NINAWASHUKURU sana wote mlionitumia salamu za pongezi. Hadi naogopa sasa. Lakini yote kwa yote nawashukuru sana, sana. Tuishi na tufurahie kuona wengine wakiishi. Mbarikiwe.
Uchokozi huu ulianzia kwa @bwaya akaupokea kuhani wetu @MayengoDr na sasa unaelekea kwa @Ufafanuzi na @mathewmndeme
Hapa kazi inazidi kuwa ngumu ๐คฃ lakini tuta-revenge tu.
Pindi utakapoelewa nguvu ya maneno yako, hutazungumza kila unachofikiria.
Pindi utakapoelewa nguvu ya fikra zako, hutawaza kila kitu kinachokuja akilini.
Pindi utakapoelewa nguvu ya uwepo wako, hutapatikana kila mahali.
Tambua Thamani Yako
Mahusiano yanayokua polepole,
Mahusiano yasiyoanza na โmlipukoโ wa mapenzi,
Mahusiano yasiyoharakisha ngono,
Huwa na uwezekano mkubwa wa kudumu.
Wapenzi wanaojipa muda kufahamiana,
Wapenzi wasioharakisha โkuaminianaโ,
Wana uwezekano mkubwa wa kuoana, kuridhika na kudumu zaidi katika ndoa.
Haraka haraka, tafiti zinasema, huleta kuteleza.
Haraka haraka hunyima umakini,
Haraka haraka kuleta kizaa zaa.
Tunagombanishwa na tafsiri za mapenzi. Unachoamini ni mapenzi kwa mwenzako kinaweza kuwa kitu kingine na kikachokoza matatizo. Kuna mtu mapenzi ni kukumbushwa furaha ya utotoni. Mwingine mapenzi ni kusahaulishwa huzuni ya utotoni. Kuna mtu humpenda mpenzi anayefukia hasira zake za migogoro ya utotoni. Mwingine humpenda anayemhakikishia usalama aloukosa utotoni.
Mwingine humpenda anayeziba ombwe la uhuru. Kwake kumfuatilia, kuingilia faragha yake ni wivu sio mapenzi. Mwingine mapenzi ni kupata mtu wa kutosha kuziba ombwe la kukosa mamlaka na sauti ya kumuelekeza. Unachokiona ni โutumwaโ na kukosa faragha kwako hayo ndio mapenzi na unapompa uhuru maana yake hujali.
Mwingine ukimfanya asikike na aeleweke anaona unamthamini. Kazoea ukaribu, kueleweka na mazungumzo ya wazi yasiyoacha makisio. Usiposema wazi unataka nini anakuona โtoxicโ. Mwingine ukimfanya asikike na aeleweke anakuchoka. Kwake mapenzi ni drama za kuviziana. Hasemi anachotaka. Anakulaumu kwa asichosema. Ukimpenda basi ujifunze kujua anataka nini bila kuambiwa. Usipojua asichokuambia humpendi.
Migogoro yetu mingi ni kutumia tafsiri zetu binafsi kwa wenzetu. Tunafikiri tunachokitaka sisi ndicho wanachokitaka wenzetu. Mapenzi, kwa hakika, ni kuelewa na kuiheshimu tafsiri ya mapenzi kwa mwenzako. Tunapofanya hivyo, mapenzi yanakuwa fursa ya kujifunza mengi yanayotibu makovu tulowahi kupitia.
Kizazi cha upweke, kinachotafuta kupendwa lakini kikichochoshwa na upendoโmatokeo halisi ya utoto uliotelekezwa (deprived childhood).
#Ushunuzi via @MwananchiNews
Kama mwanaume, ni jukumu lako kujituma kwa bidii kupata unachotaka. Elewa kwamba hakuna mtu anayekuja kukuokoa. Hakuna kitakachotokea kwa wale wasiokusaidia.