Magic Builders Pamoja na mafundi ujenzi, tunaishukuru Serikali,chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluh Hassan, Kupitia Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, Kwa kutambua mchango wa Kundi la mafundi Ujenzi, katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara ya 2025/2026.
Binafsi naamini viongozi wa CCM hawana ubongo unaofanya kazi. Najaribu kufikiri tu kama viongozi wapo hivyo, ni vipi wanachama na wafuasi wa CCM?
Hii ilikuwa ni Mei 2033, Daniel Chongolo akiwa na William Lukuvi na wazandiki wengine wakaenda kufanya ulaghai kwa wanachama wao wa CCM huko Isimani, Iringa.
Hiki ni kijiji cha Kitisi, kata ya Mapogolo, tarafa ya Idodi. Hapa hakuna hata maji. Lakini MaCCM wasivyokuwa na huruma wanafunga safari kwenda kulaghai wananchi.
William Lukuvi amekuwa mbunge wa jimbo la Isimani tangu November 1995. Hadi leo ni miaka 29. Bado anabeba wazandiki wenzake kwenda Idodi kuwadanganya wananchi.
Binafsi sina tatizo na mzungumzaji au Lukuvi au Chongolo waliopo katika huo mkutano. Tatizo ni hao wanaoshangilia na kupiga makofi, ni watu wenye ubongo wa binadamu?
Kwamba kadi ya CCM unaweza kutumia kama bima ya afya na ATM kutoa fedha benki? Na wananchi maskini wakashangilia kwa vifijo na nderemo kwa utapeli huo?
CCM wanawadharau sana watanzania. Sasa ni mwaka mmoja umepita, hakuna kitu wamepata. Waliambiwa watapata hizo kadi kabla ya kufika August 2023. UTAPELI.