Mzee Warioba ni hazina kubwa sana kwa Taifa https://t.co/EGKjZcHmx6 mtu mkweli,jasiri na muwazi.Katika Taifa lililojaa hofu ya utekaji na watu kuuliwa kama kuku ni nadra sana kuwapata wazee wengi wanaoweza kusimama na kuhesabiwa kama Warioba.
Kuna nguchiro wamechapisha namba yangu binafsi ya simu mitandaoni na kuanza kuhamasisha watu wanishambulie. Nataka kuwaambia huo ni upuuzi na ni uvunjaji wa Sheria.
Ukiondoa watu wachache sana wanatuma meseji za hovyo, asilimia 99 wananitumia meseji za kunitia moyo na kueleza utayari wao wa kuilinda nchi yao dhidi wenye nia ovu. Wale wanaoeleza changamoto za ajira na mitaji ninawapa majibu na nafikisha kwa wahusika zifanyiwe kazi.
Nguchiro na chawa wa nguchiro acheni kupoteza muda na rasilimali mkiporomosha matusi, tulieni na tuungane kujenga na kulinda nchi yetu.
Ripoti ya Tume iliyotolewa jana na Othman Chande ililenga kumsafisha Bi.Kizimkazi katika Jumuiya za kimataifa.
Tume imetumia pesa za Watanzania nyingi sana ili kusafisha mtu.Jambo la muhimu Chande ajue kwamba huyu mtu hasafishiki.Njaa ikiendekezwa inaondoa heshima ya wasomi wetu.
Ulikuwa mpambanaji usiyechoka wala kuyumba.Pia ulikataa unafiki,siasa uchwara za kidalali.Umeondoka ukiwa umetimiza wajibu wako wa kupigania haki,demokrasia na utawala bora.
Rest in eternal peace Seleman Bungara (Bwege).
Tundu Lissu amesema anaumwa lakini Jeshi la Magereza wamekanusha kwamba haumwi.
Kwa nini wanatumika vibaya na watawala kumnyima haki ya matibabu TAL?
Huu ubaya wanaofanya ni mkopo ambao watakuja kuulipa kwa riba kubwa wakati huo anayewatuma atakuwa anatumikia kifungo cha maisha.
Kuna watu walipotezwa kipindi cha utawala wake,wapo waliopigwa risasi na kuachiwa ulemavu kama Tundu Lissu kwa uonevu tu.
Pia wapo waliofilisiwa biashara zao na wengine kupelekwa jela.
Tusisahau waliokimbia nchi na kwenda ughaibuni.
Matendo yake yataambatana naye.
Hili goma la ICC halikwepeki hata iweje.Mungu yupo upande wa wenye haki siku zote.October 29,2025 ndugu zetu wengi sana wasiokuwa na hatia waliuawa.Wahusika wote wa mauaji watalia na kusaga meno very soon.
TAL ndo Rais wa Watanzania.Hupati shida kumtambua Rais wa watu maana unaona the way wanavyompokea kwa mizuka na bashasha.
Huyu ambaye ni zao la October 29 ni mharifu anayesubiri kwenda ICC tu kama ilivyokuwa kwa akina Bosco Ntaganda.
Habari nilizopata tangu jana usiku ni kwamba Award Kalonga ambaye ni Katibu wa Chadema Jimbo la Rungwe na mlinzi wa Tundu Lissu,yupo kituo cha polisi Mpemba wilaya ya Momba.
Sijui kwa nini Jeshi la polisi linamzungusha katika vituo vya polisi badala ya kumpeleka mahakamani.
Wakulima wameuziwa mbolea feki ya kupandia ya DAP iliyochanganywa na mchanga.Mazao ya mahindi yameharibika sana wilaya ya Mbozi.
Pia DAP iliuzwa Tshs.110,000 badala ya Tshs.76,000 bei ya ruzuku.CCM wameamua kufidia gharama za baiskeli na pikipiki walizogawa kwa makada wao.
Kwa kuwa Vodacom wanatumika na CCM kuna haja ya kuanzisha kampeni maalumu ya kuchoma moto line zao.
Huu ujinga wanaofanya hauvumiliki kwa namna yoyote ile.
Muasisi wa chama chetu cha Chadema Edwin Mtei umeondoka duniani ukiwa umetuachia chama imara kinachotimiza miaka 33.
Haikuwa kazi nyepesi kuacha ugavana Benki kuu ya Tanzania na kuanzisha chama cha siasa.
Umeacha alama isiyofutika mzee Mtei.
May your soul rest in eternal peace.
Siku hizi kuwashauri viongozi wa serikali hadharani ni chuki dhidi yao?
Kama hawataki kushauriwa waachie ofisi za umma.
Tatizo limeanzia pale mnapowatwisha viongozi wenye uwezo mdogo majukumu makubwa hivyo wanakurupuka tu.
Huu ndo unaitwa unafiki sasa kwa wale wasiojua.Kambambikizia kesi Lissu anayesota gerezani karibu mwaka unaenda kuisha,eti leo anadai kwamba anachukizwa na kesi za kubambikizwa.Kweli Novena inafanya kazi,tuongeze maombi.
Asanteni sana Mawakili wetu Phillip Mwakilima,Paul Kisabo na THRDC kwa Jitihada zenu.
Ndugu yetu Phillemon Mwakalinga Mwenyekiti wa CHADEMA Tawi la Majengo kata ya Mlowo alipata dhamana ya polisi juzi Dec 24,2025 jioni baada ya kukaa lockup Vwawa na Ileje kwa muda wa wiki 3.