Kesho kikosi cha Simba kinarud Dar es salaam saa 4 asubuhi na Parade la ubingwa litaanzia pale Airport Terminal Two, kupitia Tazara, buguruni, karume then kigogo sambusa, watapitia Jangwani watakaa masaa matatu kisha wataenda Msimbazi hadi Final Coco Beach.
Ahmed Ally
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars hatimae kwa mara ya kwanza katika historia inafuzu kucheza hatua ya 16 bora ya AFCON 2025 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia.
Tanzania anafuzu kama best looser akiwa ameambatana na Timu zingine zilizofuzu kama best looser ni Msumbiji, Benin na Sudan.
Angola alikuwa anaiombea Tanzania ipoteze leo ili apate nafasi ya best looser ila sasa wamefungana kwenye alama 2 na Tanzania na utofauti wa magoli -1 ila Tanzania anafuzu kwa kufunga magoli mengi 3 dhidi ya Angola aliyefunga mawili.
Hii ni mara ya nne Tanzania inashiriki AFCON 1980, 2019, 2023 na hizo zote ilikuwa inaishi makundi, sio mbaya kwenda kama best looser hata Bingwa mtetezi (Ivory Coast) alienda kama best looser 2023 😂
#MillardAyoUPDATES
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina🙏
Raila Odinga was a true champion of democracy. A child of independence, he endured decades of struggle and sacrifice for the broader cause of freedom and self-governance in Kenya. Time and again, I personally saw him put the interests of his country ahead of his own ambitions. Like few other leaders anywhere, he was willing to choose the path of peaceful reconciliation without compromising his core values. Through his life, Raila Odinga set an example not just for Kenyans, but across Africa and around the world. I know he will be missed. Michelle and I send our deepest condolences to his family and to the people of Kenya.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga amefariki dunia katika Wilaya ya Kerala Nchini India akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati akiwa anafanya mazoezi katika matembezi ya asubuhi.
Vyombo vya Habari Nchini Kenya na India vimeripoti kuwa Odinga alikuwa Nchini India kwa matibabu kwa zaidi ya siku tano sasa na alipata shambulizi la moyo kufeli ghafla akiwa ameambatana na Mtoto wake wa kike na Dada yake.
Raila Odinga alizaliwa January 7, 1945 na alikuwa Waziri Mkuu wa Kenya kutoka mwaka wa 2008 hadi 2013 lakini pia amewahi kuwa Mgombea Urais nchini humo aliyeungwa mkono na Wafuasi wengi.
Kabla ya kuwa Waziri Mkuu alikuwa Mbunge wa Langata kuanzia 1992 hadi 2007 kisha akahudumu kwenye Baraza la Mawaziri la Kenya kama Waziri wa Nishati kuanzia 2001 hadi 2002 na baadaye kama Waziri wa Barabara, kazi ya umma na makazi kuanzia 2003 hadi 2005 na kisha akateuliwa kuwa Mwakilishi wa juu wa maendeleo ya miundombinu katika Umoja wa Afrika mwaka wa 2018. #MillardAyoUPDATES
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga, January Yusuph Makamba anatarajia kuongea na Wananchi wa Bumbuli leo Jumatatu September 08,2025 hii ikiwa ni mara ya kwanza kwake kuongea nao tangu CCM ilipokata jina lake na kumpitisha Eng. Ramadhani Singano kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo hili.
January anatarajia kuongea na Wananchi wa Bumbuli katika mkutano unaofanyika katika Kijiji cha Kweminyasa Kata ya Mponde ambapo tayari Wananchi wameanza kukusanyika kwa wingi ili kumsikiliza.
January amekuwa Mbunge wa Bumbuli kwa miaka 15 tangu aliposhinda uchaguzi wa mwaka 2010 na amehudumu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa Waziri wa Nishati na Waziri wa Mambo Nje ambapo kwa sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Klabu ya Yanga Eng Hersi Ally Said amesema klabu hiyo haikuwa tayari kumuuza mshambuliaji, Clement Mzize licha ya kupokea ofa nyingi kwa kuwa klabu hiyo sio kituo cha kukuza vipaji na kuuza bali ni timu inayohitaji wachezaji wazuri ili kushinda mataji.
Aidha akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 2025 kwa klabu hiyo Eng. Hersi amesema nyota huyo amebaki sio kwa kumfanyia ukaidi au roho mbaya bali klabu imekaa naye chini na kumuongezea maslahi yake na sasa Mzize ndiye mchezaji anayelipwa ghali zaidi klabuni hapo.
#KitengeSports