Mtandao wa X umeanzisha mabadiliko mapya yanayowalenga watumiaji wasiokuwa na alama ya uthibitisho ya Blue Badge, katika jitihada za kuimarisha usalama na kudhibiti matumizi mabaya ya akaunti.
Kupitia mabadiliko hayo, idadi ya machapisho ambayo mtumiaji anaweza kuchapisha kwa siku yamepunguzwa hadi 50 pekee, kutoka 2,400.
Aidha, idadi ya maoni (comments) ambayo mtumiaji anaweza kutoa kwa siku imewekwa kuwa 200, ikilinganishwa na 2,400 za awali.
Uongozi wa X umeeleza kuwa hatua hizo zimechukuliwa ili kupambana na akaunti zinazojihusisha na vitendo visivyo halali pamoja na kupunguza usambazaji wa maudhui yanayoweza kuvuruga matumizi ya jukwaa hilo.
Pia, kampuni hiyo inalenga kuongeza idadi ya watumiaji wenye Blue Badge kwani wanaolipia huduma hiyo hutakiwa kutoa taarifa zao binafsi pamoja na nyaraka za utambulisho, jambo linalorahisisha kuthibitisha uhalisia wa watumiaji.
#KitengeUpdates