Meneja Habari na Mawasiliano @AliKamwe akiendesha semina kwa mabondia jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kutengeneza thamani zao.
Mabondia hao watakaoshiriki kwenye Dar Boxing Derby itakayofanyika June 29, mwezi huu walitembelea Makao Makuu ya Klabu yetu, Jangwani Dar Es Salaam, waliongozana na Promota Meja Selemani Semunyu🔰
#timuyawananchi
#daimambelenyumamwiko
Binafsi sioni kosa la Mashabiki wa Yanga kumzomea Maestro Feisal Salum jana na bado sioni kosa kwa Feisal kuweka penati kambani na kuwanyamazisha Mashabiki jana, huo ndio mpira wa miguu tangu zama hizo yani una raha na karaha, jeuri na ubabe wake.
Kinachoendelea naona kuna chuki ya KULAZIMISHWA kutoka nje ya Feisal na Yanga inajaribu kujengwa kati ya FEISAL na YANGA, sioni kama kiuhalisia Yanga wana chuki yoyote na Maestro! Umewahi kusikia sehemu wamempiga huko mtaani? Umewahi kusikia wamemfanya kitu kibaya huko mtaani? Jibu ni HAPANA.
Brothers and Sisters mpira wa miguu huu ndio utamu wake, watu ni vichaa haswa! Nadhani tulipaswa kuwapongeza sana Mashabiki wa Yanga na Yanga kiujumla kama taasisi lakini pia Maestro Feisal, wote wawili wamekubali yameisha kati yao na kila mmoja anaendelea na maisha yake, ulisikia katupiwa kopo la maji ama kupigwa jana? Jibu ni HAPANA.
Mwisho wa siku hakuna aliyepoteza kati yao! Yanga ameendelea kuzoa medali kama kawaida yake na Feisal ameendelea kuwa kwenye ubora wa juu kama kawaida yake, mwisho wa siku ni vita ya kimalengo na kila mmoja anashinda mechi zake tena vizuri sana, nani kapoteza kati ya Feisal na Yanga? Hilo majibu mimi sina na yako baki nayo.
Karejeeni vyema kwenye mkasa wa Luis Figo pale Netflix inaitwa Casa del Figo, ndipo utaelewa ukatili na uadui kwenye mpira baada ya yeye kuondoka Barcelona na kujiunga na Madrid, ila Feisal na Yanga ni upendo kati yao uliojificha katika chuki wala hawana tatizo hawa ila kuna namna watu wanalazimisha.
For the good of the game! Mwisho wa siku career ya Maestro Feisal itahukumiwa kwa makombe na tuzo binafsi, hivyo ndivyo Wachezaji wakubwa hupimwa! Kila la heri kwa Yanga na kwa Maestro Feisal Salum, a match made in heaven, mnapendana sana, si ajabu siku Feisal akarudi Jangwani na watamshangilia ndio Football😀
VISIT MOROGORO🇹🇿
Djigui Diarra ni Golikipa wa viwango vya juu sana, kabla ya penati kupigwa rudia mechi utaona aliwafuata Wachezaji wote wakiwa kwenye mstari na kuwaambia “Tumieni sana akili” alisisitiza kama mara mbili kuwa mikwaju inataka akili na utulivu, alirudia sana kwakuwa huwa wanampa sana kazi na anawajua vizuri.
Rejea tena video hata wakati Stephen Aziz Ki anaenda kupiga penati, ni kama Wachezaji walikuwa wamesimama tu, akasimama yeye na kuwaita kwa nguvu kuwa wanaanza wao kupiga penati ndipo Aziz Ki akaenda.
Rejea mechi ukipata muda kama sikosei penati ya tatu aligundua kuwa Kipa wa Azam ana mind game za hatari sana kwa wapigaji wake, akawa anasimama mbele kama anapiga yeye mpaka Mchezaji wake akisogea ndipo anatoka.
Mwisho rejea mechi ukipenda hii ya Azam ama ya Champions League dhidi ya Mamelodi Sundowns! Nadhani ndio Kipa pekee ambaye hatoki kwenye mstari kabla ya movement ya mpira, nadhani ni mafundisho makubwa aliyopata, hajawa nyanda kwa bahati mbaya, hata Kipa wa Azam nae alikuwa vizuri kwenye hilo kutotoka kwenye mstari kama wengine wengi.
Wengi hamkumzingatia kabisa, ila amefanya kazi kubwa sana kuituliza timu yake, amefanya kazi kubwa mno Diarra.
DIARRA WHAT A GOALIE.