Taarifa ya kumzuia wakili @MarthaKarua na Mawakili wengine kuingia Tanzania. Inathibisha udikteta ambao hata wakoloni hawakufikia, Mwl Nyerere aliposhitakiwa mawakili hawakuzuiliwa kuja kumtetea, viongozi wengi waliopigania Uhuru walitetewa na mawakili kutoka nje.
Hata Museveni hajamzuia Martha Karua na mawakili wengine kuingia kumtetea Kiza Besigye.
Nchi iko kwenye hali mbaya kuliko wakati mwingine wowote.
CHADEMA ni washindi ndani ya nyoyo za watanzania. CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa, imevuka sasa ni imani kubwa kwa watu. Hii ni leo. Mwakitolyo-Solwa na Shinyanga Mjini wamejitokeza kusikiliza elimu ya nzito yq #noreformsnoelection. Hiki ni chama tumepewa na Mungu. Tukilinde.
UKIAMINI kwamba chama cha siasa ni Ubunge, tena Ubunge wa Viti Maalum, huwezi kubaki Chadema. Tunawatakia kila la kheri. Mtarudi au mtafika mwisho wa safari yenu -CCM!
SOMENI BIBLIA .
Siyo kila Mamlaka inatoka kwa Mungu.Mamlaka zingine zinajiweka zenyewe.
Hosea 8:4
"Wamejifanyia wafalme, lakini mimi sikuwachagua; wamejifanyia wakuu, nami sikuwajua..."
Mathayo 4:8-9
"Kisha Ibilisi akamchukua Yesu mpaka mlima mrefu sana... akamwonyesha falme zote za dunia na fahari zake, akamwambia, 'Nitakupa haya yote ukianguka na kuniabudu.'"
KARAGWE
CHATO
GEITA
MWANZA
MUSOMA
SERENGETI
LAMADI
SIMIYU
BARIADI
MBEYA
LINDI
MTWARA
Yote imeenda hii, IMEENDA mapema kabisa
Hakuna namna hii imebaki
Kwa Kheri CCM kwa Kheri
Bado maeneo mengine yanayopitiwa yanapitiwa yatakwenda
‼️MAWAKILI WA SERIKALI MSITHUBUTU‼️
Tumepokea taarifa kuwa mawakili wa serikali (upande wa mashtaka) wamepanga kutofika mahakamani tarehe 19 kwenye kesi ya @TunduALissu ili kesi ishindwe kuendelea
Hii ni kwa sababu hawana hoja wala ushahidi
Hii njama imetufikia mapema na @judiciarytz ihakikishe njama kama hizi haziruhusiwi!
Tumetoa taarifa mapema mjue njama zenu zinavuja watu wamewachokeni!
#FreeTunduLissu
#FreeTunduLissuNow
Asante kanda ya ziwa nimejionea Nchi iko tayari kwa mabadiliko.
Asubuhi kabisa leo tumesalimiana na wananchi wa mtaa wa Sangai jimbo la Bariadi.
#NoReformsNoElection ndio jibu .
Ilipo hazina yako ndipo moyo wako ulipo.
Asanteni Watanzania sio jambo dogo ni upendo wa ajabu.
Tutailinda imani yenu kwa chama chetu.
#NoReformsNoElection
Polisi, tuwaulize kidogo. Kwamba mnaona wivu wananchi wakimsindikiza @HecheJohn kwenda kupumzika? Unajiuliza, nini sababu ya kutumia mabomu kutawanya watu ambao wanatembea kwa amani tu? Anyways, Musoma ilikuwa na VIBE na elimu ya #noreformsnoelection imefika na imeeleweka.
JOKA LA KAKI.
(Fasihi)
Msanii wa sanaa ya uchoraji wa picha fikirishi Masoud Kipanya ametupa jiwe la fikra kwenye bongo za wanafasihi,kila mwenye kutazama apate tafsiri kwa kadiri ya uwezo wa ubongo wake.
Mwalimu Boniface Jacob nimetafsiri hivi;
1.Joka la Kaki - hiki ni chama cha siasa kinacho vaa sare zenye rangi ya kaki kombati nchini Tanzania.
2.Ukubwa wa Joka- Ukubwa wa hicho chama katika siasa za Tanzania na uwezo wake kukabilina na changomoto za mazingira ili kuishi
3.Urefu wa Joka- ni mtandao wa chama kuenea kila semehu (mjini na vijijini) kama ishara za ukongwe wake katika siasa za Tanzania.
4.Wingi wa Vizuizi na Vigingi- Changomoto anazokutana nazo Joka (chama) za kila aina na nyingi za kutosha.
5.Kuchomoza kwa kichwa- kupenya na kufanikisha mitego na vizuizi alivyowekewa ili kukwama na kushindwa kupita lakini Joka la kaki (chama) kimepita.
6.Ubutu wa vizuizi - ni dalili kuwa siyo miti ya kawaida ya mstuni au porini bali ni vizuizi vya kutengeneza na binadamu siyo vya asili.Vizuizi hivyo ni ishara kwamba vinatangenezwa na wapinzani na maadui wa joka la kaki ili kulikwamisha.
7.Ulimi mrefu upo nje- ni ishara kuwa joka lipo makini katika kunusa hatari na kutafiti mipango ovu dhidi yake kabla haijamfikia karibu na kumdhuru na kugundua wasaliti na ku dili nao.
8.Macho ya Joka Kusinzia- yanaonyesha kusinzia kama ishara ya uchovu dhidi ya mapambano yale ya kujikwamua na kuhakikisha linahitimisha safari yake salama.
9.Vizuizi vingi kuwa kati na pembeni kuwa wazi- ni ishara kuwa joka lilikuwa na njia mbadala wa kupita kabla halijachagua hii yenye viunzi vingi kwa kupita pembeni.
Kupita kati kati ya vihunzi kunaweza kutafsirika kama uimara wa joka na likifanikiwa kuvuka litakuwa limeimarika zaidi kuliko lingeamua kupita pembeni kirahisi.
10.Ardhi ya Tambalale - ni ishara kuwa joka linakubalika zaidi kwa wananchi (ardhi) na kwamba wananchi hawana shida nalo.
Kama siyo vihunzi joka lingekuwa limefika mbali sana katika safari yake huko liendako kwa ushirikiano anaopewa na wananchi (ardhi).