"Chimbuko la matatizo haya ni uchaguzi na watu wanaotaka kubaki madarakani kwa njia ambazo si za kikatiba, tusipotatua hilo nchi hii itazalisha wakimbizi." Mhe. @HecheJohn
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 293
Katuga: Tuahirishe kidogo kutoka kwenye D4 hivyo vielelezo tuhamie eneo lingine. Ulisema hawajaleta video kwahiyo wameshindwa kuthibitisha mashitaka yao wenyewe ulisema hivyo?
Mhe. Lissu: Ndio.
Katuga: Wakati unayasema hayo ulikuwa unayajua mashitaka yanayokukabili?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: Ulikuwa umeyaelewa?
Mhe. Lissu: Sana tu.
Katuga: Mashitaka unayokabiliana nayo kuna sehemu yoyote inayosema unashitakiwa kwa kuchapisha video?
Mhe. Lissu: nachapisha maneno kwenye video iliyosambazwa na jambo Tv.
Katuga: Kwa mujibu wa ushahidi video kiushahidi ina kitu ambacho unaona na kusikia?
Mhe. Lissu: Sawa.
Katuga: Maneno yanaonwa au yanasikiwa?
Mhe. Lissu: Maneno yanasikiwa na kuonwa kwenye kesi hii. Kwa mujibu wa sheria ya ushahidi kitu chakuonwa kinaonwa na chakusikiwa kinasikiwa.
Katuga: Kwenye hiyo video maneno unaona au unasikia?
Mhe. Lissu: Iko wapi sasa hiyo video. Ninayo hapa??
Katuga: Kwahiyo walichokileta ndio walichokisia?
Mhe. Lissu: Huwezi kutenganisha video na maneno. Kivipi sasa? Maneno yapo kwenye video.
Katuga: Kila shahidi anapaswa kuaminiwa?
Mhe. Lissu: Washahidi wa kweli ndio huaminiwa. Waongo hawaaminiwi.
Katuga: Je katika mashahidi wa Jamhuri ni kifungu gani cha Sheria kinasema lazima ulete video ndio tuseme maneno yalisemwa?
Mhe. Lissu: Hiyo ni common sense tu.
Katuga: Akija shahidi akasema niliona radi imepiga na kuua watoto lazima alete video ndio tumuamini?
Mhe. Lissu: Sasa radi na video vinahusiana. Video ilirekodiwa. Sasa radi nani ameruhusu itokeee hadi useme irekodiwe.
Katuga: kama video ikifutwa mtu aliyeona hawezi kutoa ushahidi na kuthibitisha?
Mhe. Lissu: Unakuja kuthibitisha video ipi sasa wakati huna?
Katuga: Kati ya maneno au video ameleta nini?
Mhe. Lissu: Hajaleta chochote. Maneno ya kwenye video yapo kwenye video. Hayawezi kutenganishwa.
Katuga: PW17 alikuwepo Live kwenye Mkutano wako na alisema anayoyakumbuka kwamba mtazuia uchaguzi.
Mhe. Lissu: Hakusema hivyo.
Katuga: Shahidi aliyekuwepo eneo la tukio PW17 ni lazima alete video?
Mhe. Lissu: Ni lazima kwasababu aliyaleta mambo ya video mwenyewe inabidi iwepo.
Katuga: PW 17 kuna mahali alisema alikuwa anaiona na kuisikia?
Mhe. Lissu: Alikuwa anarusha matangazo live sasa atarushaje bila kuiangalia?
Katuga: Mashahidi mapolisi hawaaminiki kwasababu waliandika maelezo yao wenyewe?
Mhe. Lissu: Hawaaminiki kwasababu hawakufuata taratibu za kuandika maelezo.
Katuga: Kila shahidi anaaminika
Mhe. Lissu: Anaaminika shahidi kwasababu ya ushahidi wake sio sura yake.
Katuga: Mimi sina nia mbaya.
Mhe. Lissu: Umenishtaki kwa uhaini halafu uwe hauna nia mbaya.
Katuga: Kifungu gani cha Sheria kinakataza Mapolisi kutoa ushahidi
Mhe. Lissu: Mashahidi ambao hawakufuata utaratibu ndio ushahidi wao hauwezi kuchukuliwa kwa uzito wowote.
Part 294 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 295
Katuga: Naomba niishie hapa nisiulize maswali mengine niishie hapa. Niwaachie wenzangu.
Anasimama Job Mrema. Nae kuuliza maswali.
Job Mrema: wewe ni mwanaharakati ulisema?
Mhe. Lissu: Ndio
Job: Ulianza lini?
Mhe. Lissu: Nilisema habari za nilipokuwa sekondari, jeshini na kadhalika nilielezea.
Job: Uwanaharakati ni nini?
Mhe. Lissu: Uanaharakati ni mtu anayefanya jitihada za kupigania jambo au mambo fulani.
Job: Wewe pia ni mwanasheria?
Mhe. Lissu: Ndio
Job: Huu uanaharakati unatambulika kwa mujibu wa sheria za nchi?
Mhe. Lissu: Ndio
Job: kifungu gani?
Mhe. Lissu: Kuanzia ibara ya 12 hadi 29 ya Katiba vinatoa uwanja mpana wa kufanya jitihada za kupigania mambo mbalimbali.
Job: sasa ibara ya ngapi imesema harakati ni nini?
Mhe. Lissu: Hujielewi wewe. Nimeshakwambia hizo ibara zinasema watu ni huru, ukipigania uhuru wa watu maana yake unafanya harakati. Katiba inasema haki ya Uhai na kuishi ukipigania kupinga adhabu ya kifo maana yake unafanya harakati za kupigania haki ya kuishi.
Huyu Job Mrema yeye huwa ni kilaza wa aina yake.
Job Mrema: Ni sahihi maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka na walioyasikia waliyatafsiri kadri yalivyo?
Mhe. Lissu: Hawakutafsiri kadri yalivyo.
Job Mrema: Hakuna mahali popote kwa sheria za nchi hairuhusiwi watu kujichukulia sheria mkononi?
Mhe. Lissu: Hakuna sheria inayoruhusu watu kuvunja sheria. Kuhusu Sheria za Uchaguzi nasema kwamba uchaguzi usio huru na haki basi ni haki yao wananchi kuuzuia.
Job: Ukiwa mwanaharakati una kinga ya kufuata sheria?
Mhe. Lissu: Nilishajibu hauna kinga. Kama huna maswali ukakae.
Job: Ukiwa mwanasiasa je?
Mhe. Lissu: Huna kinga.
Job: Ulisema kesi hii ya kisiasa. Je wewe umeshitakiwa kama Tundu Lissu au mwanasiasa.
Mhe. Lissu: Nimeshitakiwa kama Tundu Lissu ambae ni mwanasiasa. Nisingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA nisingekuwa hapa.
Job Mrema: Kwa mujibu wa hati ya mashitaka kuna mahali wamesema wewe ni mwanasiasa?
Mhe. Lissu: Mashahidi wote wanasema mimi ni Mwenyekiti wa CHADEMA. PH imesema mimi ni Mwenyekiti wa Chadema. Kwahiyo hati haisemi lakini huko kwingine kote ni Mwenyekiti wa Chadema.
Job Mrema: Ulisema umewahi kushitakiwa na ushahidi uliotoa hapa hujaeleza ulishitakiwa kwa kesi gani? Kesi namba ngapi ya Mahakama gani?
Mhe. Lissu: Nilielezea taarifa zakutosha kuhusu kesi hizo mahakama inajua.
Job: Ulisema huwezi kuwa Rais wa TLS halafu ukawa mtu wa hovyohovyo?
Mhe. Lissu: Hilo nilijibu zamani sana. Nilitumikia hiyo nafasi miezi mitano nikapigwa risasi.
Job: Ni sahihi ukitoka kuwa Rais wa TLS unaweza kuwa mtu wa hovyo hovyo?
Mhe. Lissu: Huyu sio mtu wa hovyohovyo. Na nina heshima zakutosha huko Duniani
Job: Umewahi kulalamika kokote kuhusu risasi ulizopigwa?
Mhe. Lissu: Anasimama sasa. Nimelalamika sana. Na wamekataa kuandika maelezo toka nikiwa hospitali Nairobi. Hawajawahi kuandika.
Job Mrema: Umejinasibu kama Mwanasheria
Mhe. Lissu: Kwani wewe hujui kama mimi ni mwanasheria? Utanifananisha na wewe?
Job Mrema: Kifungu cha 10(1) (2)cha CPA. Kinasemaje
Mhe. Lissu: Anakisoma kinahusu kuandikwa kwa maelezo.
Job Mrema: Unakielewaje?
Mhe. Lissu: Taarifa za kosa zinatolewa kwa maandishi au mdomo kwa afisa husika kwenye eneo husika.
Job Mrema: Ulikwenda kutoa taarifa?
Mhe. Lissu: Sikwenda kwasababu nilikuwa nusu mfu. Ulitaka niende lini? Nisingeweza kutoa hayo maelezo nilikuwa napigania uhai wangu.
Job Mrema: Jinai inakufa?
Mhe. Lissu: Ndio maana nilivyorudi nilienda kwa RPC Mroto Dodoma. Nikamwambia mlikuwa mnasema sikuwepo sasa nimerudi haya nihojini sasa kuhusu haya mambo. Hawakuwahi kunihoji kokote.
Job Mrema: Unapopata taarifa ya vitisho ni sahihi upeleke polisi hizo taarifa?
Mhe. Lissu: Ni sahihi kama hivyo vitisho havitoki kwa polisi wenyewe. Kama wanakutisha polisi unaenda tena polisi kutoa taarifa hizo kuwa wanakutisha. Utakuwa mwehu sio bure.
Watu wanacheka 😂😂
Part 296 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 292
Katuga: Naomba twende kwenye D3 Lissu anasema ngoja nitafute. Ametafuta kwa muda mrefu ameipata sasa.
Katuga: D3 kielelezo alisema ananunua Ilala Boma Sokoni. Hiyo ni omission au contradiction?
Mhe. Lissu: Ni omission na ni contradiction pia.
Katuga: maneno kwamba hayamo kwenye maelezo yake kwa mujibu wa jibu hili yanakanganyana na nini?
Mhe. Lissu: Yanakanganyana na kariakoo na Posta Mpya. Wakati huku amesema Ilala Boma.
Katuga: Swali kwa PW4 kwamba alikuwa na smartphone sony Galaxy yapo au hayamo kwenye kielelezo. Alisema hayamo.
Mhe. Lissu: Ndio. Na ni Omission.
Katuga: Kuhusu kuwa na account facebook hajaandika kwenye maelezo? Unasemaje.?
Mhe. Lissu: Hakuandika ni Omission.
Katuga: Alisema amemuona Tundu Lissu kuhusu na hiyo ni Contradiction au Omission?
Mhe. Lissu: Ni Omission
Katuga: huku alisema mzozo huku amesema mabishano. Kwani utofauti ni nini?
Mhe. Lissu: Mzozo ina element za ugomvi hakuna ustaarabu mabishano ni kutofautiana mawazo. Hata marafiki wanabishana.
Wameomba break ya dakika kumi
Part 293 itaendelea baada ya break.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 291
Katuga: Kutokulipiwa na matibabu na umeeleza vitu vingi kuhusu uchaguzi. Imani yako uliposema imani yako na mahakama haipo kwahiyo huna imani?
Mhe. Lissu: Hilo ni la kuuliza kweli. Kwenye maswala haya sina IMANI KABISA NA MAHAKAMA.
Katuga: Maswala yapi?
Mhe. Lissu: Si ya Uchaguzi tunazungumzia.
Katuga: Kwahiyo hukupanga kuiomba Mahakama kutengua vifungu fulani vya Katiba?
Mhe. Lissu: Sikupanga.
Katuga: Uliamua kutafuta njia nyingine mbadala?
Mhe. Lissu: Njia ya mbadala ya Kidemokrasia.
Katuga: Jana nilikuulizia kuzuia uchaguzi ni njia ya kidemokrasia.
Mhe. Lissu: Haswaa.
Katuga: Kukinukisha ni njia ya kidemokrasia?
Mhe. Lissu: Haswaa ni njia ya kidemokrasia.
Katuga: Kuhamasisha uasi je?
Mhe. Lissu: Njia ya kidemokrasia kabisa. Mwalimu Nyerere alisema uasi dhidi ya mifumo kandamizi ni halali kabisa.
Katuga: Kifungu cha 52 cha Media Service Act iko sawa na kifungu cha 55?
Mhe. Lissu: Iko sawa.
Katuga: Sheria ya Huduma za Habari iliundwa ku regulate huduma ya habari?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: Kuzuia uchaguzi uliopo kwa mujibu wa sheria ni kuipinga serikali?
Mhe. Lissu: ni kuzuia uchaguzi. Kuipingaje tena serikali?
Katuga: Kuhamasisha uasi, kukinukisha. Ni kuipinga serikali au kuipindua serikali.
Mhe: Lissu: Hatukuwa tunazungumza habari za serikali.
Katuga: Mbona nakuuliza swali kwa heshima tu
Mhe. Lissu: Huna heshima hata kidogo. Uitoe wapi?
Katuga: Unakumbuka ulisema kuipinga serikali sio kosa?
Mhe. Lissu: Nimesema.
Katuga: Sasa ulikuwa unamaanisha nini?
Mhe. Lissu: Nassoro Katuga nimesema kifungu cha 55 hakijasema serikali peke yake
Katuga: Mimi mdogo ndio maana unanionea.
Mhe. Lissu: Wewe mdogo ungekuwa hapa? Una udogo gani wakili mkuu wa serikali?
Katuga: Ulisema mapolisi kujiandika maelezo ni kinyume cha sheria na je uliwatajia sheria.
Mhe. Lissu: Sikuwaambia lakini kifungu kipo na kinajulikana.
Katuga: Sasa mbona unaniambia sina adabu halafu wewe hujibu maswali.
Mhe. Lissu: Unataka niseme yakwako?
Katuga: Ulisema vielelezo vilivyoingia mahakamani uliviingiza wewe?
Mhe. Lissu: Viliingizwa na Mahakama.
Katuga: Kwahiyo umeridhika na content za hivyo vielelezo?
Mhe. Lissu: nimeridhika vitumike kuonesha sina hatia.
Katuga: Naomba D1 hadi D16.
WANAMTAFUTIA WAMPATIE VIELELEZO.
Katuga: Unakumbuka D1 ni kielelezo cha Kaaya ambae ni PW2 na uliomba yatumike kwa nia ya kudodosa shahidi kwa mujibu wa kifungu cha 163?
Mhe. Lissu: Kweli
Katuga: ni kweli tulisema kuhusu ommission na contradiction?
Mhe. Lissu: Nilisema.
Katuga: Ulisoma kifungu cha 163 hapa Mahakamani? Na ukasema hakuna neno omission kwenye kifungu hicho na neno pekee lililopo ni contradiction?
Mhe. Lissu: Nakumbuka.
Katuga: Ulimuuliza Kaaya ameajiriwa mwaka 2009 na ameenda Zanzibar au hajaenda? Na akajibu hayamo? Unakumbuka?
Mhe. Lissu: Nakumbuka.
Katuga: kutokuwepo kwenye maelezo yake ni contradiction au ommission?
Mhe. Lissu: Omission.
Katuga: Kwenye hiki kielelezo ni contradiction gani ipo hapo?
Mhe..Lissu: Mahakamani alisema ni Uhaini lakini kwenye maelezo amesema ni makosa ya jinai.
Katuga: Uhaini ni madai au jinai?
Mhe. Lissu: Jinai ziko ngapi sasa? Alitakiwa kueleza kuwa jinai ni ipi?
Katuga: Ni bado unasema kwenye hiyo nyaraka kuna contradiction
Mhe. Lissu: Nimeshaonesha.
Katuga: D2 unakumbuka ulimuhoji kwamba yeye ni mtaalamu wa picha aliyetangazwa kwenye GN 725 akajibu maneno hayo hayamo.
Mhe. Lissu: Ndio.
Katuga: Je hiyo ni Contradiction?
Mhe. Lissu: Ni comtradiction ndio kwasababu zilitajwa GN. mbili tofauti. Ni contradiction ya akichokisema kwenye maelezo yake ya maandishi.
Katuga: Yale majibu yote aliyosema hayamo yalikuwa ni contradiction au ommission?
Mhe. Lissu: Ni omission
Katuga: Ulisema hiyo omission inaenda kwenye root ya kesi
Lissu: Tutasema hayo mengine kwenye final submission mimi ni shahidi wa facts.
Part 292 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 297
Ajuaye: Ulitoa taarifa sasa wewe polisi?
Mhe. Lissu: Ilikuwa ni miezi sita kabla ya uchaguzi. Natoaje taarifa polisi wakati siku kwenye mkutano wa kampeni na nilishakwambia sikuwa nafanya public meeting.
Ajuaye: Soma kifungu cha 23 cha Political parties act
Mhe. Lissu: Soma wewe uliza swali.
Ajuaye: anakisoma je ulitoa taarifa
Mhe. Lissu: Siwezi kutoa taarifa mikutano ya ndani. NEXT?
Ajuaye: Kifungu kinasema public place or any other area
Mhe. Lissu: Hujui wewe hata kusoma kingereza kifungu kinasema public meeting conducted at any area. Sasa wewe umesoma shule gani Dada angu?
Ajuaye: Tulia kwanza. Una kifungu chochote kinachosema unaweza kufanya mkutano wa ndani bila kibali?
Mhe. Lissu: Hicho hicho kifungu cha 23 cha Sheria ya Vyama vya siasa.
Ajuaye: Maneno ya kukinukisha uliyakubali hata kama video hatujaleta?
Mhe. Lissu: Sikuongea maneno ya Uhaini mimi.
Ajuaye: Ni ukweli kwamba hata kama video haikuletwa lakini uliongea maneno ambayo yapo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Maneno niliyoshitakiwa kwamba yalikuwepo kwenye video yalikuwa ya masaa matatu hayakuwa ya uhaini.
Ajuaye: Video ni kifaa kilichobeba maandishi?
Mhe. Lissu: Kumbe iko hivyo? Mimi sijui.
Ajuaye: subiri nikiwa mshitakiwa au shahidi utaniuliza. Nitakuomba uwe Wakili wangu?
Mhe. Lissu: Siwezi kuwa na mteja kama wewe ambae anasingizia singizia watu makosa.
Ajuaye: ni kweli mahakama ndio inaweza kusema mtu fulani amefanya kosa fulani?
Mhe. Lissu: Itasema kama mtu huyu atakuwa amepelekwa mahakamani.
Ajuaye: Nani anasema walikamatwa kwasababu walikuwa na makosa?
Mhe, Lissu: Walikamatwa bila kuwa na makosa.
Ajuaye: Ulisema kama ukamataji wako ulikosewa?
Mhe. Lissu: Nilisema na Kiswaga aligoma kuandika na hapa nilisema kwenye mahakama hii.
Ajuaye: Ni very serious allegation hizo
Mhe. Lissu: Ndio ndio maana nilileta mahakamani na wewe ulikuwepo siku ile. Uliona.
Ajuaye: Wanaosimamia sheria ya uchaguzi ni serikali?
Mhe. Lissu: Sheria ya Uchaguzi inasimamiwa na Tume ya Uchaguzi. Na tume ya Uchaguzi sio Serikali.
NB. Leo nimeshuhudia ni kwa kiwango gani TAIFA lina Mawakili wa Serikali ni VILAZA.
Ajuaye: Kupinga uchaguzi ni takwa la kisheria?
Mhe. Lissu: Sisi tulikuwa tunataka uchaguzi usifanyike kabisa. Mambo ya kupinga hata kwenye uchaguzi halali kuna kupinga matokeo ya uchaguzi.
Anakuja askari wa Magereza huwa ni mnaa mnaa sana. Mnoko sana. Amewafuata mawakili wa serikali kwasababu imefika saa 11 na nusu kwa sasa.
Wanajadili mawakili wa Serikali muda huu.
Mhe. Lissu: Ule utaratibu wa kuishia saa 11 kamili vipi tumeubadilisha.
Jaji Ndunguru: Tulidhani wanamaliza maswali yao ndio maana tukawa tunawaangalia tu. Sasa ngoja tuwaulize. Upande wa serikali mnasemaje?
Ajuaye: Basi tuahirishe hadi kesho.
Jaji Ndunguru anateta na wenzake.
Sasa tukutane kesho asubuhi kuendelea.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 296
Wakili wa Serikali Job Mrema: Kama kuna mgogoro si unatakiwa kwenda Mahakamani?
Mhe. Lissu: Ukiwa ni mgogoro wa kiimani unaenda kanisani na msikitini kutatua. Yakisheria ndio unaenda Mahakamani.
Job Mrema: Unakubaliana na mimi kuwa ulisema majaji hawatendi haki?
Mhe. Lissu: Hilo sio geni amelisema jaji Nyalali, Tume ya Warioba imesema. Hata na kikosi kazi pia kimesema. Hakuna jipya hapo.
Job Mrema: Ulisema Majaji ni Ma CCM na Huko Mahakamani hakuendeki?
Mhe. Lissu: Ndio.
Job Mrema: Kupandikiza wananchi chuki katika mfumo wa utoaji haki ni kosa? This is general question.
Mhe. Lissu: hiyo chuki maana yake nini sasa? Niambie kwanza.
Job Mrema: Kifungu cha 52 cha Media service Act. Kinasemaje na unakionaje?
Mhe. Lissu: Kama ukisababisha chuki, dharau au kutokuridhika na mfumo wa utoaji haki ni nia ya kichochezi.
Job Mrema: ukiwa na nia unakiuka kifungu hicho
Mhe. Lissu: Kwa maana ya kifungu cha 52(2) hukiuki lakini 51(1) C ni sawa.
Job Mrema: Kuhusu Majaji ni ma ccm na mahakamani hakuendeki hiyo statement inakiuka kifungu cha 52(1)
Mhe. Lissu: Sikubaliani na wewe kabisa.
Job Mrema: Kulikuwa na amri ya kuficha mashahidi?
Mhe. Lissu: Ndio
Job Mrema: Hukuchukua hatua.
Mhe. Lissu: Niko gerezani unataka nichukue hatua gani?
Job Mrema: Unawakumbuka mashahidi wa siri?
Mhe. Lissu: Nawakumbukaje wakati nimekwambia siwafahamu? Unawafahamu wewe. Majaji na mimi.
Job Mrema: Ni sahihi kwamba uamuzi wa mashahidi wa vificho hauwezi kuzungumziwa kwenye kesi hii?
Mhe. Lissu: ingekuwa haiwezekani hivyo vizimba hapo visingefumuliwa kipindi kile. Kwani nilipinga kwenye kesi gani ya Bibi yako?
Jaji: Haya tuendelee swali lingine.
Job Mrema: Mheshimiwa tunaendelea.
Jaji Ndunguru: Sasa nyie si mpo wengi hapo Mawakili wa Serikali mwingine aingie haraka aanze kuuliza wakati huyu anatafuta maswali yake.
Watu wanacheka😂😂
Job Mrema: Uliwasilisha chochote kuhusu kupigwa Tar. 11/08/2024 kule Mbeya?
Mhe. Lissu: Nimesema kwa mdomo na ndio maana niliapa kabla ya kutoa ushahidi.
Job mrema: Tar. 23/09/2024 ulivamiwa nyumbani kwako na polisi na hakuna ushahidi wowote ulioleta?
Mhe. Lissu: Nilisema nivamiwa na kukamatwa wakanipeleka mbweni na usiku walinirudisha nyumbani. Ulitaka nilete nini kwenye hayo maneno?
Job Mrema: Ulisema watu 466 ulisema case no zao wale wa Tarime.
Mhe. Lissu: Sikueleza.
Job Mrema: PW1 ulisema alifungua jalada tarehe 04 April
Mhe. Lissu: Nilivyosema mimi au PW 1 mwenyewe ndio alisema.
Job Mrema: PW 1 Kwahiyo umesema ilikuwa ni lazima amwambie DPP kuhusu mashitaka haya?
Mhe. Lissu: Soma kifungu cha 16 na 24 cha National Prosecution Act kinasema makosa ya jinai ni DPP ndio anapaswa ku coordinate ushahidi. Sasa yeye hakufanya hivyo. Hakuwahi kumpa taarifa na alisema hivyo.
Job Mrema: Ni chombo kipi kimepewa mamlaka ya huyu ana hatia na huyu hana hatia?
Mhe. Lissu: Ilikuwaje nyie polisi mseme huyu ni mkosaji wa uhaini hata kabla ya ushauri wa DPP?
Job Mrema: Sasa kama mashitaka yalikosewa unafanya nini?
Mhe. Lissu: Najitetea kwa makosa ya kubambikizwa.
Job Mrema: Mahakama hii imetoa uamuzi kuhusiana na makosa yako?
Mhe. Lissu: Haijatoa.
Job Mrema. Amerudi kwa wenzake wanaongea kama dakika tano hivi. Jaji Ndunguru anawaangalia kwa hasira sana.
Anasimama anasema naomba kuishia hapa nimkaribishe Ajuaye Zengeli.
Ajuaye: Ni sahihi kwamba wakati mnafanya mkutano huo hamkuwa na kibali chochote?
Mhe, Lissu: Hakuna mkutano wa ndani unahitaji kibali. Pia hakuna mkutano wowote wa vyama vya siasa unahitaji kibali unatakiwa kutoa taarifa tu.
Ameingia kilaza mwingine huyu Ajuaye.🚮
Ajuaye: PGO 403
Mhe. Lissu: Soma wewe inasemaje nikujibu swali.
Ajuaye: Basi soma PGO 402
Mhe. Lissu: Inahusu mikutano ya kampeni
Watu wanacheka😂
Ajuaye: Umekielewaje?
Mhe. Lissu: Mambo ya uchaguzi na taratibu za kampeni za uchaguzi
Part 297 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 294
Mwenyekiti ameingia tayari baada ya kumaliza kuongea na mawakili wake na break pia kwa ajili ya Chakula cha Mchana.
Alipata nusu saa pia ya kukaa na Mawakili wake na mashahidi wake wengine. Mh. Heche, Mnyika, Amani na Brenda walikuwepo nae.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa uko tayari tuendelee.
Mhe. Lissu: Niko tayari.
Katuga: Mh. Jaji naomba Exhibit D15. Makarani wanaitafuta. Ni maelezo ya PW 16. Ulisema wapelelezi hawakukuuliza maana ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: PW 1 alisema alikuhoji kuhusu maana ya maneno yako?
Mhe. Lissu: Hakunihoji hilo.
Katuga: PW 1 alisema alikupa nafasi kuhusiana na haya maneno kwanini yasiwe ya uhaini?
Mhe. Lissu: Nilimjibu mmeshanikamata na mmeshanishitaki tutakutana mahakamani ndio nilimjibu.
Katuga: PW 1 alikupa nafasi au hakukupa nafasi?
Mhe. Lissu: Alishanishtaki kwa uhaini.
Katuga: Ulizuiwa nini ulipoambiwa utoe maelezo yako?
Mhe. Lissu: Tutakutana mahakamani
Katuga: Ndio maana hukutaka kutoa maana ya maneno?
Mhe. Lissu: Sikuulizwa kuhusu maneno alisema kuhusu uhaini, nikamwambia twende mahakamani.
Katuga: Ungeweza kutoa maana ya maneno au usingeweza pale angekuuliza?
Mhe. Lissu: Sasa halikuulizwa hilo nitoleee nini? Ningejibu angeniambia.
Katuga: Ulirejea Maelezo D15 ni maneno ambayo umeyaamini na yapo kwenye kielelezo chako?
Mhe. Lissu: Maneno yapi? Unauliza mambo jumla jumla. Eleweka.
Katuga: Baada ya kuunda timu mimi na timu tulisikia
Mhe. Lissu: Tulisikiliza sio tulisikia soma vizuri wewe
Katuga: Nina miwani siku hizi sioni vizuri.
Mhe. Lissu: Ukiwa na miwani ndio unasoma vizuri acha uongo.
Katuga: Yangu ni ya bei halisi
Lissu: Sasa unalipwa nini? Au unajitutumua bure tu hapa?
Katuga: Je haya maneno nimesoma ulirejea?
Mhe. Lissu: In relation na ushahidi wa PW1 ndio niliyarejea. Kuhusianisha na PW 16 alichosema.
Katuga: Kwahiyo ulikiamini kielelezo?
Mhe. Lissu: Nilikiamini kivipi? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.
Katuga: Kwahiyo ulikiamini?
Mhe. Lissu: Mimi niwaamini Mapolisi hawa? Nilikitumia kuonesha utofauti wa mashahidi wawili wa Jamhuri.
Katuga: Sasa nijibu unayaamini yaliyomo humo?
Mhe. Lissu: Niamini nini?
Katuga: Uko sawa kweli?
Mhe. Lissu: Wee unanionaje?
Katuga: Naona uko sawa.
Mhe. Lissu: Sasa unaniuliza nini kama unasema niko sawa?
Jaji: Sasa wakili toka hapo. Tumeshapata majibu.
Katuga: Ulisema haya maelezo yote kuanzia D1 hadi D16 ulitaka yatumike kwa ajili yako?
Mhe. Lissu: Nilishajibu toka zamani. Kwa ajili ya kuonesha utofauti wa ushahidi. Contradiction ya ushahidi na ommission zilizofanyika.
Katuga: Kuna sehemu ulisema mahakama i exclude baadhi ya maneno yaliyopo humu?
Mhe. Lissu: Hiyo ni kazi ya submission.
Katuga: Narudia tena ulisema au hukusema?
Mhe. Lissu: Nimekwambia hiyo ni kazi ya submission.
Jaji Ndunguru: jibu tu swali shahidi umeiambia mahakama au hujaiambia.
Mhe. Lissu: Narudia tena nitawaambia wakati wa final submission nimemaliza.
Jaji Ndunguru: Haya sasa wakili wa serikali endelea mbele. Jibu ndio limeshatoka hilo na halitabadilika.
Kicheko kutoka kwa umma 😂😂😂
Katuga: Mheshimiwa Jaji naomba nirudishe kielelezo.
Anaendelea kupekua makaratasi yake. Kamaliza maswali ila anatupotezea muda tu hana lolote mshenzi huyu.
Part 295 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 290
Katuga: Ulisema Mashahidi waliolindwa walifanyaje?
Mhe. Lissu: Walikuwa ni washitakiwa na watuhumiwa wa makosa
Katuga: Sheria inawazuia wasiwe mashahidi
Mhe. Lissu: Haiwazuiii.
Katuga: Mashahidi wa Jeshi la Polisi walieleza kuwa walikamata wote?
Mhe. Lissu: Walisema wamewakamata waliowatambua.
Katuga: Kwahiyo kuna wengine hawakukamatwa?
Mhe. Lissu: Ntajuaje sasa?
Katuga: Ile kauli yako ya tutavuruga uchaguzi ulisema mtu yeyote anaweza kutafsiri anavyoona?
Mhe, Lissu: Sahihi
Katuga: Walisema hawa mashahidi kuwa waliyopanga yalitokana na maneno yako?
Mhe. Lissu: Najuaje sasa watu siwajui na siwafahamu. Nasemaje watakuwa wanasema ukweli.
Katuga: Katika ushahidi wako umeiambia mahakama hii tukufu kuwa hawa mashahidi hawasemi kweli?
Mhe. Lissu: Nimeiambia mahakama kuwa huu ushahidi ni wa wahalifu na ni waongo.
Katuga: Katika utetezi wako ulisema kuwa wewe uliwachochea?
Mhe. Lissu: Wapi nimesema hivyo? Sijasema mimi.
Katuga: Wanasema maneno yako ndio yaliwachochea sasa wewe uliwaambia majaji kuwa maneno haya hayawezi kuwachochea.
Mhe. Lissu: Nimewaambia Majaji maneno haya hayawezi kuwa uchochezi sio kosa pia. Labda kama ulikuwa umelala.
Katuga: Waheshimiwa naogopa kurudia maswali. Amekaa kimya anatafuta tafuta. Sasa wale mashahidi waliolindwa
Mhe, Lissu: mimi nimekwambia mashahidi waliofichwa hiyo kulindwa umetoa wapi?
Katuga: Witness protection ni nini kiswahili?
Mhe, Lissu: Mashahidi waliolindwa. Lakini sasa mimi nimesema kwangu ni mashahidi waliofichwa. Hiyo ya kulindwa ni yakwako.
Katuga: Je wale mashahidi walifichwa kweli?
Mhe. Lissu: ni ushahidi wangu kuwa hao mashahidi hawajulikani
Katuga: Huo ni ushahidi wa kuona au kusikia.
Mhe. Lissu: Ni ushahidi wa inference hakuna anayewajua isipokuwa mapolisi.
Katuga: Hizo ni speculations au ushahidi wa direct.
Mhe. Lissu: Huo ni ushahidi.
Katuga ameenda kunong'ona na wenzake.
Anauliza sasa swali: Nimehama kwenye inference. Maneno unawezekana maneno ya mashahidi wakulindwa inawezekana walikuwemo humu ndani wakati kesi inaendelea.
Mhe. Lissu: Nimeshasema hawajulikani na mtu yeyote.
Katuga: Ni kweli au sio kweli?
Mhe. Lissu: Ni ushahidi wa inference. Huelewi nini? Kwasababu mnawajua nyie peke yenu.
Katuga: Mimi sitoki hapa
Mhe. Lissu: Hata mimi sitoki.
Katuga: Mahakama inakunote
Mhe. Lissu: Kwanini wewe haikunote?
Katuga: kwahiyo ni kuona au kusikia?
Katuga: Shahidi shule si ulikuwa unafundishwa multiple choice?
Mhe. Lissu: Mimi sijafundishwa multiple choice. Mimi nimefundishwa critical thinking. Sheria unafundishwaje multipe choice? Ndio maana unakuwa mjinga.
Katuga: Hii kauli hawa mashahidi inawezekana walikuwepo mahakamani ni maoni au ushahidi?
Mhe. Lissu: Ni ushahidi wangu maoni kivipi.
Katuga: Kwenye ile video kuwa Majaji ni Maccm ulisema hukumbuki?
Mhe. Lissu: Nilisema nakumbuka. Huwa sikatai maneno yangu.
Katuga: Una kesi nyingine ya jinai ya kuchapisha taarifa za uongo?
Mhe. Lissu: Ipo Kisutu anawatajia hadi namba nyingine ya kesi.
Katuga: Ulisomewa hoja za awali na imeanza kusikilizwa?
Mhe. Lissu: Imesomwa lakini sikumbuki.
Katuga: Uliposomewa hoja za awali na kwamba ulitoa maneno kuwa majaji ni Ma CCM? Ulijibuje?
Mhe. Lissu: Sikumbuki. Sasa unaniulizaje hayo mengine.
Katuga: Mwenyekiti wa CHADEMA ni kweli ulitangaza kutogombea uchaguzi wa Mwaka jana?
Mhe. Lissu: Sikumbuki.
Katuga: Chama chako kilishiriki Uchaguzi mwaka jana?
Mhe. Lissu: Uchaguzi gani sasa? Hakikushiriki.
Part 291 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 27, 2026
Last time tuliishia part 288 so leo tunaendelea na -;
Part 289
Majaji wameingia muda huu na Mwenyekiti ameingia Mahakamani.
Anasimama Karani wa Mahakama anasema Criminal Session No. 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Iwapendeze Majaji Naitwa Ajuye Zengeli, Nassoro Katuga, Job Mrema, Cathbert Mbiringe, Winiwa wote tunaiwakilisha Jamhuri na Mtuhumiwa yupo hapa. Tuko tayari kuendelea na maswali ya Dodoso.
Mh. Lissu naomba nipate nafasi ya kuconsult mawakili wangu kidogo.
Anasimama Dr. Nshala anashauriana nae hapo kizimbani kwa dakika kama tano.
Sasa niko Tayari.
Katuga: Kaka angu Shikamoo?
Mhe. Lissu: Marahaba
Katuga: Kama nilikuelewa unasema kuna tuzo ulipewa ilitokana na kupigania haki kwa nchi za Afrika. Je ulitaja hizo nchi za Afrika ulizopogania?
Mhe. Lissu: Sikutaja
Katuga: Ulisema heshima imeongezeka ulifanya sensa wapi?
Mhe, Lissu: Heshima haipatikani kwa sensa. Inatokana na watu wanaoheshimika wakakuheshimu.
Katuga: Kwahiyo imeongezeka ni kwasababu wazungu wamesema?
Mhe. Lissu: sijasema wazungu nimesema Jumuiya za Kimataifa na zinaheshimika kweli.
Katuga: Ulisema mgombea wa Mlimba alirudisha fomu akakuta ofisi imefungwa? Je ulikuwepo?
Mhe. Lissu: Hizo ni taarifa rasmi sio lazima niwepo, nilisoma kwenye taarifa rasmi.
Katuga: Ukitoa mashahidi kutoa Jeshi la Polisi hawa waliolindwa hawajulikani na mtu yeyote?
Mhe:Lissu: Ndio
Katuga: Haya maneno umesema kuonesha ukweli wako?
Mhe. Lissu: Kweli
Katuga: Uamuzi wa Majaji ulisemaje kuhusu mashahidi wa siri?
Mhe. Lissu: wawaone wao.
Katuga: Uliwaambia kuwa hawawajui majina na kila kitu?
Mhe. Lissu: ni ushahidi wangu hawawajui ndio
Katuga: kwahiyo hawawajui majina?
Mhezx Lissu: Sasa mtu gani anaitwa P2, Sijui P
Katuga: Kwahiyo hayo ya P1, P2 sio majina?
Mhe. Lissu: Sio majina hayo nimesema.
Katuga: Hizo si ni synonim?
Mhe, Lissu: Synonim sasa ni majina? Hayo sio majina.
Katuga: Umesema ni sheria gani shahidi anapaswa kutoa jina?
Mhe, Lissu: CPA na sheria ya Ushahidi zote zinasema jambo hilo.
Katuga: Naomba Kifungu?
Mhe, Lissu: Kifungu cha 192 cha CPA
Katuga: kisome sasa wapi wanasema wataje majina?
Mhe, Lissu: kisome uone kinasemaje ngoja nikusomeee kinapotaja hitaji la jina?
Katuga: sitaki ukisome.
Mhe. Lissu: Hutaki tena nisome.
Katuga: Kwahiyo neno la kuwa lazima watoe jina lipo?
Mhe: Lissu: Unadhani kwanini mashahidi huwa wanaulizwa majina yao Mahakamani?
Katuga: Hilo sijakuuliza.
Mhe, Lissu: Hiyo sasa utajua mwenyewe kama hujaniuliza.
Katuga: Pw 17 alisema kuna muda waandishi wa habari walitolewa mkabaki wenyewe na kikao cha ndani? Uliwahi kukanusha hilo?
Mhe. Lissu: Nikanushe la nini? Ndio ukweli
Katuga: Una volunteer sana information.
Mhe.Lissu: Ndio kazi yangu.
Katuga: Majibu yako yana vutia sana.
Mhe. Lissu: then, you should be happy.
Katuga: Kwahiyo nichekecheke
Mhe. Lissu: Fanya hivyo
Katuga: Kwahiyo mliwatoa waandishi nje, wewe na wenzako?
Mhe. Lissu: Tuliwatoa.
Katuga: Mliwatoa kwasababu hayo mengine hayakuwa sehemu ya mliyowaitia. Kwahiyo yale ambayo mlitaka wayachapishe ndio mliruhusu wawepo?
Mhe. Lissu: Ndio.
Katuga: Ambayo hukutaka yachapishwe mliwatoa waandishi?
Mhe. Lissu: Yote tuliyotaka watu wajue waliyajua.
Katuga: Je kwenye ushahidi wako ulisema sheria mahsusi kwamba ukigundua kosa la uhaini unapaswa kuwasiliana na DPP?
Mhe.Lissu: Nikitaje cha nini? Haina maana hakipo kama sikukitaja.
Katuga: Mimi lazima nikuulize maswali nisipofanya nitakuwa sifanyi kazi yangu
Mhe. Lissu: Fanya kazi yako.
Katuga: Ulisema kuna mgogoro binafsi na Wambura na Kingai?
Mhe. Lissu: nimesema kuna chuki kubwa dhidi yangu. Nimekuwa persecuted maliciously 24yrs.
Katuga: Umewahi kufungua malicious prosecution
Mhe. Lissu: Haina maana yoyote sijawahi kuwafungulia lakini haiondoi ukweli wowote.
Part 290 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 299
Jaji Ndunguru anamwambia Mhe. Lissu, sasa hayo uliyosema si ndio mwongozo tunapaswa kumpa?
Mhe, Lissu anasema tutafika tumechoka sana kama mwongozo wenyewe mnaopaswa kuutoa ni huo kila mara.
Yeye mwenyewe wakati anaomba ni kama alikuwa hajielewi anaomba nini hana uhakika kabisa.
Jaji anateta na wenzake kwa dakika kadhaa hapa. Sijui wanateta nini? Hizi kazi ni ngumu sana.
Wazee sio bure watakuwa na presha nyingi. Jambo tunaloona ni dogo wameshajadili karibu dakika 10 hadi sasa. 😂😂
Mhe. Lissu Mungu ambariki tu, Imagine kikundi cha Mawakili 10 wa Serikali yeye yuko peke yake pale kizimbani lakini wanateseka kiasi hiki🙌.
Majaji wako watatu nao wanashauriana dakika za kutosha, hili linatuma ujumbe mkubwa sana. Ngoja tuone.
Jaji Ndunguru anawasha MIC sasa pamoja na kwamba umesema kuwa umejibu na suala hili ni dogo lakini Mahakama ni muhimu ikatolea muongozo hili.
Sasa suala ni scope ya hiyo re examination. Sasa tutajikita kwenye scope hiyo na kama kutakuwa na new matters basi serikali wazuie au wataomba kukuuliza maswali. Mahakama pia ina nafasi ya kuuliza na hatuwezi kuzuia Re-Examination. Kazi yetu tunaijua vizuri.
Mhe. Lissu anasema naomba wasaidizi wangu wanipatie swali la mwisho lililoulizwa.
Anapatiwa sasa.
NB: Kwa kifupi walichoamua Majaji ni kwamba kwa maneno mengine wamesema KATUGA ni KILAZA na Jina KATUGA linapaswa kuanza kutumika kumuelezea MWANASHERIA yeyote ambae ni KILAZA basi aitwe KATUGA.
Majaji wanapiga story na kuangalia kompyuta zao sijui kuna nini tena, Mhe. Lissu hajaanza bado re examination.
Anasimama Ajuaye Zengeli anasema Waheshimiwa Majaji naona utaratibu unakiukwa. Shahidi anaomba washauri wake wampe sio utaratibu.
Mhe. Lissu: Kwamba naulizwa maswali lazima niwe naandika na kujibu hapo hapo inawezekana? Hili nalo lina shida kweli mimi kuandikiwa? Watu wameandika maswali na majibu hawa vijana wangu shida iko wapi? Mapingamizi ya bure kabisa.
Jaji Ndunguru: Basi endelea.
Mhe.!Lissu: Niliulizwa kuhusu nia inathibitishwa kwa matendo, nikasema sio kweli. Ufafanuzi wangu ni kwamba sio kila nia inathibitishwa kwa matendo. Nyingine ni kuchapisha.
Jaji Ndunguru: Tuendelee
Mhe. Lissu: Aliniuliza kuhusu Mahakama kutokulazimishwa au haipangiwi na baraza la umoja wa Mataifa. Ufafanuzi wangu ni kwamba Mahakama mapendekezo au maoni hayo ya vyombo vingine ni muhimu pia kuzingatia ushauri wa hizo taasisi zingine.
Katuga: Mambo ya Umuhimu asiyalete.
Mhe. Lissu: Basi niseme Mahakama huwa inaangalia maamuzi ya vyombo vingine.
Katuga: Mimi sitaki aende huko. Asililete sasa hivi.
Kwa kifupi Bwana Katuga kwa sasa ameamua kutupotezea muda humu ndani ilimradi tu.😂😂😂😂
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu tuzo na kwamba nimezileta nikasema sijazileta na ni legal principles na kwamba mimi sio mwenye wajibu wa kuthibitisha sina hatia bali mzigo wa uthibitishaji uko upande wa mashitaka. Iko hivyo.
Hiyo naona imeingia. Hawajasimama akina KITUGA.
Mhe. Lissu: Niliulizwa vilevile kwamba niliwahi kuwa Rais wa TLS na nikajibu kweli na nikaulizwa wakati unashitakiwa na kesi hii ulikuwa Rais wa TLS na je kunakupa kinga.
Jaji Ndunguru: Naona hilo ni obvious hata usilitoleee ufafanuzi.
Mhe. Lissu: Sawa basi kuna swali la njia za Kidemokrasia nilisema ipo ya Mahakama na maandamano ya kidemokrasia. Nikaulizwa ipo kwenye kifungu gani cha Katiba nikasema kifungu cha 20(1) Cha Katiba. Naomba kutoa ufafanuzi kuwa hizo njia za nje ya mahakama zinatambulika kikatiba na zimethibitishwa hivyo na Mahakama
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 225
Mhe. Lissu anaendelea hapa.
Kama mtakumbuka nilisema ninavyoishi Ukonga, siruhusiwi kuonana na Mawakili wangu in private.
Mnaruhusiwa kutembelea Magereza naomba mliangalie na hili kama itawapendeza inawapa Mamlaka ya kutoa mapendekezo na mamlaka za Magereza kurekebisha masuala yanayohusu wafungwa kama haya niliyosema.
Ni muhimu kwamba kuwasiliana na washauri wangu wa kisheria ilindwe kama sheria inavyosema bila kusikilizwa na maafisa wa Magereza.
Ni hayo tu Waheshimiwa
Mhe. Tundu Lissu amemaliza na amekaa sasa.
Majaji wanaandika hapa.
Anasimama Renatus Mkude kuwa tutampatia hizi nyaraka ndani ya siku 14 tutampatia.
Hili la masuala ya utawala wa mambo ya magereza kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha National Prosecution Act na sisi ofisi ya DPP tutatembelea ili kuhakisha kunakuwa na fair trial.
Wameombwa Majaji anasema DPP ataenda eti huko Magereza kuangalia haki za Mtuhumiwa. Uongo uongo uongo. Hawana hata aibu hawa jamaa.
Majaji wanaandika baada ya kusikia hayo kutoka kwa Wakili wa Serikali, Renatus Mkude.
Majaji wanajadili pale.
Yuko Jaji muda wote yeye huwa anacheka anafurahi tu sijui huwa anatabasamu jambo gani? Wanaofika hapa Mahakamani wanamfahamu vizuri.
Jaji Ndunguru: Tumesikia hoja za Jamhuri na Hoja za Mshitakiwa nae kama ambavyo mshitakiwa ameturahisishia kuwa mikono yetu imefungwa kwamba yapo hayo maombi ya marejeo Mahakama ya Rufani.
Sasa shauri hili linasimama hadi pale Mahakama ya Rufani itakapotoa uamuzi.
Suala la Gerezani wakili wa Serikali amesema na sisi pia tumelichukua.
Mwenendo wa shauri hili unasimama hadi pale mambo ya Court of Appeal yatakapoisha.
So kesi hii imeahirishwa hadi hapo itakapoitwa tena.
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 28, 2026
Last time tuliishia part 297 so leo tunaendelea na -;
Part 298
Saa nne kasoro robo Mhe. Lissu anaingia na wananchi wanapiga makofi kwa pamoja.
Hii ni style mpya leo ya kumkaribisha hapa Ukumbi Na. 1 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Inapigwa Courtttttt harakaharaka na Jaji Karyemaha ametangulia kwa kasi sana.
Anafuatia Jaji Ndunguru na Mzee wa Burudani Jaji Kiwonde yuko nyuma yao.
Wanaingia wanakaaa.
Mwenyekiti Lissu nae anatafuta Vitabu vyake.
Karani anasoma namba ya kesi na kukaaa.
Anasimama Ajuaye Zengeli anasema anasaidia na Katuga, Mrema, Thawabu, Cathbert na Winniwa Kasawa wote ni Mawakili wa Serikali.
Na shauri limekuja kwa mshitakiwa kuulizwa maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu : Niko tayari kuendelea.
Mhe. Lissu anaomba niongee na Mawakili wangu kwanza, anaenda pale Dr. Nshala, Mahinyila, Nashon Nkungu, Dorice Kafuku,
Ajuaye: Nia ya kutenda kosa inathibitishwa na tendo?
Mhe. Lissu: Sio kweli
Ajuaye: Waheshimiwa tulikuwa na swali moja kwa shahidi na tumemaliza maswali ya Dodoso kwa shahidi huyu.
Huyu Ajuaye ni kilaza sana, ameuliza swali moja na amesema amemaliza kabisa.
Majaji wanaandika na Mheshimiwa Lissu anapanga makabrasha yake hapa.
Mhe. Lissu anaomba kufanya re-examination baada ya kuwa wamemaliza kufanya cross examination.
Anasimama Katuga kuwa naomba tutoe hoja anasema Re examination ni moja ya examination ya utoaji ushahidi. Kifungu cha 155 Sura ya 6/2023.
Kifungu cha 156(3) cha Sheria ya Ushahidi kinasema Re-Examination itafanyika kwenye mambo gani na utaratibu wa kufuata.
Nimerejea kwenye hivyo vifungu ili tupate tafsiri kuwa yale maswali aliyoulizwa ndio tutaita re examination. Alikataa uwakilisha yeye mwenyewe ni jinsi gani atajifanyia maswali ya ufafanuzi kutokana na majibu yake. Lengo ni kutoa ufafanuzi.
Waheshimiwa Majaji tunaomba mahakama ijiulize. Majibu shahidi katoa mwenyewe, na kujiuliza anajiulizaje mwenyewe.
Huwezi kuwa Jaji kwenye kesi yako. Principle zetu za kisheria ziko hivyo. Unajuaje wengine hawajakuelewa hadi utake kutoa ufafanuzi.
Haya maswali ya re-exanination yanaulizwa na nani? Hili eneo ni gumu na muangalie vifungu vya Sheria unless tutakuwa tunafungua uwanda mwingine wa ku introduce inshu mpya.
Ili kuepuka hili la usijijibu wewe na ukajiuliza wewe. Mahakama inaweza kumuuliza yenyewe. Hiyo right ya re-examination iko kwa party iliyomuita shahidi.
Jaji Ndunguru: Sasa ombi lako ni nini?
Katuga: Mahakama kama itataka kumuuliza imuulize yenyewe lakini pia imuelekeze shahidi nini cha kujibu na naomba Mahakama itoe maelekezo kwenye eneo hilo. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru: Anateta na wenzake. Naona wanachungulia PC kwenye ile ya Karyemaha. Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Lissu: Naomba Wakili wa Serikali aiambie Mahakama kama ameleta pingamizi aseme au ameleta mapendekezo na maelekezo kwa Mahakama.
Amesema anawapa ushauri kama ni ushauri tuachane nao tufanye kazi iliyotuleta na kama ni pingamizi basi nitamjibu.
Jaji Ndunguru: mnasemaje serikali
Katuga: Labda kama alikuwa hasikilizi, mimi naomba mwongozo wa Mahakama.
Mhe. Lissu: Hakunaga kuomba mwongozo Mahakamani lakini basi ngoja nijibu huo mwongozo.
1. Re examination ni haki ya shahidi aliyekuwa examined ndo maana kifungu cha 156(1) alichotaja ni haki ya re-examination ni haki yangu basi Wakili wa Serikali alipaswa kunyamaza kimya.
2. Anasema Atajiongozaje kama hana Wakili. The fact kwamba shahidi kwamba ndo mshitakiwa haimuondolei haki ya kufanya re exanination. Sasa nitafanyaje? Nitarejea maswali niliyoulizwa nitasema majibu yangu na nitaweka ufafanuzi wangu hapo.
3. Hii inaweza kuwa ni fursa ya ku introduce new facts huwa wana rise objection kwahiyo hofu yake ni unfounded completely. Ni hofu ya bure kabisa.
4. Hamna mwongozo wa kutoa hapa na kesi ndio zinaendeshwa hivyo.
Part 299 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 300
Mhe. Lissu anaendelea na Re-examination
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu Ndyanabo na Mtikila na nikasema Mtikila alienda Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika na hadi sasa serikali haijatekeleza maamuzi ya Mahakama ya Haki za Binadamu za Afrika.
Jaji Ndunguru: Hiyo naona ni the obvious nayo usifafanue kabisa.
Mhe. Lissu: Haina shida. Niliulizwa sana kuhusiana na scope ya kifungu cha 39(2)(d) juu ya neno Or kati ya Overt act or deed. Ufafanuzi wangu ni kwamba act or deed is the same thing. Act something that is done and a deed is something is done.
Katuga: Huu ni ushahidi au submission. Anakoenda ni kutoa tafsiri ya overt act or deed.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naona Mahakama inisomeee ili tusivutane vutane hapa.
Jaji Karemaha anasoma kilichoandikwa, anasema kwa vile nimeandika kingereza nitasoma.
Mhe. Lissu: Basi naomba niendelee. Kuhusu mihimili mitatu na kazi zake. Nikasema moja ya kazi za Bunge ni kutunga Sheria na serikali kusimamia sheria. Ufafanuzi wangu ni kwamba kutunga sheria sio kazi pekee ya Bunge.
Mhe. Lissu: Kuhusu mashahidi wa mashitaka hawakuja kutoa ushahidi kuhusu namna nilivyokamatwa. Uhalali wa kukamatwa kwangu ni suala tofauti kwasababu sheria zimeweka utaratibu wa namna ya kukamata na ulifuatwa au laaa suala hilo lilipaswa kujibiwa na upande wa mashitaka.
Mhe. Lissu: Nimeulizwa kuhusu waandishi wengi wa habari waliokuja Tar. 03/04 niliulizwa kama waandishi hao walikuwa wanajua nilichokuwa naenda kuwaambia na kama niliwapa hotuba yangu mapema. Nikasema sikuwapa. Nataka kufafanua, waandishi wa habari huwa hawapewi taarifa hizo kabla.
Katuga: Hilo la kwamba huwa hawapewi hizi taarifa hilo sikuuliza.
Mhe. Lissu: Yeye ndo alileta habari za constructive publication
Jaji Ndunguru: Na wewe ukasema kuwa hukuwa na control ya hao watu, nafikiri hata hili majibu yako yalinyooka tu.
Mhe. Lissu: Sawa. Kuhusu maandamano na kuzuia uchaguzi. Nilisema uchaguzi usiokuwa huru sio uchaguzi.
Mhe. Lissu: Niliulizwa kuhusu adhabu ya kifungu cha 39(2)(d) cha Penal Code atahukumiwa adhabu ya kifo na Wakili akasema sentenced to death. Mimi nilisisitiza ni adhabu ya kifo.
Jaji Ndunguru: Hivyo vifungu vinatofautiana cha mwaka 2022 na cha mwaka 2023. Kuna sheria moja ina liable to death na nyingi shall be sentenced to death. Kwahiyo ile ya 2022 ni kwamba sio lazima upewe adhabu ya kifo lakini ya 2023 ndio haina hiyo option. Inasema direct sentenced to death.
Mhe. Lissu: Haya tuendelee. Kulikuwa na maswali kuhusiana na mashahidi wa kificho na nasisitiza hawakuwa wanajulikana kwa mtu yeyote isipokuwa aliyewaleta.
Kuna hili lingine la kwamba tuliwatoa nje waandishi na nikasema kwa yale ambayo hatukutaka yachapishwe tuliwatoa ni kwasababu walichoitiwa kilikuwa kimeshakamilika.
Naomba sasa vielelezo D1 hadi D16 kwasababu vilitumika sana kwenye cross examination.
Anasubiria kupatiwa.
Part 301 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 302
Majaji wanaingia.
Ajuaye anasema wako tayari kuendelea wao upande wa Jamhuri.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mh. Lissu nae anasema yuko tayari kuendelea. Na shahidi wake anaitwa JOHN JOHN MNYIKA.
Katibu Mkuu Mhe. John Mnyika anaitwa na anapanda kizimbani amevaa Shati nyekundu ya Chama.
Anafuatwa na Karani wa Mahakama wanateta na Mnyika anacheka.
Jaji: unaitwa nani?
Mnyika: John John Mnyika,
Jaji: umri wako?
Mnyika: Miaka 46
Jaji: Kazi yako
Mnyika: Katibu Mkuu wa Chadema.
Jaji: Dini yako?
Mnyika: Mkristu
Jaji: haya muapishe.
Mimi John John Mnyika naapa ushahidi nitakaotoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu na Mungu anisaidie.
Sasa Mhe. Lissu anaanza.
Mhe. Lissu: Nitakayokuuliza uyajibu kwa utaratibu maana Majaji wanaaandika na mimi nafahamu una sauti nzuri tu.
Sasa waeleze majaji umeshikilia nafasi hii ya Chadema kuanzia lini?
Mnyika JJ: Kuanzia 2019 mimi ni Katibu Mkuu.
Mhe. Lissu: Kabla ya hapo ulikuwa na nafasi yoyote nyingine?
Mnyika JJ: Kabla ya KM nilikuwa Mkurugenzi wa Vijana Chadema Taifa kuanzia 2003 hadi 2011 wakati naishikilia nafasi hiyo mwaka 2007 niliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa habari na uenezi hivyo nilishikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja. Nafasi ambayo niliitumikia mwaka 2014.
Na wakati huo huo kati ya mwaka 2009 hadi 2011 nilishikilia nafasi ya Mkurugenzi wa mambo ya nje na uhusiano wa Kimataifa wa CHADEMA.
Na Mwaka 2014 niliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa nafasi ambayo niliishikilia hadi 2019 nilipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu.
Nilipokuwa mbunge pia
Mhe. Lissu: Huko tutakwenda pia bado subiri. Nafasi nyingine je?
Mnyika: Nilikuwa Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni kwa vipindi viwili.
Mhe. Lissu: Nafasi nyingine?
Mnyika JJ: Nilikuwa Katibu wa Wabunge wa Chadema Bungeni kati ya mwaka 2010 mpaka 2015 na nikawa tena Katibu kuanzia mwaka 2016.
Jaji ulikuwa mbunge wa?
Mnyika: Nilikuwa Mbunge wa jimbo la Ubungo 2010 hadi 2015 na baadae Jimbo la Kibamba 2015 hadi 2020.
Mhe. Lissu: Nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema ni nafasi ya aina gani katika uongozi wa Chama.
Mnyika: Ni nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Chama ambae ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Chama na ni msimamizi mkuu wa rasilimali, utawala, uendeshaji wa Chama. Na Katibu Mkuu ndie msimamizi mkuu wa utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya vikao vya juu vya Chama ambavyo ni Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama.
Mhe. Lissu: Taratibu tararibu.
Mnyika anapeleka moto kwa kasi 😂
Vilevile ni msimamizi mkuu wa wafanyakazi wa Chama na waliopo makao makuu ya Chama ikiwemo pia makatibu wote wa Chama.
Mhe. Lissu: Sasa nisubiri mimi.
Eheee Sasa shahidi naomba waeleze Majaji kama Chama Chako huwa kinafanya vikao au mikutano ya Chama na utaratibu wake ukoje?
Mnyika: Chama huwa kina mikutano ya aina mbili kuu ambazo ni Mikutano ya ndani.
Usiposikia Jaji amesema Mhhhhhhh ndo uendeleee.
Mnyika: Kuna Mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani.
Jaji Ndunguru : Sio lazima niseme mhhhhhh naweza sema endelea.
😂😂😂😂 kicheko.
Mnyika: Kwa mikutano ya ndani ngazi ya utendaji chombo husika ambacho ni sekretarieti kinakaaa kikao cha ngazi ya Kitaifa chini ya Katibu Mkuu na kufanya maandalizi ya kikao hicho. Na majukumu yanagawanywa ya maandalizi yake.
Mhe.Lissu: Hapohapo. Subiri. Sasa waeleze majaji nani ni wajumbe wa hiyo sekretarieti?
Mnyika: Ni Katibu Mkuu wa Chama Taifa ambae ndie Mwenyekiti wa Sekretarieti. Manaibu Katibu wakuu wawili. Mmoja wa Zanzibar na Mwingine wa Bara, Wakurugenzi wa Kurugenzi za Chama Taifa, Wataalamu na Katibu wa Sekretarieti anayeteuliwa na Katibu Mkuu na Makatibu wa Mabaraza ya Chama kwa maana ya Baraza la Wazee, Baraza la Vijana na Wanawake. Anataja na vifupi vyake BAZECHA, BAWACHA na BAVICHA.
Part 303 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 26, 2026
Last time tuliishia part 276 so leo tunaendelea na -;
Part 277
Mwenyekiti ameingia tayari Mahakamani akiwa vibe.
Amesema naona wameanza kunyoana wenyewe.
Watu 😂😂😂
Amewaona akina Mzee Lwaitama na Jenerali Ulimwengu anasema nyie Wazee hamjakata moto kama wale wazee wengine.
Amemuona Makamu Mwenyekiti Heche anasema Makamu ongeza kupeleka moto.
Tunawaona mashahidi watatu wa Mh. Lissu wapo hapa Mahakamani, John Heche, John Mnyika na Amani Golugwa.
Majaji wameingia tayari muda huu. Na wakati anaingia watu walikuwa wanaimba mtetezi wa wanyonge kwa sauti na kwa vibe.
Nimemuona anaongea na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Wakilli Mahinyila anamuuliza mmeshaandaa mashahidi tayari. Anamjibu kitu anasema haya leo tutamaliza hakuna shida.
Inapigwa high court
Wanaingia Majaji na kukaa sehemu yao.
Anasimama karani Criminal session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Lissu.
Anasimama Ajuaye Zengeli wakili wa serikali yupo na Katuga, Job Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa kikundi chote kinaiwakilisha Jamhuri na Lissu yupo anajiwakilisha mwenyewe.
Waheshimiwa majaji na mimi niko tayari anajibu Lissu. Na mashahidi wangu wako humu naomba watoke ila wasikae mbali.
Majaji wanateta na kucheka kidogo. Makamu Heche, Mnyika, Golugwa na Brenda wanatoka zao nje.
Watu wanajiset kwenye viti vyao hapo wanakaaa.
Majaji wanateta kidogo kisha wanasema tuendeleee.
Mhe. Lissu anasema haitakuwa vibaya mkinikumbusha nilipoishia.
Jaji Ndunguru pale ulipomtaja Askofu Pissa.
Mhe. Lissu sasa leo nataka nijikite kwenye kesi kama ilivyowasilishwa kwenu na Upande wa Mashitaka. Ushahidi wao walivyouleta, Waheshimiwa Majaji naomba niseme utangulizi ufuatao:
1. Mashahidi walioletwa mbele yenu ni mashahidi wa aina gani na ushahidi wao unapaswa upewe uzito wa aina gani?
2. La pili nitazungumzia ushahidi wenyewe. Ushahidi uliotolewa na mashahidi hawa. Na nitaonesha hakuna kosa la Uhaini na hakuna kosa lolote la jinai kwahiyo hayo ndo mawili ya utangulizi.
Sasa nianze na la kwanza kuhusu hao mashahidi.
Wakati wa Preliminary hearing upande wa mashitaka ulileta orodha ya mashahidi 30. Ambao walisema hao ndio wataleta ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za uhaini dhidi yangu.
Upande wa mashitaka haukuleta mashahidi wote hao 30 badala yake walileta mashahidi 17 peke yake.
Hao 13 ambao hawakuletwa, hawakuletwa kwasababu muhimu fulani na nitazisema.
Hiyo ommission ya hao mashahidi 13 is neither insignificant nore without importance.
Sio kwasababu hawana maana na sio kwasababu hawana umuhimu.
Nianze na ambao waliletwa.
Katika mashahidi 17 walioletwa. Mashahidi 8 ni askari Polisi.
Mashahidi 9 waliobaki ni mashahidi wa kificho.
Mahakama haiwafahamu majina yao. Haiwafahamu kabisa, haifahamu wanaishi wapi? Haifahamu wanafanya kazi gani na haifahamu chochote zaidi ya majina ya P, P1, P2 P nini huko.
Inaweza kuwa tumekuwa nao throughout hapa kesi ikiwa inaendelea kwasababu Mahakama haiwajui na upande wa utetezi hauwajui hata kidogo.
Kwahiyo ushahidi wa hao mashahidi 9 ni ushahidi wa watu wasiojulikana na Mahakama wala utetezi, Watu pekeee wanaowajua ni waendesha mashitaka waliowaleta.
Part 278 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 278
Inawezekana mashahidi hao wa siri ni Mapolisi au mtu yeyote, hao ndio mashahidi wa kesi ya Uhaini.
Mashahidi 8 ambao ni Mapolisi hao ni mashahidi wa Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Camilius Wambura na DCI Ramadhani Kingai ambao nimeonesha kuwa nina ugomvi nao wa zaidi ya miongo miwili.
Person vendetta dhidi yangu, Hii vendetta ni neno la kiitaliano lenye maana ya Chuki.
Hawa watu wamekuwa na chuki dhidi yangu ndio wameleta hao mashahidi waje kunitolea ushahidi wa uhaini.
Waheshimiwa Majaji ushahidi wa Shahidi Na. 1 na Na. 16 PW1 na PW 16, ni ushahidi muhimu sana.
Sio kwamba una uzito lakini ni muhimu unaonesha aina ya ushahidi ulioletwa.
PW 1 George Bagyemu (ukisikia PW jua ni Prosecution Witness) alisema kwenye ushahidi wake kwamba, Yeye ndie aliyeongoza timu ya wapelelezi wa kesi hii kati ya Tarehe 04 April na Tarehe 08 April, 2025.
PW1 kwa maneno mengine alikuwa anaongoza upelelezi siku moja kabla sijakamatwa.
PW1 alisema kwenye ushahidi wake in chief na kwenye cross examination kwamba wakati anaongoza timu ya upelelezi kuanzia hiyo Tarehe and 04 alikuwa anawasiliana moja kwa moja na DCI Kingai kwa kupitia Ramadhani Ng'azi Deputy Commissioner of Police.
Kwenye Cross Examination nilimuuliza kama aliwahi kuwasiliana hata mara moja na ZCO ambae ni Boss wake akasema hapana.
Akasema pia hajawahi kuwasiliana na office ya DPP kwasababu huyu ndie anaratibu upelelezi wa jinai akasema HAPANA.
Nilimuuliza kama amewasiliana Regional security officer amewahi kuwasiliana nae? Akasema Hapana. Kwamba mkuu wa usalama wa mkoa alisena hajafanya hivyo.
Mtu aliyekubali aliwasiliana nae ni DCI Ramadhani Kingai kupitia kwa DCP Ramadhani Ng'anzi.
PW1 alisema aliunda timu tatu za Upelelezi. Ambazo ni 1. Operesheni, 2 inteligentsia na 3. ushauri.
Kwenye hizo timu 3 timu ninayotaka kuitolea ushahidi ni timu Oparesheni ambayo alisema ilihusika na ukamataji. Nilimuuliza ni wewe ndio uliyeamuru nikamatwe akasema Hapana yani Kiongozi mkuu wa upelelezi hafahamu nani aliyeamuru nikamatwe.
Ilikuwaje nikakamatwa? Akajibu kuwa alipigiwa simu na DCP Ng'anzi kuwa mtuhumiwa amekamatwa Mbinga na analetwa Dar es salaaam.
Kumbuka yeye anasema ndie mpelelezi mkuu wakati huo, sasa Waheshimiwa Majaji huyo aliyetoa taarifa kuwa nimekamatwa ni yule ambae alikuwa ni kiunganishi kati yake na DCI Kingai na presumably na IGP Wambura.
Sasa ni ushahidi wangu kuwa nilikamatwa kwa amri ya KINGAI DCI na Presumably na IGP Wambura ndio walioamuru nikamatwe na ndio walitengeneza kesi sio hawa hapa anamuonesha Katuga.
Na hawa akina Kingai miaka 24 iliyopita wamekuwa kwenye Mkakati wa Kunifunga. Wameshindwa siku zote. Waheshimiwa Majaji hayo aliyoysema PW 1 yalithibitishwa substantially 16 aliyathibitisha ACP Amin Mahamba.
Mashahidi wengine ni PW2, PW 3, PW 6, PW 9, PW 12 na PW 15. Ushahidi wao kwa ujumla wao ni ushahidi wa watu wa Ramadhani Kingai na Camilius Wambura.
Maafisa wa Polisi ambao wakubwa wao wamekuwa na mkakati wa kunifunga kwa miaka 24. Mtakapofanya majumuisho ya ushahidi huu na wa namna hii hauna thamani yoyote.
Ni ushahidi wa mashahidi wenye maslahi unahitaji kuwa corroborated na ushahidi huru.
Nataka kusema ndio ushahidi tulionao na nitaileta baadae.
Sasa nizungumzie ushahidi wa mashahidi wasiokuwa Polisi. PW4, PW 5, PW7, PW 8, PW 10, PW 11, PW13 na PW 14. Hawa ndio mashahidi ambao hakuna anayewajua isipokuwa prosecutor.
Mashahidi wote hawa tuna maelezo yao ya maandishi na maelezo yao ya midomo wakiwa hapa Mahakamani. Isipokuwa PW 1 ndio hatuna ushahidi wake wa maandishi ila wengine wote tunao.
Sasa nirudi kwa mashahidi wa kificho ukimwachia PW 4 wengine wote 7 walisema hivi kwa maandishi na wakiwa kizimbani hapa.
Part 279 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 279
Mhe. Lissu anaendelea kutoa utetezi wake.
1. Walipanga njama za kufanya uhalifu wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka jana. Wote walisema hivyo kwa maandishi hawa mashahidi wa siri na maelezo hayo yaliandikwa Polisi. (Kupiga watu, kuchoma vitu) ni wao walisema hayo. Na ushahidi huo uko hapo mko nao.
2. Wote hao isipokuwa PW4 walikamatwa na Polisi kwa kufanya njama hizo kwa kufanya fujo na wote walikamatwa kwa hizo siku nne yaani Tarehe 04 na Tarehe 08 April. Polisi waliwajua na kuwakamata wote within four days.
3. Mashahidi wote hao baada ya kukamatwa na Polisi wali confess. Walikiri kuwa tunapanga kufanya vurugu kwenye Uchaguzi, wakiwa kizimbani walisema kwamba walipanga kufanya uhalifu tena walikiri hivyo kwa maandishi
4. Mashahidi ambao walikamatwa kama watuhumiwa wote waliachiwa ili waendeleee kupanga njama yani unamkamata mtu kwa uhalifu na unamuachia.
5. Wote waliitwa na Polisi PW 16 Amin Mahamba na kuwambia kubalini kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu na mkikubali tutawafutia mashitaka.
Wahalifu wamekiri mbele ya Polisi, Wakaachiwa na kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu.
6. Wahalifu hao self confessed walitoka Dar es salaam na Dar es salaam Oktoba walikufa watu 182 kwa mujibu wa Jaji Chande.
PW 10 and PW 11 Walitoka Arusha na Arusha walikufa watu 53 kwa mujibu wa Jaji Chande. PW13 na PW 14 walitokea Mbeya na huko waliuawa watu 80 kwa mujibu wa Jaji CHANDE. (Polisi walikamata watu waliosema wamepanga kufanya uhalifu Oktoba na wakawaachia na hiyo Oktoba ukatokea huo uhalifu watu hao wakiwa uraiani.) Pw 5 na Pw 7 walitokea Songea na Jaji Chande anasema huko nako walikufa watu ila hawakutaja idadi ya waliokufa Songea.
PW 16 Amin Mahamba alisema alikuwa kwenye timu ya wapelelezi walioyachunguza mauaji ya Oktoba 29 na nikamuuliza hao waliosema walipanga kufanya fujo Je mliwachukulia hatua yoyote kwasababu machafuko yalitokea? Akajibu kuwa HAPANA, hakuna hatua walichukua.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa wahalifu wa aina hii una uzito gani KISHERIA?
Huu ndio ushahidi wa Serikali dhidi yangu.
Ushahidi wa wahalifu waliokiri tutafanya uhalifu wakaja Mahakamani wakakiri. Wakarudi walikokuwa wanapanga na baadae watu wakauwawa wengi huko mitaani. Ushahidi wa aina hii una uzito gani kwenye kesi ya uhaini?
Mashahidi wa aina hii ni totally unreliable. Nitaleta kwa maandishi hoja hizo za kisheria.
Waheshimiwa Majaji shitaka linasema nilitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nikathibitisha nia hiyo kwa kutamka yale maneno maarufu.
Anatizama juu Mwenyekiti Lissu na kuonesha hawa watu ni wajinga sana. Ngoja tusikie ataendeleaje hapo.....kuna kaukimya kidogo. 😂
Sasa Waheshimiwa Majaji kuhusiana na shitaka hili na kwa mujibu wa maamuzi ya kisheria tuliyozungumza sana kitu cha muhimu ni uwepo wa nia ya kutenda kosa la uhaini.
Ushahidi wa Jamhuri unasemaje kuhusu hiyo nia ya kutenda kosa la uhaini? Mashahidi waliotoa ushahidi kuthibitisha hoja hii ni hawa wafuatao.
PW1, PW2, PW16 na PW17 ambae ni P yule mwandishi kwa ridhaa yenu naomba nipatiwe exhibit D1, D15 na D16.
Kimya kidogo kinapita.
Majaji wanaandika na hizo exhibit zinatafutwa.
Ushahidi wa PW 1 George Bagyemu Msaidizi wa Mafwele kuhusiana na nia ya kutenda kosa la uhaini inayodaiwa katika hati ya mashitaka kwenye ushahidi wake alisema kwamba mimi nilitengeneza nia ya kuitishia serikali.
Aliona nia ya kutenda kosa la uhaini katika kauli niliyotoa. Nia aliiona kwenye maneno yeye.
Waheshimiwa Majaji shahidi mwingine aliyeona nia hiyo ni PW 16 Amin Mahamba. Waheshimiwa Majaji Exhibit D15 maelezo yake Polisi alisema huyu Mahamba akasema hivi
"Mimi pamoja na timu nzima ya upelelezi tuliitizama na kuiskiliza video hiyo tukabaini kuna kosa la uhaini na kuchapisha taarifa za uongo."
Part 280 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 280
Anasimama Wakili wa Serikali Katuga anasema huu ni utetezi na kielelezo hiyo kilipokelewa kama kielelezo D.
Kinapokelewa kuonesha contradiction na kuanza kukirejea kama kielelezo cha kawaida. Kitakuwa na kinyume cha kifungu cha 163 kipo for specific purpose na mkiruhusu tutakitumia dhidi yake. Kitakula pande zote mbili, tunaiomba Mahakama irudi kwenye hiyo purpose ya kukipokea hicho kielelezo.
Jaji Ndunguru anaandika
Mh. Lissu anacheka ngoja tusubiri majibu ya Lissu hapa.
Mhe. Lissu anasema sasa mimi niseme kuwa kwao kama ni furaha mimi kukitumia nataka iwe furaha.
Mimi sina shida na wao wayatumie tu, Kielelezo kinahusu kesi hii na Mahakama lazima ikisome ikiangalie.
Hamna kielelezo kinachukuliwa kwa ajili ya cross tu peke yake, Waheshimiwa nakitumia kwa sababu kinahusu kesi.
Sasa kwa vile wamesema ni furaha yao nashangaa kwanini wanalalamika. Mimi nilikiingiza makusudi ili na wao wakitumie, nashangaa tena hawataki.
😂😂😂😂 Watu wanacheka hapa.
Kumuelewa Katuga unapaswa kuwa umerogwa au huna akili hata kidogo.
Majaji wanateta hapa kama dakika 5 sijui nao wana shida gani huko.😂 haya ngoja tuone.
Jaji Ndunguru ameteta na wenzake kwa muda mrefu sana. Halafu huwa ana tabia sana ya kuzungumza na huyu Jaji Karyemaha kwa muda mrefu sana. Sijui huwa anaongea nae nini? Huyu Jaji Kiwonde ambae yuko kushoto kwa Ndunguru yeye ni kama huwa hana habari kabisa.
Jaji Ndunguru anasema kwa vile kielelezo kimeingia hatuwezi kusema tunazuia matumizi ya hicho kilelezo. Kwahiyo wewe endelea tu, kelelezo tayari kipo Mahakamani we kitumie.
Mhe. Lissu anasema sawa naendelea.
Amin Mahamba amesema kuwa mimi pamoja na timu tulitazama video na kuona makosa ya uhaini na kusambaza taarifa za uongo.
Kwahiyo PW 16 aliona nia ya kutenda kosa akiwa na PW 1 hawa waliona nia.
PW2 na PW 17 Je waliona nia?
Waheshimiwa Majaji kwa mujibu wa kielelezo D1 John Kaaya anasema katika picha mjongeo niliona Tundu Lissu akitamka matamshi yenye viashiria vya jinai.
Hakuna mahali kokote alipozungumzia uhaini, kosa la uhaini na nia ya uhaini.
Aliona viashiria vya jinai.
PW 17 anasema kwenye maelezo yake anasema hivi. Katika mkutano huo masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni masuala kuhusu Uchaguzi Mkuu na agenda yao ya No reforms, No election na matatizo yao wanayokumbana nayo kwenye Uchaguzi. Huyu yeye hakuna uhaini aliouona hata mmoja.
Anasema alituona tunazungumzia No Reforms No Election na Matatizo tunayokumbana nayo, hakuna uhaini aliousema kabisa.
PW 17 ndie shahidi pekee aliyekuwepo kwenye mkutano na hakuona kosa lolote wala uhaini.
Hoja ya pili inayogombaniwa kwenye kesi hii ni manifestation ya hiyo nia. Maneno ni haya wanasema kitu kimoja hapa, msimamo huu unaashiria uasi ........ anayasoma yote.
Yanayodaiwa kusemwa ndio maneno hayo.
Sasa ushahidi unasemaje kuhusu haya maneno?
Kuhusiana na hayo maneno, ushahidi wa PW1, PW2 na PW 16 unafanana na mashahidi wote hao wanasema kuwa waliona hiyo video yenye maneno hayo.
Na ushahidi wao wamesema mimi ndie niliyechapisha na kuyapeleka Jambo TV. Ushahidi wa PW 17 the eye witness unasemaje?
Shahidi Na. 17 wa upande wa mashitaka kwenye maelezo yake D16 anasema hivi katika mkutano huo masuala yaliyokuwa yakiongelewa ni kuhusu uchaguzi mkuu na mambo ya No Reforms No Election.
Hakuna kokote kwenye D15, hakuyaona hayo maneno hakuyasikia, hajayaandika wala hajayasema hapa. Aliyekuwepo hajayaona, hajayasikia kwasababu hajayaandika na hajayasema.
Angeyasikia angesema, angeyaona angeyaandika.
PW17 alisema hapa Mahakamani na iko kwenye D16 kwamba yeye ndio alipiga picha na kurusha akiwa na wenzake wanne wakitumia camera za SON. Wote ni wafanyakazi wa JAMBO TV. Walirusha mkutano huo ukiwa Live.
PW17 alisema kwa maandishi na hapa Mahakamani pia kuwa yeye ndie aliyehifadhi hizo video kwenye mtandao wa Jambo kule Youtube, X na instagram. Alisema yeye sio mimi.
Part 281 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.