โผ๏ธREAD LETTER FROM TUNDU LISSUโผ๏ธ
Received from Ukonga Prison - from @TunduALissu
Barua rasmi ya Lissu kwetu sote! Alituma kwa Kiingereza neno kwa neno kupitia mtu aliyenifikishia na nimeweka hapa chini ๐๐พ tafsiri isiyo rasmi
Nalaani vikali shambulio dhidi ya Padre Dk. Charles Kitima na kushambuliwa kwa kipigo kikali na kutekwa kwa Mdude Nyagali. Rais Samia na Serikali yake wanahusika na vitendo hivi viovu vya kigaidi. Natoa wito kwa Rais Samia na serikali yake kuhakikisha kuwa Mdude Nyagali anaachiwa mara moja na anapata huduma ya dharura ya matibabu anayohitaji.
Kwa Padre Kitima, namtakia ahueni ya haraka na kumsihi yeye na Maaskofu wa Tanzania kudumisha misimamo yao thabiti na yenye misingi mikuu katika mapambano ya kudai Tanzania ya haki, usawa na demokrasia.
Kwa viongozi wa CHADEMA, wanachama, wapenzi, na wananchi wa Tanzania kwa ujumla, nawaomba kutokata tamaa wala kukatishwa tamaa katika kupigania demokrasia ya nchi yetu. Ninataka wajue kwamba nipo thabiti kabisa na siyumbishwi, na hakuna kuta za gereza zitavunja roho yangu. Ninawapenda wote, na nitarudi.
P.S. Nisipopelekwa kortini Jumanne kama inavyostahili, nitaanza mgomo wa kula."
Tundu Antiphas Mughwai Lissu.
(Gereza la Ukonga).
@John_Pambalu All the best CDM. Nyie ni chama cha upinzani msikubali kuishi kama chama tawala...Mbowe na Lissu wakae pamoja waamue FATE ya chama.
Punguzeni kuhongeka
@tanescoyetutz@tanescoyetutz Hivi kwa nini emergency response za Mikocheni na Mbezi Beach ziko very poor ? Those people are arrogant, and they really don't care.
They can take up to 2 days to attend a ticket!! You guys must improve for sure ,your KPI is getting worse day by day.