduliwa na Mhe Dokta Rais Samia pia Waziri Mkuu Dokta Mwigulu kwa nyakati tofauti.
MKUTANO huu umeleta pamoja mamia ya wajumbe kutoka dunia nzima kwa ajili ya siku 4-5 kuhudhuria mkutano huu muhimu sana na uliosheheni watu kutoka mataifa mbalimbali.
NIMEJIULIZA maswali mengi sana ya msingi kuhusu mkutano huu kufanyika Tanzania ikiwemo Je? Kama Tanzania kungekuwa hakuna amani na utulivu huu mkutano ungefanyika? Kama Tanzania ingekuwa inatazamwa vile wanaharakati wanaitazama Tanzania huu mkutano ungefanyika kweli?
Sektretarieti ya IPU ilikuwa na options nyingi sana za kuhamisha mkutano huu kama Tanzania ingekuwa siyo nchi yenye amani. Kulikuwa na uwezekano wa kupeleka mkutano huu kweingineko duniani lakini kwa kuwa walijiridhisha na hali ya Tanzania na uimara wa serikali hii wakaamua mkutano huu uendelee kufanyika Tanzania pamoja na porojo za wanaharakati huku na kule.
NILISIKIA wendawazimu hawa wanaojiita wanaharakati wakipayuka payuka kuwa wanataka kufanya maandamano wakati wa mkutano wa IPU huko Arusha . Nataka kujua wamefikia wapi na maandalizi ya maandamano yao! Au walishaandamana mimi ndiyo sijui kama waliandamana yaani.
KUFANYIKA kwa mkutano huu ni kielelezo kuwa Tanzania i kubwa kuliko harakati uchwara zinazofanywa na watu waliolaaniwa na kukosa muelekeo wa maisha yao kama akina Maria wanaotaka kila siku Tanzania iwe kwenye shida na matatizo.
WAMEHANGAIKA sana kuichafua Tanzania huko duniani. Wamehangaika sana kuhakikisha Tanzania inapakazwa tope kwelikweli na inachafuka lakini badala yake sasa ndiyo imekuwa kinyume na Tanzania inang'aa kwelikweli..
NAWAKUMBUSHA tu kuwa hakuna maandamano mtakuja kufanya tena kwenye nchi hii yakafanyika! Kama mnabisha niambieni yale makelele yenu ya kuwa mnaandamano kuzuia mkutanao wa IPU yameishia wapi au mtaandamana siku mkutano ukiwa umeisha?
#KigogoMediaUpdates
Jump cuts kumi kwa dakika moja halafu mnaiita hii broadcast rasmi? Mkutano wa kimataifa ukija Arusha, Rais anabaki screen. Hii ni stadi za ukumbi wa michezo.
Angalia hili takataka! Hivi hili jitu liko sawa kichwani kweli?
Aisee mbona linaandika mambo ya kijinga hivi? Hizi harakati tuliwaambia mtahangaika sana hamkuwa mnasikia haya sasa ona mnavyohangaika yaani
Hivi kuna ugumu gani kulima au hata kufungua kibanda cha kuuza uji wa ulezi na chapati kuliko huu ujinga unaofanya na unaita ni kazi?
@MwanzoTvPlus KIUT, Raiyan, na wengine wasioandikwa gazetini. Kesho story itakuwa ukurasa wa tatu, kisha tuliamka maisha ya kawaida. Hakuna anayewajibika. Hii ni FAILURE ya mfumo wa usalama, si bahati mbaya.
Mkutano mzuri. Swali ni moja tu: kama amani ni ya kweli, kwa nini kila mtu anayezungumza CHALLENGES anaitwa muhalifu? Amani ya ku-host mikutano ni rahisi. Amani ya kusikiliza wananchi ndio ngumu.
Dunia yote iko Tanzania kubadilishana mitazamo na kuandaa maazimio kuhusu masuala yanayogusa dunia nzima.
Wanashudia Tanzania iliyojaa Amani na utulivu;Wanaharakati mnalakujifunza, wanaowatumia kuchafua nchi yenu leo wako hapa na wanaisifia nchi hiyo hiyo wanaowatuma kuichafua
"Watanganyika msikubali maridhiano baada ya uchaguzi,Ni laana" -@-Balozi humphrey polepole.
Bado tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu Kaka Humphrey polepole.Hatujakusahau.
Leo umetimia mwaka mmoja tangu madhulmati
Yakuteke na kukuficha kusikojulikana.
#FreeHumphreyPolepole
@Mwamba_hi Hii ni PR ya kidiplomasia. Ndani ya nchi dialogue inaitwa UGAIDI. Mwulize Mkunda, mwulize Lissu kama dialogue ipo. Tumeshindwa hata kuchagua leader wa kitongoji, sasa tunafundisha dunia demokrasia? 😅
@Deviant_Space Accountability to wananchi? Sema tu. Mimi nasubiri Bunge lifuatilie ripoti za CAG hadi mwisho, mtumishi aulizwe, atakaye. Mpaka sasa hakuna. Bunge bila nguvu ya kuwajibisha ni karamu tu yenye mada.