@Sirajitz1 Yanga yoyote anakaa bench, umesahau chama alikaa benchi? aziz ki alikaa bench? Mayele alikaa benchi? yanga hta aje mesi akitkiw akae bench anakaa tu..uyo zmbwe hmn mechi kaanza boka kakaa bench? Io sio simba na miktba ynu ya mchzj lzm achze mechi zote kma alivotaka chama
Takribani mwaka mmoja baada ya kifo cha Mumewe, Mwanamke mmoja aitwae Kouri Richins wa Utah, Marekani alichapisha kitabu kilicholenga kuwasaidia Watoto wake watatu kukabiliana na huzuni ya kumpoteza Baba yao lakini mwezi mmoja baada ya kuandika kitabu hicho Mwanamke huyo alikamatwa na kushtakiwa kwa madai ya kumuua Mumewe huyo waliyeishi miaka 9 kwa kumlisha sumu mwaka 2022 kwa nia ya kupata faida ya kifedha ya BIMA yake ya maisha na kuanza maisha mapya na Mwanaume wake mwingine ‘Mchepuko’.
Kesi ya Kouri (35) ambaye pia anadaiwa kujaribu kumtilia sumu Mumewe siku ya Valentine, wiki chache kabla ya kifo chake inaendelea ambapo amekana mashtaka ya mauaji ya kukusudia, jaribio la mauaji ya kukusudia, udanganyifu wa bima na kughushi nyaraka ambapo kwa mujibu wa sheria anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha jela endapo atapatikana na hatia katika shtaka kubwa zaidi ambapo pia anakabiliwa na mashtaka mengine ya kifedha katika kesi tofauti.
Mumewe Eric Richins (39), alikutwa amefariki dunia ndani ya chumba chao alfajiri ya tarehe 4 Machi 2022 ambapo usiku wa jana yake Mkewe alipeleka vinywaji (cocktails) chumbani kwao kusherehekea mafanikio Mume huyo aliyopata katika biashara yake ya Real Estate ambapo baadae Kouri alilazimika kwenda kulala kwenye chumba cha Mtoto mmojawapo aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya na aliporejea katika chumba chao alimkuta Mumewe akiwa amefariki kitandani.
Ilielezwa kuwa Eric aliwahi kuwaambia Rafiki zake wawili kuwa alihisi kama Mke wake alijaribu kumuua kwa kumuwekea sumu kwenye sandwich ambapo kwa upande mwingine uchunguzi umeonesha kuwa Kouri alifuta zaidi ya MSG 800 kwenye simu kuanzia Januari hadi katikati ya Machi 2022 huku historia ya intaneti yake ya simu ikionesha kuwa alitembelea tovuti kutafiti kuhusu gereza la Wanawake la Utah, malipo ya bima ya maisha na jinsi polisi wanavyopata data zilizofutwa kwenye simu.
Uchunguzi mwingine umebaini kuwa alimuua Mumewe ili kupata faida kutokana na biashara yake yenye mapato makubwa na sera zake za bima ya maisha, fedha ambazo angeweza kutumia kuendeleza biashara yake ya Real Estate iliyokuwa ikikabiliwa na changamoto. #MillardAyoUPDATES
“Tathmini inaonesha kuwa wananchi walio wengi wanaridhishwa na utendaji wa serikali katika kutekeleza programu na miradi ya maendeleo. Kwa mfano, utafiti uliofanywa na Taasisi ya Afrobarometer mwezi Juni – Julai 2024 ulionesha kuwa asilimia 71 ya wananchi waliohojiwa walisema wanaridhishwa na utendaji wa serikali, na asilimia 70 walisema nchi ipo katika mwelekeo sahihi. Hii inaonesha kuwa wananchi walio wengi wanaridhishwa na utendaji wa serikali yao” - Prof. Kitila.
Sehemu ya hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26, bungeni jijini Dodoma, Alhamisi Juni 12, 2025