@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
MaCCM yana wakati mgumu sana kuliko yanavyofikiria, yamechafua roho za watu kila kona
yanafikiria yanaweza ua na kuteka kila anayeyaambia ukweli
Huko mbele kuwa CCM inaweza kuja na gharama kubwa sana, watatafuta Wanaharakati na CHADEMA kuongea na wananchi, ambapo itakuwa too late
Viongozi wa CHADEMA, hizi mambo za ku-sympathize na watu waliosaliti na kutuumiza halafu wanarudi mnawalamba masikio, this time Lissu akiwa gerezani, aisee mnatukosea sana sisi wananchi. Mnatuona sisi ni mazuzu kama CCM wanavyotuona sio? Mmeshaona mnatumudu watanzania eeh! Okay.
Leo, tarehe 07 Juni 2026, Kamati Maalum ya CHADEMA Zanzibar imeketi katika kikao chake kilichofanyika Kisiwani Pemba. Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Mhe. Said Mzee Said, na kuhudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika.
Kikao hicho kinajikita katika kujadili hali ya siasa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla, kwa lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa kisiasa na kuweka mwelekeo wa hatua za chama katika kipindi kijacho.
Aidha, kikao hicho kinajadili na kupitisha Mpango Mkakati wa CHADEMA Zanzibar wa miaka mitano, utakaokuwa mwongozo wa utekelezaji wa shughuli, sera na vipaumbele vya chama kwa kipindi husika.