(✍🏻 mwandishi wetu wa Dar Es Salaam)
IMETOSHA SASA! Hivi ndivyo ambavyo tunaweza kusema na serikali ielewe kuwa watanzania wanataka ukweli na uongo na ubabaishaji sasa hauna nafasi tena.
Kwani kuna ugumu gani kwa serikali kukiri kuwa ni lazima wamama waja wazito wawe na hela ili kupata huduma za kujifungua? Kuna ugumu gani kuwaaambia watanzania kuwa huduma za afya siyo bure ni lazima kulipia? Kuna ugumu gani kuweka hilo wazi ili mtu anapompachika mkewe mimba awe anajua kabisa kuwa siku ya kwenda kujifungua lazima awe na hela ya kulipia ili kupata huduma.! Kuna ugumu gani kufanya hivyo?
Yaani haiwezekani nchi nzima na vituo vyote vya afya na mahospitali wawe hawajui kama huduma za kuzalisha wamama ni bure na wakafanya kinyume na agizo hilo la serikali. Haiingii akilini kila siku tunasikia matukio ya namna hii yanatokea nchini na bado tunakuja kudanganya watu na kauli za waziri wa afya kuwa sijui anaunda tume mara waziri Mchengerwa naye anasimamisha watu kazi na blah blah za hivyo. Hivi mnataka mpaka nani afe ili muweze sasa kusema ukweli kuwa huduma za wamama kujifungua siyo bure kama mnavyosema?
Haya mambo yanatia uchungu sana na kwa kweli tufike mahali tuwaambie watanzania kuwa huduma za afya siyo bure na wanatakiwa kulipia kuliko kusema uongo na kuwadanganya watanzania na mwisho wa siku wanakutwa na majanga kama haya yasiyo ya lazima.
Mnawaonea sana madaktari na nyie serikali mnajua kuwa mnawaonea na wanachofanya kudai fedha ili kuhudumia wamama wajawazito ni maagizo yenu na miongozo yenu sasa mnapotaka watibu watu bure huku mna miongozo mmewapa kudai fedha kwa ajili ya matibabu ni kuwaonea.
Huyu Mbunge anaongea kwenye hii video sijui hata wamemruhusu kuja kufanya nini kwenye huu msiba kwa sababu anaujua ukweli na na yeye ni sehemu ya hili tatizo ,bado na huyu mwenyekiti wa CCM ndiyo hovyo kabisa na anaongea vitu havina hata mantiki. Hawa watu wa CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote haya na wamekuwa wanawafanya watanzania wajinga na hizi ngonjera zao kama mnavyowasikia hapa.
Kwa kuwa matukio haya yamekuwa mengi sana na yanatokea kila siku iendayo kwa Mungu ni wazi sasa chama cha madaktari Tanzania nimewekwa mfukoni na kinashindwa kutetea wanachama wao na vilevile kimefika bei ndiyo maana huwezi kuona wanatetea wanachama wao ambao ni madaktari wanaoonewa kwenyw matukio kama haya. Kiko wapi kile chama cha madaktari cha enzi za akina Dokta Ulimboka? Chama hiki kinajua kuwa serikali inatoa miongozo ya kuchukua kodi/tozo kwa wamama kujifungua sasa kwa nini wanakaa kimya wanapoona madaktari wenzao wanaonewa na kubebeshwa lawama na mizigo isiyo ya kwao?
CCM kwani kuna ugumu gani haswa wa kusema mmekwama na mmeishiwa mbinu za kutatua changamoto ndogo ndogo kana hizi? Yaani serikali yenu takatifu inawezaje kuagiza na kutoa miongozo wamama walipie huduma hizi halafu wakifa kwa kukosa hela mnaanza kuwapa lawama madokta?
Haya mambo mnayofanya nyie wizara ya afya mnamkwamisha sana mheshimiwa Rais Samia na kwa kweli dhambi hizi mnazochuma kuna siku mtakuja kuzilipa kwa kuwa machozi ya watu haya hazitaenda bure.
#KigogoMediaUpdates
@manoahwilliam@JaonathanM investment na kupata mapato bila kumpa burden mwananchi asilimia 100. ushabiki wako unaharibu reputation ya rais kwa wananchi wake
@manoahwilliam@JaonathanM kama unaujua uchumi ata wa kusimuliwa kuna source nyingi sana za kukuza uchumi nje ya tozo toka kwa wananchi tu. angalia resourses ambazo nchi inazo serikali ina fursa kubwa uya kupata mapato huko na kupungu ukali wa maisha ya wananchi wake. serikali pia inauwezo wa kufanya