VIDEO:
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi.
Rais wa TEC na Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, amesema kuwa amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutumia nguvu bali kwa maridhiano na haki, akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani ya nchi kwa kuhakikisha mifumo ya uchaguzi inarekebishwa ili kutoa nafasi kwa upatikanaji wa viongozi wa haki na wa kweli.
“Katika hali ya kawaida, nani anaharibu amani? Anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule anayesema ‘jamani turudi mezani ili tuangalie mifumo yetu ya uchaguzi kwani mifumo ya sasa haiwezi kutupatia viongozi wa haki na kweli’?” amehoji Askofu Pisa.
Akizungumza katika mkesha wa Pasaka uliofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Kagwa, Jimbo Katoliki Lindi, Askofu huyo amesema kuwa kama kurudi mezani ndiko kunakoweza kulinda amani, basi kila anayehamasisha hilo anapaswa kuungwa mkono, si kukandamizwa au kukamatwa.
“Kwa maana hiyo wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti, na wengine wasikamatwe wala kusumbuliwa. Pia mihimili isiingiliwe bali itende kazi zake kwa haki,” amesisitiza.
Amesema kuwa amani ni tunu adhimu inayopatikana kwa gharama kubwa, hivyo haipaswi kuchezewa, huku akisisitiza kuwa taifa linapaswa kuikataa dhana ya kuimba wimbo wa amani isiyotokana na haki.
Kauli ya Askofu Pisa imekuja wakati ambapo mjadala wa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na ushiriki wa vyama vya siasa umekuwa ukitawala anga ya kisiasa nchini, huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu kukamatwa kwa viongozi wao wakubwa akiwamo Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu @TunduALissu , na ukosefu wa haki katika uendeshaji wa siasa.
@Mwanahalisitz Haki ndiyo inaanza , ukipora haki za watu unaondoa amani yao! Vyema chama cha mapinduzi kikahubiri haki na kuiishi haki. Mbali na kuondoa aman pia inasababisha chuki kati ya kundi fulani na kundi lingine! Kwa sasa wapo watu wengi tu ambao wana chuki na hasira dhidi uovu unaoendel
Msome Baba Askofu Dkt. Benson Bagonza, Mkuu Wa Kanisa La KKKT Dayosisi Ya Karagwe.
Mama unasoma huu ujumbe? Tumekueleza Muda mrefu sana unahujuimiwa. Au, umeamua kuibomoa nyumba yako kwa mikono yako mwenyewe na kurudi Kizimkazi mapema…
Kwanini vijana wa @ACTwazalendo wanashambulia zaidi Chadema kuliko CCM?
Wanaiogopa au wanaihusudu CCM?
Malengo yao ya kisiasa ni kupambana na Chadema au hawajui malengo yao?
Ni mpango wao wa kichama au wanajiongoza tu wenyewe?
Je! ACT ni Satelite party cha CCM.
Nauliza.
NEMO DAT QUOD NON HABET. Maana yake huwezi kutoa usicho nacho. Mdimu hauwezi kuzaa embe wala mama-yoka hawezi kuzaa kuku, ingawaje mayai anataga. Asiye na maadili hawezi kusimamia maadili ya wengine. Taasisi zilizooza haziwezi kusimamia lolote la afya kwani uoza kuzaa mafunza.
BAGONZA:KUIBA KURA NI UHAINI MAANA UNAPINDUA MADARAKA YA WANANCHI
“Kuiba kura ni uhaini kwa sababu unapindua madaraka ya wananchi. Tunazo serikali nyingiiii barani Afrika zilizoiba kura na zinalaani wizi wa kura.Kukalia kimya wizi wa kura, kuwezesha wizi wa kura, kukubali matokeo ya wizi wa kura ni uhaini. Uwiiiii, hata mimi ni mhaini maana nami nimo humu”-Askofu Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe
#TANZANIA:BAGONZA:ALIYESINGIZIA EBOLA KAVUMILIWA ALIYESEMA TUTAKINUKISHA MNAMUHUKUMU
“Yule pale kasingizia kuna Ebola na M-pox, akavumiliwa kwa sababu magonjwa hayo hayapo. Aliamka vibaya siku hiyo au alisahau kumeza dawa.Huyu kakurupuka, “tutakinukisha na mashindano ya kujaza fomu hayatafanyika”. Mvumilie naye mlivyomvumilia yule. Kwani mashindano ya kujaza fomu yameishakwama? iAu mnahukumu nia? Wahukumuni wote basi”-Askofu Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe
TANZIA: Mwanasiasa mkongwe Tanzania, Prof. Mwesiga Baregu, amefariki dunia, usiku wa kuamkia leo Jumapili, Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu. Familia imethibitisha. Enzi za uhai wake, alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Ninavyojua, kimila, msisitizo uliwekwa kwenye uwezo wa mwanamume kuhimili mihemko yake badala ya nguo za mwanamke. Kwa nini wanaume wa siku hizi hupenda kuwaamulia wanawake nguo zao badala ya kushughulikia udhaifu wao wa kujitawala.
Kitendo tu cha kuthibiti bunge, mahakama, vyama vya upinzani na vyombo vya habari kilitosha kumshitua kila mwenye akili kwamba huu sio uelekeo sahihi wa kujenga Taifa.
Asante sana Kaka